ASILI YETU - Back to the Roots

ASILI YETU - Back to the Roots Katika ukurasa huu utajifunza mitindo ya maisha ya asili ya kiafrika na namna ya kutatua changamoto.

Zamani mtoto alikuwa ni mtoto wa jamii nzima. Mtu yeyote alikua na wajibu wa kumfunza adabu mtoto asie wake. Malezi lili...
14/06/2026

Zamani mtoto alikuwa ni mtoto wa jamii nzima. Mtu yeyote alikua na wajibu wa kumfunza adabu mtoto asie wake. Malezi lilikua ni jukumu la jamii nzima.

Leo mtoto ni wako pekeako, simu na tv

πŸ‘‰ Je tunapotea au tuko sawa?
#𝐰𝐚𝐭𝐨𝐭𝐨

MBONO/NYONYO/MBARIKA (Castor Plant). Mbono (Ricinus communis), unaojulikana pia k**a Castor Plant, ni mmea ambao umetumi...
14/06/2026

MBONO/NYONYO/MBARIKA (Castor Plant).
Mbono (Ricinus communis), unaojulikana pia k**a Castor Plant, ni mmea ambao umetumika kwa karne nyingi katika tiba za asili Afrika, Asia na Mashariki ya Kati. Sehemu za mmea huu, hasa mafuta yanayotokana na mbegu zake, majani na mizizi zilitumika kwa madhumuni tofauti ya kiafya.

πŸ”Ή 1. Kwa Kufunga Choo (Constipation)
Haya ndiyo matumizi maarufu zaidi ya mbono duniani. Mafuta ya mbono (castor oil) yalitumjka kwa kunywa kiasi kidogo.
Mara nyingi kijiko 1–2 kwa watu wazima.
πŸ”Ή 2. Kwa Maumivu ya Viungo na Mgongo.
Mafuta ya mbono yalipashwa moto kidogo.
Kisha kupakwa kwenye viungo vinavyouma k**a magoti, mgongo au kiuno.
πŸ”Ή 3. Kwa Kuvimba/Uvimbe wa Mwili.
Majani makubwa ya mbono yalipashwa moto kidogo na kuwekwa au kukandia sehemu yenye uvimbe.
πŸ”Ή 4. Kwa Kuchochea Uzalishaji wa Maziwa ya Mama.
Majani yalipashwa moto kidogo na kuwekwa juu ya matiti kwa muda. Iliamini kuwa husaidia kuongeza mtiririko wa maziwa kwa mama anayenyonyesha.
πŸ”Ή 5. Kwa Nywele na Ngozi ya Kichwa.
Mafuta ya mbono yalipakwa kichwani na kufanyiwa masaji. Husaidia kukuza nywele na hupunguza ukavu wa ngozi ya kichwa.
πŸ”Ή 6. Kwa Maumivu ya Meno
Majani au mizizi ilichemshwa kisha maji yake yalitumika kusukutua mdomo.

⚠️ Tahadhari muhimu: Mbegu za mbono mbichi zina sumu kali inayojulikana k**a ricin. Hazipaswi kuliwa mbichi. Matumizi ya jadi yaliyo salama yalihusisha mafuta yaliyotayarishwa kwa uangalifu au matumizi ya nje ya mwili.

πŸ‘‰ Je, mbono/mbalika unajulikana kwa jina gani katika eneo lenu, na unatumikaje?

MCHAI CHAI (Lemon grass)Mchai chai, unaojulikana pia k**a Lemongrass, ni mmea ambao umetumika kwa karne nyingi katika ti...
13/06/2026

MCHAI CHAI (Lemon grass)
Mchai chai, unaojulikana pia k**a Lemongrass, ni mmea ambao umetumika kwa karne nyingi katika tiba za asili. Mbali na kutumika k**a kiungo cha chai, ulithaminiwa kwa matumizi yake mbalimbali ya kiafya.
πŸ”Ή Kwa mafua, kikohozi na homa.
Majani kadhaa yalichemshwa katika maji kwa dakika 10–15 na chai yake kunywewa ikiwa ya moto. Katika baadhi ya jamii, watu walijifukiza mvuke wake kusaidia kufungua pua zilizoziba na kifua.
πŸ”Ή Kwa maumivu ya tumbo na gesi.
Chai ya mchai maji ilinywewa baada ya chakula ili kusaidia mmeng'enyo wa chakula, kupunguza gesi tumboni na maumivu ya tumbo.
πŸ”Ή Kwa msongo wa mawazo na usingizi.
Katika tamaduni nyingi za Asia, chai ya mchaichai ilinywewa jioni kwa kuaminiwa kusaidia mwili kutulia, kupunguza wasiwasi na kuboresha usingizi. Pia husaidia kurudisha kumbukumbu.
πŸ”Ή Kwa shinikizo la damu.
Baadhi ya jamii zilikuwa zikinywa chai ya mchai maji mara kwa mara kwa kuamini kuwa husaidia afya ya moyo na mzunguko wa damu.
πŸ”Ή Kwa afya ya figo na njia ya mkojo. Baadhi ya jamii zilitumia chai yake k**a kinywaji cha kuongeza mkojo (diuretic), wakiamini husaidia mwili kuondoa takamwili. Pia kutibu maambukizi ya njia ya mkojo(UTI)
πŸ”Ή Kwa afya ya kinywa.
Maji yaliyochemshwa na majani ya mchai maji yalitumika kusukutua mdomo ili kusaidia kupunguza harufu mbaya ya kinywa.
πŸ”Ή Kufukuza mbu na wadudu.
Majani yalichomwa au kusagwa ili kutoa harufu inayofukuza mbu. Leo hii, mafuta ya lemongrass bado hutumika katika baadhi ya dawa za kufukuza wadudu.

πŸ‘‰ Je, katika eneo lenu mchaichai ulitumika kutibu tatizo gani?

Jani la Uzazi/Mvuti  (Lantana camara)Ingawa wengi huutambua mmea huu kwa maua yake yenye rangi nzuri na matunda yake meu...
12/06/2026

Jani la Uzazi/Mvuti (Lantana camara)

Ingawa wengi huutambua mmea huu kwa maua yake yenye rangi nzuri na matunda yake meusi ambayo huliwa, katika jamii mbalimbali za Afrika, Asia na Amerika ya Kusini, Mvuti/Jani la uzai umetumika kwa muda mrefu katika tiba za asili.

πŸ”Ή Kwa vidonda na majeraha.
Majani mabichi hupondwa na juisi yake kuwekwa moja kwa moja kwenye vidonda, michubuko na majipu ili kuharakisha iponaji.

πŸ”Ή Kwa homa na malaria.
Majani yake huchemshwa na chai yake kunywewa kwa kiasi kidogo kusaidia kupunguza homa na Malaria.

πŸ”Ή Kwa kikohozi na matatizo ya kifua.
Chai ya majani yaliyochemshwa hunywewa au mvuke wake kuvutwa ili kusaidia kupunguza kikohozi, na mafua .

πŸ”Ή Kwa maumivu ya tumbo
Baadhi ya jamii walitumia mchemsho wa majani kwa maumivu ya tumbo, kujaa gesi na matatizo ya mmeng'enyo wa chakula.

πŸ”Ή Kwa afya ya wanawake
Katika baadhi ya tamaduni, chai ya mizizi au majani ya mmea huu hutumika kurekebisha mzunguko wa hedhi kwa wanawake, kutibu uvimbe ktk tumbo la uzazi, kusaidia mwanamke kushika mimba, n.k.

πŸ”Ή Kwa kumbukumbu na afya ya ubongo.
Baadhi ya jamii hutumia chai ya mmea huu kwa imani kuwa husaidia umakini na kuongeza kumbukumbu. Lkn jambo hili bado halijathibitishwa kisayansi.

⚠️ Tahadhari: Mama mjamzito haruhusiwi kutumia mmea huu.

πŸ‘‰ Je, mmea huu unajulikana kwa jina gani katika eneo lenu, na wazee wenu waliutumia kutibu tatizo gani?

TULSIScientific Name: Ocimum tenuiflorum/Ocimum sanctumCommon Name: Holy Basil/Sacred Basil/TulsiSwahili Names: Kivumbas...
04/06/2026

TULSI
Scientific Name: Ocimum tenuiflorum/Ocimum sanctum
Common Name: Holy Basil/Sacred Basil/Tulsi
Swahili Names: Kivumbasi/Mrihani

MEDICINAL USES OF HOLY BASIL (Tulsi)
Holy Basil has been regarded as a medicinal and sacred plant for thousands of years, especially in India, but it has also been adopted into traditional medicine in East Africa.

1. Colds, Flu, and Respiratory Conditions
This is one among of its most famous traditional use. Fresh leaves boiled in water and consumed as a warm herbal tea.

2. Stress, Anxiety, and Fatigue
One of the reasons Tulsi became famous globally is its reputation as an adaptogen.
Daily tea made from fresh leaves consumed in the morning or evening to improve mental clarity, reduce emotional stress and promote calmness

3. Stomach Upset and Digestion
Leaves chewed fresh or leaf tea prepared from boiled leaves used to relieve indigestion, bloating, mild diarrhea and stomach discomfort.

4. Blood Pressure and Heart Health
Traditional preparation
Tulsi tea consumed regularly was believed to promoted blood circulation and maintain cardiovascular balance.

5. Blood Sugar Control
Leaves chewed on an empty stomach or daily herbal tea. Used traditionally among people concerned about excessive thirst and other symptoms associated with elevated blood sugar.

6. Insect Repellent
Fresh plants grown around homes, leaves rubbed onto the skin or dried leaves burned to deter Mosquitoes and Flies

7. Spiritual and Cultural Uses
In Hindu tradition: Tulsi is regarded as a sacred plant. Often grown near homes and temples. Associated with purification, protection, and spiritual well-being.

Scientific Findings:
Researchers have identified that Tulsi has several chemical compounds like Eugenol, Rosmarinic acid, Ursolic acid, Linalool and various flavonoids.
These compounds have demonstrated Antioxidant activity, Antimicrobial properties and Potential stress-reducing effects

➑️What is this plant called in your area, and what did your elders traditionally use it for?

Kuwa wa kisasa haimanishi usahau ulikotoka.Modernity without roots is emptiness.πŸ‘‰ Unasemaje?
03/06/2026

Kuwa wa kisasa haimanishi usahau ulikotoka.
Modernity without roots is emptiness.

πŸ‘‰ Unasemaje?

Majani ya Mpera (guava Leaves)Je, wajua kuwa majani ya mpera yalikuwa sehemu ya tiba za nyumbani katika jamii nyingi dun...
02/06/2026

Majani ya Mpera (guava Leaves)

Je, wajua kuwa majani ya mpera yalikuwa sehemu ya tiba za nyumbani katika jamii nyingi duniani?

Wazee wetu walitumia majani ya mpera yaliyochemshwa kwa matatizo ya tumbo k**a kuharisha, gesi na maumivu ya tumbo.

Pia, katika baadhi ya tamaduni za Asia, chai ya majani ya mpera ilinywewa kusaidia afya ya moyo yaani kurekebisha Shinikizo la Damu na kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu.

πŸ‘‰ Je, nyumbani kwenu majani ya mpera yalitumiwa kutibu tatizo gani?

Afrika haikuanza baada ya ukoloni. Tulikuwa na mifumo yetu, sheria na maadili.πŸ‘‰ Tuambie, unajua historia gani ya kabila ...
31/05/2026

Afrika haikuanza baada ya ukoloni. Tulikuwa na mifumo yetu, sheria na maadili.

πŸ‘‰ Tuambie, unajua historia gani ya kabila lako?

Address

Nairobi

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ASILI YETU - Back to the Roots posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share