HPE FILMS MEDIA

HPE FILMS MEDIA Capturing moments Creating legends

Sare mpya ya Polisi Kenya itakuwa na muundo maalum kwa maafisa wa k**e wajawazito.Sare hiyo iliyozinduliwa na Rais Willi...
28/08/2026

Sare mpya ya Polisi Kenya itakuwa na muundo maalum kwa maafisa wa k**e wajawazito.

Sare hiyo iliyozinduliwa na Rais William Ruto ina shati la samawati hafifu, suruali ya bluu iliyokolea, bereti au kofia ya bluu na buti nyeusi za kikazi.

28/08/2026

Polisi wanavyo wafukuza wafanyibiashara wanaoandamana Nairobi

28/08/2026

Wafanyabiashara wa CBD Nairobi Waandamana Kupinga Kodi

Wafanyabiashara wadogo katika CBD ya Nairobi wameandamana kupinga ongezeko la kodi na ushuru wa uagizaji bidhaa.Polisi w...
28/08/2026

Wafanyabiashara wadogo katika CBD ya Nairobi wameandamana kupinga ongezeko la kodi na ushuru wa uagizaji bidhaa.

Polisi walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakielekea katika ofisi za KRA, huku shughuli za biashara na usafiri katika baadhi ya maeneo ya CBD zikitatizika.

Msanii wa Gengetone kutoka jijini Nairobi Stupid Boy ameripotiwa kuaga Dunia Kwa kujitia kitanzi
28/08/2026

Msanii wa Gengetone kutoka jijini Nairobi Stupid Boy ameripotiwa kuaga Dunia Kwa kujitia kitanzi

Jackline Wangui Njoroge, aliyekuwa akitafutwa kwa karibu wiki mbili, amepatikana amefariki katika machimbo ya Kogoto, Ba...
28/08/2026

Jackline Wangui Njoroge, aliyekuwa akitafutwa kwa karibu wiki mbili, amepatikana amefariki katika machimbo ya Kogoto, Bahati, Nakuru.

Mwili wake ulipatikana Agosti 22 ukiwa na majeraha makubwa kichwani na dalili za kushambuliwa.

Polisi wameanzisha uchunguzi wa mauaji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua CP Salum Hamduni kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.Kabl...
27/08/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua CP Salum Hamduni kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Kabla ya uteuzi huo, CP Hamduni alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemhamisha Queen Sendiga kutoka nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa...
27/08/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemhamisha Queen Sendiga kutoka nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara na kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

Sendiga anachukua nafasi ya Adam Malima, ambaye amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Mwigizaji wa Hollywood, Tyrese Gibson, ameondoka Uganda na kuelekea Kenya baada ya kumaliza ziara yake nchini humo.Gibso...
27/08/2026

Mwigizaji wa Hollywood, Tyrese Gibson, ameondoka Uganda na kuelekea Kenya baada ya kumaliza ziara yake nchini humo.

Gibson alitembelea Africa Coffee Park mjini Ntungamo, ambako alijadili fursa za uwekezaji katika sekta ya kahawa nchini Uganda.

Ziara yake Uganda pia ilihusisha mikutano na viongozi mbalimbali, akiwemo Rais Yoweri Museveni.

Nguli wa kimataifa wa Pantsula kutoka kundi la Soweto Skeleton Movers, Jabulani Manyoni, amefariki dunia.Manyoni alijuli...
27/08/2026

Nguli wa kimataifa wa Pantsula kutoka kundi la Soweto Skeleton Movers, Jabulani Manyoni, amefariki dunia.

Manyoni alijulikana kwa umahiri wake wa kucheza na uwezo wake wa kipekee wa kunyumbulika mwili. Kifo chake ni pigo kwa sanaa ya Pantsula.

Address

Nairobi

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when HPE FILMS MEDIA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share