
15/05/2024
“Football can be cruel sometimes…”
Matukio haya mawili yanafanana sana! Kwakuwa ni k**a kisu kikali kilichowakata maini na kuwakata tamaa mashabiki wa soka, wachezaji na makocha wao! Baada ya ile “save” ya karne kutoka kwa Kipa wa Argentina Emmy Martinez katika mechi ya kombe la dunia, hapo jana Steffan Ortega wa Manchester City nae alifanya “save” kubwa na muhimu sana katika mechi yao dhidi ya spurs!
Kwa wale wapenzi wa soka basi wanatambua kua save hii ya Ortega iliwaliza sio tu mashabiki wa Spurs kwa kukosa nafasi wazi ya kufunga goli bali pia iliwakatisha tamaa ya kutwaa Unbingwa wa Uningereza timu ya Arsenal!
Huu ulikuwa unyama mwingi kutoka kwa walinda lango hawa wawili!