05/10/2025
πππππ πΌππΌπππΌππππ ππππ ππππππ ππππ πππππππ πΎπππΎππππ:
1 Samweli 15:22
[22]"Naye Samweli akasema,
je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA?
Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu. "
Litukuzwe jina lipitalo majina yote kwa kulituma somo hili adhimu leo...
Maandiko matakatifu hapo juu ni mazungumzo kati ya Samweli nabii wa Mungu kwa Mfalme Sauli aliyekuwa anatawala Israel na Yuda nyakati hizo...
Kwa ufupi ni kwamba Sauli aliagizwa na Mungu akaangamize kila kitu........
Lakini Sauli akaacha kuangamiza mfalme na wanyama walionona kwa kigezo kwamba atakwenda kumtolea Mungu sadaka...
Sauli alikiuka maagizo ya Mungu akiamini kwamba atamfurahisha Mungu kupitia kumtolea sadaka na dhabihu. Lakini Mungu alichukizwa na kitendo cha Sauli kuasi maagizo yake,
Ndipo sasa akamtuma nabii Samweli kwenda kumwambia sauli kwamba kwasababu hukunitii nilichokuagiza kuanzia sasa hutakuwa mfalme tena juu ya watu wangu Israel. Jambo hili lilimfadhaisha mfalme Sauli..
Nini Mungu anatufundisha hapa??
Mungu anataka kutuambia kwamba kutii maagizo yake ni bora kuliko kitu kingine chochote chini ya jua. Mambo mengi yanamchukiza Mungu lakini hili la kutotii maagizo yake ni kero kwa Mungu
Wengi wetu leo hii tumekuwa watu wazuri sana kwenye idara ya kumtolea Mungu sadaka lakini hatuko vizuri kwenye kutii maagizo ya Mungu.
Hatufuati nini Mungu anataka tufanye lakini tunatoa sadaka tukiamini kupitia kufanya hivyo Mungu atasamehe kirahisi dhambi na maovu yetu...
Yaani tunatumia sadaka k**a kigezo cha kujisafisha huku tukiamini kupitia kufanya hivyo Mungu anasamehe...
Ukweli wa neno la Mungu ni kwamba Mungu anavutwa zaidi na Mtu anayemtii kuliko anayemtolea sadaka...
Roho Mtakatifu anafanya kazi na watiifu. Ili sadaka zako zipate kibali machoni pa Mungu ni lazima uanze kutii kwanza. Ukishindwa kutii lakini ukatoa sadaka, hizo sadaka za Mtu asiyetii ni chukizo na si kitu machoni pa Mungu.
Mithali 15:8
[8]Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa BWANA;
Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake.
Mithali 21:27
[27]Sadaka ya wasio haki ni chukizo;
Si zaidi sana ailetapo mwenye nia mbaya!
Na utii unaozungumziwa hapa si tuu kupuuza neno la Mungu lakini pia kule kushindwa kuitii sauti ya roho wa Mungu inayotusemesha ndani yetu.
Mara nyingi Roho amekuwa akituambia rohoni usifanye hiki, acha hivyo, nyamaza, usichukue, usitukane, n.k. lakini tumekuwa wakaidi, tunapuuza na kufanya tunayotaka sisi...
Huyu ni Mungu anatusemesha tunapokaidi tunamkosea aliyetuumba
Kuna mambo mengi sana leo tunahangaika nayo kwasababu tulipuuza sauti ya Mungu ndani yetu
Kuna vitu vingi vibaya yameota na kuketa madhara kwenye maisha yetu kwasababu ya hatukutii maagizo ya Mungu.
Kutokumtii Mungu kumeleta anguko kwenye utumishi, ndoa, uchumi, afya, vifo, kukataliwa, kupoteza, nuksi, nk
Kuna watu wanadhani unaweza kumtii Mungu kwenye mambo fulani na mengine ukayapuuza....
Mungu anaanza kupima uaminifu wa mwanadamu kwa mambo yanayodhaniwa kuwa madogo madogo sana ndipo sa anaanza kukuamini kwa viwango vikubwa. Ukishindwa kuwa mwaminifu kwenye mambo madogo huwezi kauminiwa kwenye mambo makubwa
Luka 16:10
[10]Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.
Je ni wapi ambapo unashuhudiwa nafsini mwako kwamba unatakiwa kutiiii??
Basi omba rehema
Msihi Mungu akusamehe na amua kubadilika, anza kumtii Mungu na kuyaishi maagizo yake. K**a neno la Mungu lisemavyo;
Yakobo 4:7
[7] "Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
Kwa watumishi wa Mungu, kabla hujawahimiza waumini wako kutoa sadaka, wafundishe kwanza kuwa watii, maana utii ni chanzo cha mema yote chini ya jua.