15/12/2025
Quarter Finals | Zone B | Leg 1
Osanga Classic Cup inaendelea kuandika historia huku mashindano yakiingia hatua nyeti ya Quarter Finals – Zone B (Leg 1). Hapa, makosa hayaruhusiwi kwani dakika 90 za mwanzo zinaweza kuamua hatma ya kutinga Semi Finals.
Kwa ratiba rasmi, michezo yote miwili itapigwa saa sita kamili, katika viwanja vya Mirere na Itete.
Mirere F.C vs Munami F.C
📍 Mirere Grounds
Mechi ya presha na heshima. Mirere F.C wakiwa nyumbani wanategemea sapoti ya mashabiki wao, huku Munami F.C wakilenga kupata matokeo mazuri ugenini kuelekea Leg 2. Mapambano ya kati ya uwanja, nidhamu, na maamuzi ya haraka yanatarajiwa.
“Mambo itakua mbaya” — ni soka la kweli.
Besta F.C vs Blackstar F.C
📍 Itete Grounds
Hapa ni soccer santimaa. Timu zote zinapenda kushambulia na kucheza soka la kasi. Besta wanatafuta faida ya nyumbani, huku Blackstar wakitegemea nidhamu na uzoefu. Kosa dogo linaweza kugharimu tiketi ya Semi Finals.
“Mmoja lazima akate tiketi” — hakuna kurudi nyuma.
Saa Sita Kamili
Kick-off: saa sita kamili. Hakuna kusubiri, hakuna kuchelewa.
Leg 1 ni mwanzo wa vita — mwanzo unaoweza kubeba majibu mengi.
Osanga Classic Cup — mahali ambapo soka linaongea