
17/08/2025
Timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, waliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Chipolopolo ya Zambia kwenye mechi yao ya mwisho ya Kundi A CHAN 2024. Chipukizi Ryan Ogam aliendeleza makali yake kwa kufunga dakika ya 75 na kuipeleka Kenya kileleni mwa kundi.