10/12/2025
WATASOMA WANAFUNZI BORA AU LA? >>SINTOFAHAMU YAENDELEA KUHUSU UTARATIBU WA KUTANGAZA MATOKEO YA KJSEA
Huku taifa likisubiri kwa hamu kutangazwa kwa matokeo ya mtihani wa Kenya Junior School Education Assessment (KJSEA), maswali yanaibuka kuhusu namna sherehe rasmi ya kutangaza matokeo hayo itakavyoendeshwa na iwapo majina ya wanafunzi bora yatawekwa hadharani.
Taarifa za awali zinadokeza kuwa katika mfumo mpya wa mtaala wa Umilisi (CBE), awali ukijulikana k**a CBC, wanafunzi wataorodheshwa kwa viwango tofauti kulingana na makundi ya masomo. Kila kaunti ndogo inatarajiwa kutambua wanafunzi sita bora katika kitengo cha STEM, watatu bora katika Social Sciences, na wawili bora katika Arts and Sports. Wanafunzi watakaong’ara zaidi KITAIFA wanadaiwa kuhakikishiwa nafasi katika shule walizozichagua.
Hata hivyo, hatua ya iwapo majina ya wanafunzi hao bora yatasomwa hadharani bado haijawekwa paruwanja na imeibua mjadala mpana.
Daudi, ambaye ni mwanahabari, mwalimu na mhariri katika kituo cha Ibuka FM, anapendekeza kuwa serikali iwasikilize washikadau na kuwatambua wanafunzi bora namna ilivyokuwa tu katika mtaala wa 8.4.4. ili kuwapa motisha. Anasema kutowataja wanafunzi bora kwa majina, shule na hata kaunti watokazo kutawanyima hamasa, hasa ikizingatiwa kuwa wao ndio kizazi cha kwanza kupitia mtaala mpya wa Umilisi.
Kenya ina jumla ya kaunti 47 na kati ya kaunti ndogo 290 hadi 295. Kwa mujibu wa wachambuzi, kutambua mwanafunzi bora kitaifa, kisha watatu bora na hatimaye kumi bora, kutasaidia kuweka rekodi za kwanza za kihistoria za mfumo huu mpya.
Wakati uongozi wa elimu ukisubiriwa kutoa mwelekeo, inaaminika kuwa vyombo vya habari vitakuwa na jukumu kubwa la kusaka na kutangaza orodha pana zaidi, ikiwemo mia bora au hata orodha za wanafunzi waliofanya vyema katika kila kaunti ndogo.
゚viralシfypシ゚