15/05/2026
πππππ ππππ πππ πππππππ πππππππ
πππππππ π
Shinda yenu ni kutolike π« si ulike before usome. Annaliza ameshtuka kuona Kefa amefika. Akamwambia sikiza,ni utoke ama niite polisi lakini Kefa akamwambia relax,sina ubaya babe,I just want us talk. Annaliza akamwambia usiniite babe,iam not your babe we divorced na iliisha hivyo. Kefa alimwambia sikiza na unisikize vizuri,ushawai jiuliza mbona nilikubali kusign nitoke jela? To teach you a lesson for betraying na mambo ni mawili, its either uwe wangu or nobody will have you,kaa ukijua hilo. Annaliza alimwambia sikiza bro,hutanitishia mimi,naolewa na Robert na ukitaka I will invite you.
Kefa alitoka akakuja akapata Robert hapo. Robert kumuona akamshika tai akamuuliza unafanya nini? Kefa akamwambia hii ni hosi,nimekuja kutibiwa alahπ€£π€£π€£Robert karibu amvae vae Kefa but Annaliza akakuja akamwambia babe,dont create a scene.
Robert alimuuliza Annaliza huyu gaidi anataka nini? Annaliza akamwambia hata yeye hajui,amekuja tu kwa ofisi yangu akaanza kusema ati sijui ooh bado mimi ni wake. Robert akamwambia basi, ndio ajue tuko serious tunaoana very soon infact closer ndio ajue tuko serious.
Tyrone na yeye,aligundua Sabina hayuko happy akamuuliza,si umeambiwa umepona,mbona hauko happy? Sabina akadanganya akasema ni venye Tinah wangu hayuko hapa so hata siezi furahia. Tyrone akamwambia dont be soo hard on yourself,ingia twende home lakini Sabina akamwambia acha tu nitembee wee enda nakuja. Si ati Sabina anataka kutembea,anataka kurudi adeal na huyu daktari mbona amlipe na amcheze ππ
Tyrone kuenda tu hivi,Sabina akarudi kwa yule daktari,akamuuliza si tulikua na deal,mbona umenibeba ujinga? Lakini daktari akamwambia sikiza,yes ulinipea pesa but mimi ni daktari I have my stand na siezi nunuliwa na pesa ju ya ujinga wako mwanamke mzima k**a wewe,unadhani 300k zinaeza ninunua? Na k**a ni pesa zako unataka ndio hizi,alah! Sabina akarudishiwa pesa zake na akaambiwa kanyaga nje.πππ
Baadaye Robert alikuja akaambia Tyrone,we had plans tufanye wedding pamoja but venye mambo inaendelea seems kwako itadelay so sisi tulikua tumeona tuoane mapema mapema as you try to fix your family. Tyrone alimwambia haina shida,its still ok.
πππππππ π
Tufike mtaa wa Kibra, na sasa hapa ndio nataka mfungue macho vizuri sana. Huku ni kibera na huku ndio Tinah alitekwa nyara amefungiwa huku. Kamefungwa miguu,kisha sasa,nani huyo amesimama kando yake? Sabina! Makosa. Sabina alimteka nyara mtoto wake kutumia yule gaidi beshte wa Ray ,alafu makosa ni Tinah hakuli,but Sabina aliambia gaidi wake sikiza,make sure she eats na atakaa huku until I get what I want,. Its Sabina guys!
Report ilifika kwa kina Tyrone na Robert inasemekana Brayson has been bailed out...walishtuka sana lakini chenye kiliwashtua zaidi after kuambiwa mwenye alimbail out, Saida. Tyrone aliisha tuπππ
Sabina ndio anarudi nyumbani anajifanya stressed but deep down ako sawa. Pale juu Saida alikuja akamwambia sikiza mama,now that umepona nataka uondoke kwangu lakini punde si punde,Tyrone akafika akawambia Saida njoo we need to talk haraka sana.
Tyrone alikuja akamuuliza Saida, what kind of nonsense,mbona unambail Ray? Saida akamwambia naamini he is innocent na ndio maana nikamtoa. Tyrone akamuuliza,mbona hukuniuliza? Saida akamuuliza nikuulize k**a nani? Saa ngapi na kila saa uko na Sabina? Tyrone alimwambia sikiza, si ati hauko kwa akili yangu ni venye niko na mambo mingi but yoh,mi bado nakupenda Saida ama unataka nifanye nini ndio ujue nakupenda? Hata Saida hakufikiria alimwambia Sabina umtoe kwa hii nyumba na Ray umpe nafasi ingine.
Kylian na yeye akiwa ametulia alipigiwa simu na Kefa. Kylian akamuuliza unataka nini? Ama unataka kunitishia? Kefa akamwambia relax,nataka kukusaidia,nasikia sister yako amekua kidnapped,niambie kila kitu unajua I can help. Kylian akamwambia sijui mengi but nasikia mwisho alikua na Ray,...punde si punde,Annaliza akafika akamuuliza Kylian unaongea na nani? Kylian akadanganya akasema ni beshte yangu tu. Wakamwambia incase Kefa anakucall usijaribu kushika simu. Kylian akasema siezi shika kabisa,saa hiyo ndio Kefa mwenyewe amekua anaongea na yeye.
Will Kefa help? Kwa leo ni,tuachie hapo.. goodnight everyone
Follow DAN