25/04/2025
MCHUNGAJI POTOVU AZUILIWA MALINDI.
Mchungaji tata huko Chakama, eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi alikamatwa hiyo Jana kwa madai ya kuwapotosha waumini wake na hata kusababisha maafa miongoni mwa baadhi ya waumini.
Abel Kahindi Gunga, mchungaji wa Kanisa la New foundation amekuwa akitumia " Mti wa Uzima" ulioko kando ya Kanisa Hilo kuwatoa waumini wake mapepo yanayowatatiza.
Akizungumza na vyombo vya habari , Abel Mwenye umri wa miaka 48, alitetea nguvu za mti huo akisema kwamba ni wengi waliosaidika na mti huo mara tu walipoupanda.
Hata hivyo ameitaka Serikali kuendelea na uchunguzi wa Kwa kina ili kubaini ukweli wa Kesi inayolikumba kanisa lake.
Akiongoza kikosi cha oparesheni hiyo, Naibu Kamishana wa Kilifi Kaskazini alitangaza kufungwa kwa kanisa Hilo mara Moja, uchunguzi ukiendelea.