14/01/2024
MAOMBI
✅Ninafuta kila Shutuma za kipepo zinazofuatilia maisha yangu, kila shutuma mbaya juu yangu...... nazifuta kwa Damu ya Yesu Kristo.
✅Kwa Damu ya Yesu nawanyamazisha maadui zangu wote waliojipanga 2024 waliopanga foleni kunionea mwaka huu nawanyamazisha kwa Damu ya Yesu Kristo....Hawatanionea Biashara yangu, Uchumi, Ndoa yangu, watoto wangu nawanyamazisha kwa Damu ya Yesu
✅-Kwa Damu ya Yesu naishinda hiyo nguvu inayonishambulia mwanzo wa mwaka kwa Damu ya Yesu, Magonjwa ya mwanzo wa mwaka nayashinda kwa Damu ya Yesu, Nashinda Majaribu ya Mwanzo, vifo vya ghafla, kutaabika kwa mwanzo wa mwaka, umaskini wa mwanzo wa mwaka....Kila nguvu inayoshambulia mwanzo mwaka naishinda Kwa Damu ya Yesu .
✅Natuma Damu ya Yesu kwenda kuharibu kila madhabau ya ukoo inayopambana kuharibu vitu vizuri, kila madhabau iliyonitabisha miaka iliyopita uliyo haribu vitu vyangu vizuri iharibike....madhabau ya ukoo wa baba yangu, ukoo wa Mama yangu iharibike kwa Damu ya Yesu Kristo
✅-Navunja kila mipaka iliyowekwa kwenye maisha yangu, waliowekewa ndugu zangu, familia yangu, watoto wa tumbo la mama yangu, kila mipaka ya ukoo isihusiane na uzao wa tumbo la mama yangu, mipaka ya umaskini, ujinga kutokusoma, roho ya kuishia njiani ivunjike kwa Damu ya Yesu Kristo sawa na neno la Kinabii