16/04/2026
Wiki hii kwenye PEVUKA, tutaangazia mada mbalimbali zenye uzito katika jamii na maendeleo binafsi.
Katika kitengo cha Taswira ya Jamii, tutaangazia ulimwengu wa taarab ya Kenya, historia yake, ubunifu wake, na mchango wake katika kuimarisha utamaduni wetu.
Kupitia Darasa la Maisha, tutajadili umuhimu wa kuwa na ujuzi wa ziada mbali na elimu ya darasani, na jinsi unavyoweza kuongeza nafasi katika soko la ajira.
Katika Ladha ya Lugha, tutachambua msemo “Tabia ni ngozi”, tukieleza namna tabia ya mtu humfuata kila mahali na umuhimu wa kujijenga kitabia.
Kupitia Jifunze Nami, tutaangazia maisha ya Harriet Tubman, ujasiri wake katika kupigania uhuru na mchango wake mkubwa katika historia ya ukombozi.
Jiunge nasi Ijumaa hii kuanzia saa tatu asubuhi ndani ya unc radio ili uweze kujifunza na kutafakari kupitia maudhui yenye maana.
Saa: 9:00 a.m