19/09/2026
Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi nchini Kenya (COTU), Francis Atwoli, amesisitiza kwa dhati kuwa hakuna mwanafamilia wake atakayechomwa moto (cremation) wakati yeye bado yuko hai.
Atwoli amesema hata k**a mwanafamilia atakayeweka takwa hilo kwenye wosia wake (will), yeye atapinga vikali na kuhakikisha taratibu za mila na utamaduni zinafuatwa kikamilifu. Zaidi ya hayo, kiongozi huyo ameeleza nia yake ya kuishi hadi kufikisha miaka 130.