Al Haajar TV Kenya

Al Haajar TV Kenya Fast growing || Islamic Media Channel || Coast region of Kenya πŸ‡°πŸ‡ͺ

11/01/2026

πŸ“ΊπŸ”΄: TALAKA KISA MKE MWENZA || USTADHA ABLA NAHIDA

09/01/2026

πŸ“ΊπŸ”΄: MAONI YA IJUMAA || MASJID LANDHIES NAIROBI || ALLAH NI MZURI ANAPENDA MAZURI

09/01/2026

KHUTBA YA IJUMAA – MASJID LANDIES, NAIROBI

Sheikh Ahmad Othman alikumbusha waumini kuwa Allah ni Mzuri na Anapenda Mazuri. Alisisitiza kuwa uzuri unaopendwa na Allah hauko kwenye muonekano pekee, bali uko kwenye imani, tabia njema na matendo mema.

Aliwahimiza Waislamu kuishi kwa usafi, uadilifu, lugha njema na Taqwa, wakiepuka dhulma, uongo na majivuno. Hitimisho lake lilikuwa wito wa kujipamba kwa Taqwa, kwani ndilo pambo bora mbele ya Allah.

Al-Haajar TV – Mwangaza kwa Ummah

©️ Al-Haajar TV Kenya 2026

ZIJUE SABABU ZA KUFUNGULIWA RIZKIKatika kipindi maalum cha Urunzi Yetu, jiunge nasi mubashara kwa mawaidha yenye kugusa ...
08/01/2026

ZIJUE SABABU ZA KUFUNGULIWA RIZKI

Katika kipindi maalum cha Urunzi Yetu, jiunge nasi mubashara kwa mawaidha yenye kugusa maisha halisi, yatakayowasilishwa na Sheikh Ramadhan Mwangi, Imam wa Parkroad Masjid. Sheikh ataeleza kwa kina misingi ya Kiislamu inayofungua milango ya rizki, ikiwemo kumcha Allah, dua, subira, juhudi halali na kuacha madhambi yanayozuia baraka.

Ni kipindi chenye lengo la kuamsha matumaini, kurekebisha mienendo ya maisha na kuwaongoza waumini kuelekea rizki yenye baraka kwa mujibu wa Qur’an na Sunnah. Usikose nafasi ya kujifunza na kujikumbusha kuwa rizki ya kweli hutoka kwa Allah pekee.

πŸ“… Alhamisi, 8 Januari 2026
⏰ 8:30pm – 9:30pm
πŸ“Ί Mubashara kupitia Al-Haajar TV
πŸ“² Pakua App ya Al-Haajar TV ufuatilie moja kwa moja

Al-Haajar TV – Mwanga kwa Ummah

AJALI MBAYA KERICHO | WATU KADHAA WAFARIKIWatu kadhaa wamefariki dunia kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyotokea kat...
06/01/2026

AJALI MBAYA KERICHO | WATU KADHAA WAFARIKI

Watu kadhaa wamefariki dunia kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyotokea katika eneo la Tunnel, kando ya barabara ya Londiani–Fort Ternan katika Kaunti ya Kericho. Ajali hiyo ilihusisha basi la abiria na lori, ambapo uharibifu mkubwa ulishuhudiwa na juhudi za uokoaji kuanza mara moja.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Kericho, James Ngetich, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo halisi. Tukio hili la kusikitisha linajiri wakati huu ambapo taifa linashuhudia ongezeko la ajali za barabarani, hasa wakati wananchi wakirejea kutoka mapumziko ya sikukuu.

πŸ“… Tarehe: 6 Januari 2026
πŸ“ Mahali: Tunnel, Kericho

Al-Haajar TV – Mwangaza kwa Ummah

©️ Al-Haajar TV Kenya 2026

29/12/2025

πŸ“ΊπŸ”΄: HAPPY NEW YEAR!!! || SHEIKH NURDEEN KISHKI

27/12/2025

SHEIKH KISHKI APOKEWA KWA BASHASHA NCHINI ETHIOPIA

27/12/2025

πŸ“ΊπŸ”΄: SHEIKH KISHKI APOKEWA KISHUJAA MOYALE YAZIZIMA ATOA KHTUBA YA IJUMAA YA MWAKA.

πŸ“‘ Inarushwa Mubashara kupitia Al-Haajar TV
🌐 www.alhaajar.tv | Pakua App ya Al-Haajar TV

Al-Haajar TV – Mwangaza kwa Ummah

©️ Al-Haajar TV Kenya 2025

Picha kwa matukio kutoka ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam πŸ“ΈMiski ya Roho 2025 imefunguliwa kwa mandhari ya kuvut...
27/12/2025

Picha kwa matukio kutoka ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam πŸ“Έ

Miski ya Roho 2025 imefunguliwa kwa mandhari ya kuvutia na yenye utulivu mkubwa, huku waumini kutoka maeneo mbalimbali wakimiminika mapema katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam. Masheikh na Viongozi wa kidini wakiwa tayari wamewasili, nyuso zao zikionyesha bashasha na unyenyekevu, wakijiandaa kuwasilisha mawaidha yatakayolisha na kuhuisha nyoyo za waumini.

Ukumbi umejaa hali ya subira, dua na matarajio makubwa ya kupata elimu yenye manufaa na ukaribu zaidi na Mwenyezi Mungu.

Ni mkusanyiko wa kiroho unaobeba uzito wake, ambapo sauti za tasbihi,Miski ya roho ni zaidi ya kongamano bali ni safari ya kiroho inayolenga kuamsha nyoyo, kuimarisha maadili na kuunganisha Umma katika nuru ya elimu na mawaidha ya kweli. ✨🀲

25/12/2025

Asanteni sana waumini wa Msikiti wa Quba Moyale kwa kujitokeza kwa wingi na kwa hamasa kubwa kumsikiliza dai wa kimataifa, Sheikh Nurdeen Kishki, katika muhadhara wake wenye mawaidha na elimu yenye manufaa.

Tunawashukuru pia kwa kufuatilia muhadhara huu uliorushwa mubashara (live) kupitia AlHaajar TV na N Kishki TV, hali iliyoruhusu waumini wengi zaidi ndani na nje ya Moyale kunufaika na ujumbe huo. Ushiriki wenu uliadhirisha mapenzi ya dhati kwa dini, ari ya kutafuta elimu, na mshikamano wa kiimani.

Mwenyezi Mungu awalipe kwa kheri tele na azidishe baraka katika jamii ya Moyale.

Al-Haajar TV – Mwangaza kwa Ummah

©️ Al-Haajar TV Kenya 2025

25/12/2025

πŸ“ΊπŸ”΄: HAIFAI MWANAMUME KUMPAMBA MWANAMKE || SHEIKH ALI BAHERO

25/12/2025

πŸ“ΊπŸ”΄: KOSA KUBWA MUME KUMPIGA MKE || SHEIKH ALI BAHERO

Address

Kenyatta Avenue
Mombasa
80100

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Al Haajar TV Kenya posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Al Haajar TV Kenya:

Share