09/01/2026
Muuguzi mmoja katika jimbo la Georgia ameripotiwa kurudishwa nyumbani bila kulipwa baada ya wagonjwa kulalamikia mtindo wake wa nywele uliokuwa mrefu na wa kipekee, aliouelezea kuwa una umuhimu wa kitamaduni kwake.
Kwa mujibu wa taarifa, wasimamizi wa hospitali hiyo walitaja mtindo huo wa nywele kuwa hauna taaluma (unprofessional) na pia kuwa hatari ya kiusalama katika mazingira ya kitabibu. Uongozi ulidai kuwa mtindo huo unakiuka viwango vya mavazi ya kazini na unaweza kuathiri taswira ya hospitali mbele ya umma.
Hata hivyo, muuguzi huyo alipinga vikali uamuzi huo, akisisitiza kuwa nywele zake hazikuwahi kuingilia utoaji wa huduma kwa wagonjwa wala hazikukiuka kanuni zinazolinda nywele asilia kazini. Aliongeza kuwa alizingatia usafi na usalama k**a wafanyakazi wengine wote wa afya.
Tukio hilo lililotokea mapema Januari 2026 lilienea kwa kasi mitandaoni na kugawanya maoni ya wananchi. Baadhi ya watu waliona mitindo mikubwa ya nywele k**a hiyo inaweza kuhatarisha usafi au usalama hospitalini, huku wengine wakitaja tukio hilo k**a ubaguzi wa wazi, wakirejea Sheria ya CROWN ya Georgia, inayolinda watu dhidi ya ubaguzi unaohusiana na mitindo ya nywele inayohusishwa na rangi au utamaduni.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, muuguzi huyo tayari ameajiri wakili na anatarajiwa kufungua kesi ya ubaguzi, huku mjadala ukiendelea kuhusu mipaka kati ya taaluma kazini na haki ya kujieleza kitamaduni.
Swali linaloendelea kugawa maoni ni:
Je, waajiri wake walikuwa sahihi kumrudisha nyumbani kwa kuzingatia usalama na taswira ya hospitali,,,,,,alaah jibu unalo
Picha Kwa hisani ya E.A news
media # kedu radio