30/09/2025
Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina, amevunja serikali inayoongozwa na Waziri Mkuu Christian Ntsay kufuatia maandamano ya vijana wa kizazi cha “Gen Z” yaliyosababishwa na ukosefu wa huduma za msingi k**a maji na umeme. Maandamano hayo yaligeuka vurugu na kusababisha vifo pamoja na majeruhi, huku Rais akiahidi kuunda serikali mpya itakayoshughulikia malalamiko ya wananchi.