Western Nyota 87.8 Busia Fm

Western Nyota 87.8 Busia Fm Western Nyota Busia Fm 87.8 Hits, is a leading in local languages Ateso and luhya in western kenya
(2)

Zaidi ya wanachama 50 WA kituo hiki Cha western nyota radio katika Kaunti ya  Busia wamenufaika na namna ya Kukabili tat...
06/08/2025

Zaidi ya wanachama 50 WA kituo hiki Cha western nyota radio katika Kaunti ya Busia wamenufaika na namna ya Kukabili tatizo la msongo wa mawazo pamoja na wadukuzi wa kimtandao.

Kulingana na mkurugenzi wa shirika la Dhamira moja cbo Sarah martha, ni kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwasaidia wananchi kuhimili matatizo yanayowasibu katika maisha yao ya kila siku.

Kauli yake imeungwa mkono na afisa wa miradi katika shirika Hilo Eunnita Nafula ambaye amesema kuwa mafunzo yao yatawawezesha wananchi kujilinda dhidi ya walaghai pamoja na mbinu za kuitunza afya yao ya kiakili Mitandaoni katika sehemu zao mbali mbali.

Wanachama walionufaika katika mafunzo hayo wakiongonzwa na mwenyekiti wa vyama vya western Nyota butula Joseph Kesa, wa matayos Moses Oduor, Usula Musundi na Praxides Auma wamewashukuru viongozi wa shirika hilo wakisema kuwa mafunzo waliopokea yatawasaidia kujiimarisha zaidi kwenye shughuli zao za kila siku.

WANAWAKE NCHINI WAMEOMBWA WAKUMBATIE UMOJA NA KUHUDUMIA WANANCHI KWA USAWA POPOTE WALIPOSPIKA WA BUNGE LA KITAIFA MOSES ...
04/08/2025

WANAWAKE NCHINI WAMEOMBWA WAKUMBATIE UMOJA NA KUHUDUMIA WANANCHI KWA USAWA POPOTE WALIPO

SPIKA WA BUNGE LA KITAIFA MOSES WETANGULA AKIWA KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA MIWILI YA KONGAMANO LA WANAWAKE WA MAGHARIBI ULIOFANYIKA KATIKA SHULE YA UPILI YA BUSIBWABO KAUNTI YA BUSIA, ,AMEWAHIMIZA WAMAMA KUDUMISHA UMOJA NA KUEPUKANA NA SIASA ZA UKABILA HUKU AKIOMBA WANANCHI KUWAHESHIMU KINA MAMA KILA ENEO

VIONGOZI HAO WAKIWEMO, MWAKILISHI WA KINA MAMA KAUTI YA BUSIA BI CATHERINE OMANYO,WA KAKAMEGA BI ELSIE MUHANDA,WA BUNGOMA CATHERINE WAMBILIANGA WAZIRI MKUU WA WIZARA YA MAZINGIRA DEBORAH MULONGO NA WENGINEO WAMEHIMIZA JAMII YA MULEMBE KUENDELEZA UMOJA WAKIELEZA KUWA HILO LITAWAHAKIKISHIA UWONGOZI MKUU KATIKA TAIFA HILI

WETANGULA NA DEBORAH WAMEOMBA WAKENYA KUMPA RAISI WILLIAM RUTO NAFASI YA KUENDELEA KUWAHUDUMIA K**A WATANGULIZI WAKE ILI AKATIMIZE AHADI ZAKE KWA WAKENYA

KINAMAMA WAMEIRAI SEREKALI KUU KUENDELEA KUSAIDIA KATIKA MIRADI YAO WANAOENDELEZA KWENYE VYAMA VYAO K**A NJIA YA KUJIKIMU MAISHANI HUKU WAKIMUSHUKURU RAISI WILLIAM RUTO KWA KUWAPUNGUZIA BEI YA MBOLEA

Western Nyota Salaams Club Members Empowered on Cyber Security and Mental Health AwarenessBusia, July 30, 2025 —Members ...
31/07/2025

Western Nyota Salaams Club Members Empowered on Cyber Security and Mental Health Awareness


Busia, July 30, 2025 —
Members of the Western Nyota Salaams Club today gathered for a crucial training session focused on Cyber Security and Mental Health Awareness, a timely and much-needed initiative aimed at empowering local business owners and community groups with knowledge to navigate the digital world safely and address growing mental health concerns.

The training, held in Busia, was organized by DHAMIRAMOJA Community-Based Organization (CBO) under the leadership of its Director Sarah Martha. The session was facilitated by Eunita, a mental health and cyber safety expert, who took participants through interactive discussions and practical strategies on digital protection and emotional wellness.

With the rise in online fraud, social media threats, and digital scams, Salaams Club members—who include small business owners and leaders of community savings groups (chamas)—were taught how to recognize cyber threats, protect their data, and create safe online environments for their businesses and families.

Beyond the digital sphere, the training also delved into the importance of mental health awareness, especially within grassroots communities. Participants were encouraged to normalize conversations around emotional wellbeing and support one another through mental health struggles.

A key highlight of the session was a passionate appeal to men in the community to speak out and seek help when faced with Sexual and Gender-Based Violence (SGBV)—an issue that remains largely unspoken among male victims due to stigma and societal expectations. The facilitators emphasized that vulnerability is not a weakness, and that healing begins with open conversations and community support.

Speaking at the event, DHAMIRA MOJA Director Sarah Martha stated:

“Our goal is to build resilient communities, not just economically, but also mentally and emotionally. We must ensure that as we grow our businesses and chamas, we’re also protecting our minds and our digital spaces.”

The event concluded with a commitment by the Salaams Club members to carry the message back to their networks, raise awareness, and become champions of both cyber safety and mental health support in their circles.

This initiative marks yet another milestone in DHAMIRA MOJA’s ongoing work to empower local communities through information, advocacy, and grassroots mobilization.

Western Nyota 87.8 Busia Fm

Zaidi ya shule 30 kutoka eneobunge la butula zimeweza kupata tarakilishi katika shule zao kutoka kwa mbunge wa eneo bung...
30/07/2025

Zaidi ya shule 30 kutoka eneobunge la butula zimeweza kupata tarakilishi katika shule zao kutoka kwa mbunge wa eneo bunge Hilo Joseph Oyula,

Akiongoza hafla iliyofanyika katika shule mbalimbali za eneo hilo, ikiwemo shule ya upili ya wasichana ya Buduma, lugulu AC , shule ya upili ya wavulana ya butula na Ile ya bukhalarire, Mbunge Joseph Oyula aliongoza zoezi la kupeana tarakilishi hizo kwa wanafunzi wa somo la tarakilishi huku akisisitiza umuhimu wa kujifunza teknolojia kwa maendeleo ya wanafunzi na taifa kwa ujumla.

Katika usemi wake oyula ameelezea kuwa ni muhimu kwa kila mwanafunzi kuelewa matumizi ya kompyuta na teknolojia akiwahimiza Wale ambao hawajasoma somo hilo kujiunga ili kuwa sawa na wenzao vilevile amewarai walimu wakuu wa shule kuhakikisha kuwa vifaa hivyo vinatumika ipasavyo kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi kuwa na maarifa ya kiteknolojia. Aidha akisisitiza kuwa elimu ya teknolojia itawawezesha wanafunzi kushindana katika ulimwengu wa sasa wa kidijitali.


Kwa upande wake, Vincent Wang, mmoja wa wadhamini wa mradi huo kutoka taiwan, alisema uhusiano bora kati yake na shule za Butula utaleta mabadiliko makubwa kwa wanafunzi kwani Ujuzi wa kompyuta .....

WITO UMETOLEWA KWA WANANCHI NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KAUTI HII YA BUSIA KUWEKA MIKAKATI JINSI WANAWEZA KU...
28/07/2025

WITO UMETOLEWA KWA WANANCHI NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KAUTI HII YA BUSIA KUWEKA MIKAKATI JINSI WANAWEZA KUKABILIANA NA TATIZO LA MSONGO WA MAWAZO DHIDI YA WANAHABARI KAZINI

AKIZUNGUMZA KATIKA MKAHAWA MMOJA MJINI BUSIA ,SARA MARTHA, MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA DHAMIRA MOJA CBO, AMEELEZA AZMA YA SHIRIKA HILO KULETA MAFUNZO YANAYOLENGA KUWAJENGA WANAHABARI KUHUSU MASUALA YA AFYA YA AKILI NA AINA ZOTE ZA MSONGO WA MAWAZO., WAKISHIRIKIANA NA SHIRIKA LA TRUSTLAB NA EUROPEAN UNION.

HATA HIVYO, WANAHABARI WAKIONGOZWA NA EMMANUEL JUMA NA VICTOR ODANYA WAMEELEZEA JINSI MAFUNZO HAYO YATAKAVYOWANUFAISHA NA KUBORESHA KAZI YAO YA UANAHABARI.

Siku moja tu baada ya Mahak**a kuu mjini busia kuwafunga jela maisha wanaume wawili na mmoja miaka 15 Baada ya kupatikan...
25/07/2025

Siku moja tu baada ya Mahak**a kuu mjini busia kuwafunga jela maisha wanaume wawili na mmoja miaka 15 Baada ya kupatikana na hatia ya kudhumu watoto wasichana kwa kuwanajisi, shirika lisilo la kiserikali la Linda Mtoto limeweza kuandaa mafunzo kwa viongozi wa makanisa (pastors) na wa dini la kiisilamu mjini busia kuwahamasisha kuhusu umuhimu wa haki za watoto

Kulingana na Everlyn Achieng mmoja wa shirika Hilo amesema kuwa lengo lao kuu kuleta mafunzo hayo kwa waumini ni kuwa kuwaelimisha Sheria za serikali kuhusu kulinda watoto wakati wanaendeleza mahubiri kanisani na mahali ambapo wanaweza kupeleka kesi hiyo Mtoto anapodhulumiwa

Mafunzo hayo yameleta pamoja zaidi ya wachungaji 45 kutoka eneobunge la Teso na mjini busia kuangazia mwaswala kadhaa yakiwemo kuwahudumia watu wa jinsia mbili na pia kujua jinsi Mtoto mdogo akishikwa k**a amejihusisha kwa Mambo yasiyo ya kawaida jinsi ya kishugulikiwa

Wakizungumza baada ya mafunzo hayo yaliyofanyika katika kanisa moja Eneo la Burumba,mchungaji John Omuyinda, Mustafa Juma, mchungaji Anastasia,wameweza kushukuru shirika Hilo la Linda Mtoto kwa kuwaletea mafunzo hayo kwani yatawasaidia sana hata wakiwa wanaendesha huduma zao kanisani huku wakiomba wananchi kushirikiana na serikali kumaliza visa hivi vya dhuluma kwa watoto na kuwachana na Mambo ya kangaroo korti

Jambo sawia lilisemwa na Cythy Nekesa Makila hakimu mkuu mwandamizi wa Mahak**a kuu mjini busia wakati wa kutoa uamuzi wa kifungo Cha maisha jela kwa wanaume wawili mjini busia akisema adhabu hiyo kali itasaidia katika kumaliza tabia hiyo ya kudhulumu watoto

Wananchi wamehimizwa kukumbatia makundi Kwa mnajili ya kujiimarisha kiuchumi na hata kupata usaidizi Kutoka Kwa serikali...
10/06/2025

Wananchi wamehimizwa kukumbatia makundi Kwa mnajili ya kujiimarisha kiuchumi na hata kupata usaidizi Kutoka Kwa serikali ndio himizo Kutoka Kwa mwakilishi mteule Kutoka kaunti ya Busia Mweshimiwa Beatrice wakati alipozuru wanachama wa Soko posta.

Wito umetolewa kwa wazazi eneo bunge la Nambale kulipa karo ya wanao ili kusaidia shule kuendeleza shuguli zake ipaasavy...
10/06/2025

Wito umetolewa kwa wazazi eneo bunge la Nambale kulipa karo ya wanao ili kusaidia shule kuendeleza shuguli zake ipaasavyo

Wakizungumza kwenye hafla ya kupeana hundi ya basari ya milioni 46 katika shule za eneobunge la Nambale, mbunge wa eneo hilo Geoffrey Mulanya na viongozi wengine wamehimiza wazazi kutochoka kulipa karo ila waendelee kulipa karo kwani basari haiwezi toshelesha wanafunzi wote shuleni.

Mulanya ametoa wito kwa wazee kutojiingiza kwa ulevi sana kwani wanachangia watoto wao pia kujipata kwenye Hali sawia ila wajukumike kwenye maswala ya wanao

04/06/2025
Maadimisho ya 62 ya Madaraka Katika gatuzi ndogo ya Matayos  yanaadimishwa Kwenye shule ya msingi ya Maabale wodi ya May...
01/06/2025

Maadimisho ya 62 ya Madaraka Katika gatuzi ndogo ya Matayos yanaadimishwa Kwenye shule ya msingi ya Maabale wodi ya Mayenje.Maadimisho haya yanaongozwa na mwakilishi wodi Richard Okello Mudibo,mwakilishi wadi mteule Concepter,aliyekua waziri Katika utawala Wa Serikali ya KANU Philip Masinde miongoni mwa viongozi wengine wengi.

Heri njema za Madaraka Kutoka Kwa spika Wa kaunti ya Busia Hon Fredrick Wafula Odilo.
01/06/2025

Heri njema za Madaraka Kutoka Kwa spika Wa kaunti ya Busia Hon Fredrick Wafula Odilo.

Pokea heri njema Kutoka Kwa mgombea wa kiti cha ubunge Kutoka eneo Bunge la Butula Hon Timothy Sibuda Namatsi
01/06/2025

Pokea heri njema Kutoka Kwa mgombea wa kiti cha ubunge Kutoka eneo Bunge la Butula Hon Timothy Sibuda Namatsi

Address

Bulanda Checkpoint
Nairobi Industrial Area
P.OBOX450BUSIA

Telephone

+254723784848

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Western Nyota 87.8 Busia Fm posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Western Nyota 87.8 Busia Fm:

Share