Dennis putin kenyatta

Dennis putin kenyatta 1.Ukurasa wa habari za michezo
2.pata ratiba
3.matokeo na
4.Tetesi za soka barani ulaya
(10)

Toka mwaka 2020, Chelsea ndiyo timu iliyoingiza pesa nyingi zaidi kuliko timu yeyote kwa bara zima la Ulaya kwa kuuza wa...
04/08/2026

Toka mwaka 2020, Chelsea ndiyo timu iliyoingiza pesa nyingi zaidi kuliko timu yeyote kwa bara zima la Ulaya kwa kuuza wachezaji:
1. Chelsea – Paundi bilioni 1.10
2. Benfica – Paundi milioni 770.40
3. RB Leipzig – Paundi milioni 719.42
4. Atalanta – Paundi milioni 667.47
5. Aston Villa – Paundi milioni 659.85
6. Stade Rennais – Paundi milioni 636.47
7. Wolves – Paundi milioni 636.44
8. Manchester City – Paundi milioni 635.73
9. Brighton – Paundi milioni 617.47
10. PSG – Paundi milioni 531.61

Wale unifanya niwapostie kila siku wako huku nawatambua sana ♥️
04/08/2026

Wale unifanya niwapostie kila siku wako huku nawatambua sana ♥️

HERVÉ RENARD AREJEA KUINOA CÔTÉ D'IVOIRE.Shirikisho la Soka la Côte d'Ivoire linatarajiwa kumtangaza rasmi Hervé Renard ...
03/08/2026

HERVÉ RENARD AREJEA KUINOA CÔTÉ D'IVOIRE.

Shirikisho la Soka la Côte d'Ivoire linatarajiwa kumtangaza rasmi Hervé Renard kuwa Kocha mkuu mpya wa timu ya taifa, hatua inayomrejesha kwenye kikosi hicho alichowahi kukiongoza kwa mafanikio makubwa.

Renard amekubali kurejea kuinoa timu hiyo, akianza awamu mpya ya kuijenga kuelekea mashindano yajayo ya AFCON.

Renard anakumbukwa kwa kuiongoza Côté d'Ivoire kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2015, hivyo kurejea kwake kunazua matarajio makubwa kwa mashabiki wanaoamini anaweza kuirejesha timu hiyo kwenye ushindani wa kiwango cha juu barani Afrika.

Toa maoni yako

INFANTINO ADAIWA KUTAFUTA MSAADA WA TRUMP KULINDA NAFASI YAKE FIFA.Ripoti kutoka vyombo vya habari vya Marekani zinaelez...
03/08/2026

INFANTINO ADAIWA KUTAFUTA MSAADA WA TRUMP KULINDA NAFASI YAKE FIFA.

Ripoti kutoka vyombo vya habari vya Marekani zinaeleza kuwa Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino, alijaribu kutafuta uungwaji mkono wa Rais wa Marekani, Donald Trump, ili kuimarisha nafasi yake katika uongozi wa FIFA.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Infantino alipanga kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, Jumatatu hii Agosti 3, 2026, Mazungumzo hayo yalidaiwa kulenga kujadili nafasi ambayo mchezo wa soka unaweza kuwa nayo katika kuimarisha ushawishi wa Marekani katika jukwaa la kimataifa.

Taarifa hizo zimeibua mjadala kuhusu uhusiano kati ya uongozi wa soka duniani na siasa za kimataifa, huku zikisubiriwa ufafanuzi zaidi kutoka kwa wahusika husika.

🚨 Paris Saint Germain wanataka kufanya haraka kukamilisha Usajili wa Mshambuliaji wa Barcelona Ferran Torres wiki hii, M...
03/08/2026

🚨 Paris Saint Germain wanataka kufanya haraka kukamilisha Usajili wa Mshambuliaji wa Barcelona Ferran Torres wiki hii, Mazungumzo yanaendelea. 🇪🇸

🚨🇧🇷 Vinicius Jr akiwa kwenye Saloon ya Camavinga akitengeneza muonekano wake mpya vizuri. ✂️
03/08/2026

🚨🇧🇷 Vinicius Jr akiwa kwenye Saloon ya Camavinga akitengeneza muonekano wake mpya vizuri. ✂️

🚨 Christian Eriksen amerejea rasmi kwenye Kambi ya Timu yake ya Wolfsburg ambao wanajindaa na msimu mpya baada ya kupata...
03/08/2026

🚨 Christian Eriksen amerejea rasmi kwenye Kambi ya Timu yake ya Wolfsburg ambao wanajindaa na msimu mpya baada ya kupata shida ya moyo mwezi Uliopita akiwa na timu yake ya taifa ya Denmark.🇩🇰

Christian Eriksen bado hajapona kabisa hivyo atarud tena kwao Denmark kukamilisha matibabu yake💔🇩🇰

Kabla ya kukutana na Cristiano Ronaldo, Georgina Rodríguez alikuwa akifanya kazi k**a mhudumu wa mauzo katika duka la Gu...
03/08/2026

Kabla ya kukutana na Cristiano Ronaldo, Georgina Rodríguez alikuwa akifanya kazi k**a mhudumu wa mauzo katika duka la Gucci jijini Madrid.

Mwaka 2016 Ronaldo aliingia dukani hapo k**a mteja, na tukio hilo lisilotarajiwa likabadilisha maisha yao wote wawili kwani walitokea kupendana wakaanzisha familia, na kilichofuata ni historia.

Georgina amewahi kueleza mara nyingi jinsi alivyotoka kwenye maisha ya kawaida akifanya kazi kwa saa nyingi bila hata kufikiria kwamba siku moja angeishi maisha ya kifahari kiasi hicho.

Leo hii ni mjasiriamali mwenye mafanikio, mwanamitindo, na mmoja wa wanawake wanaofuatiliwa zaidi duniani kwenye mitandao ya kijamii.

Pia ni mama wa watoto wa Ronaldo, na kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, anatarajiwa kufunga ndoa na nyota huyo wa soka wiki ijayo

✍️ Sema shemeji lipo si mbaya ila sio k**a kile chuma cha naniì😁

Kwenye moja  ya mahojiano  yake Zlatan anasema wakati anajiunga na Ajax  mwaka 2001 kwa  dau la  €7.8  jezi yake ilikuwa...
03/08/2026

Kwenye moja ya mahojiano yake Zlatan anasema wakati anajiunga na Ajax mwaka 2001 kwa dau la €7.8 jezi yake ilikuwa inasoma jina lake pekee yaani Zlatan,ila baba yake mzazi hakupendezwa na hilo.

Anasema ilichukua muda kundua hilo maana ni k**a mzee alikuwa anamaind sana kwanini halijawekwa jina lake kwenye jezi ya Zlatan.

Zlatan anasema ilikuwa akizungumzwa kwenye magazeti jina lililokuwa linatajwa sana ni Zlatan so mzee alitaka utambulishe wake kwa mwanae ila kumwambia ndiyo alikuwa hataki.

Anasema baada ya kugundua hilo alilazimika kubadilisha jina la jezi yake na kusoma Ibrahimovic ili tu kumfanya baba yake ajiskie vizuri kwa kijana wake.

Neymar amebadilisha maisha ya familia hii kwa kununua tu kitafunwa maarufu kinachoitwa Vaso da Felicidade.Baada ya kuwa ...
03/08/2026

Neymar amebadilisha maisha ya familia hii kwa kununua tu kitafunwa maarufu kinachoitwa Vaso da Felicidade.

Baada ya kuwa mteja wa duka dogo la mikate liitwalo Un Toque de Amor, umaarufu wa duka hilo uliongezeka kwa kasi mpaka wafuasi wao kwenye mitandao ya kijamii walipanda kutoka 2,000 hadi zaidi ya wafuasi 40,000, huku mauzo yakiongezeka kwa 80%.

Mafanikio hayo yaliiwezesha familia hiyo kukarabati duka lao lote na k**a ishara ya shukrani, waliamua kubadilisha jina la kitafunwa hicho kinachouzwa zaidi na kukiita NEYDIM kwa heshima ya Neymar.

Address

30036_00100
Nairobi
33004

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Dennis putin kenyatta posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Dennis putin kenyatta:

Shortcuts

Share

Category