IBN UMMAR CLIPS

IBN UMMAR CLIPS Bringing you powerful lectures, visual reminders, and timeless wisdom from trusted scholars.

Our mission is to spread the light of Islam through engaging videos that touch the heart, inspire reflection, and nurture.

Qur’an na Utulivu wa MoyoMoyo wa mwanadamu mara nyingi huchoka kutokana na mihangaiko ya dunia, huzuni, hofu na mitihani...
07/09/2025

Qur’an na Utulivu wa Moyo
Moyo wa mwanadamu mara nyingi huchoka kutokana na mihangaiko ya dunia, huzuni, hofu na mitihani ya maisha. Lakini Mwenyezi Mungu ametupa tiba kubwa zaidi ya yote – Qur’an Tukufu.

Qur’an ni nuru, ni maneno ya Allah yanayopenya moja kwa moja kwenye moyo. Mwenyezi Mungu anatuambia:

> “Hakika kwa kukumbuka Mwenyezi Mungu, nyoyo hupata utulivu.” (Qur’an 13:28)

Unapoisoma Qur’an, kuisikiliza au hata kuikumbuka kwa dhikr, unaona moyo unapata faraja, huzuni hupungua, na matumaini hujaa. Qur’an siyo tu kitabu cha kusomea ibada, bali ni rafiki wa moyo wako katika kila hali ya maisha.

👉 Hebu tujiulize: Je, tunachukua muda kila siku kuipa nafasi Qur’an kutuliza na kuunganisha nyoyo zetu na Allah?

🕌 Qur’an ndiyo dawa ya huzuni, tiba ya wasiwasi, na chanzo cha furaha ya kweli.
Kuelewa ni nini Qur'an na kwa nini imeteremshwa, tazama kwenye channel yetu ya youtube. Link: https://www.youtube.com/

Mwanaume, Acha Uzembe – Wewe Ndio Mtafutaji!Kuna kitu wanaume wengi wanapuuza wanapofikiria kuhusu ndoa. Wengi hukimbili...
02/09/2025

Mwanaume, Acha Uzembe – Wewe Ndio Mtafutaji!

Kuna kitu wanaume wengi wanapuuza wanapofikiria kuhusu ndoa. Wengi hukimbilia kuangalia body size, uso mzuri au ladha ya muda. Wengine hujikuta hata hali ya tumbo lao (njaa au shibe) ndiyo inawaongoza kufanya maamuzi. Ukiwa na njaa, kila kitu kinaonekana kitamu; ukiwa umeshiba, ghafla unakuwa na “standards.” Lakini je, familia hujengwa kwa tamaa za dakika au hisia za tumbo?

Hapana.

Mwanaume lazima ajue: wewe ndiye mtafutaji, wewe ndiye kiongozi, na wewe ndiye unaweka msingi wa familia. Uzembe wako wa leo ndio machozi ya kesho ya mke na watoto.

🔑 Usioe kwa macho pekee, kwa sababu urembo unaoonekana leo unaweza kupotea kesho.
🔑 Usioe kwa tamaa ya mwili, kwa sababu miili hubadilika – leo mnene, kesho mwembamba, au kinyume chake.
🔑 Usioe kwa msisimko wa muda, kwa sababu tamaa ikitulia, ndoa itabaki tupu.

Chagua mke wa dini na tabia njema.
Mtume ﷺ alisema: “Mwanamke huolewa kwa sababu nne: mali yake, nasaba yake, uzuri wake na dini yake. Chagua mwenye dini, utabarikiwa mikono yako.” (Bukhari na Muslim)

Mke wa dini si wa kupendeza kwa macho tu, bali ni wa kuimarisha moyo na nyumba yako. Yeye ndiye atakayekusaidia wakati huna, atakufariji wakati wa shida, atakushauri kwa hekima, na atakukumbusha Mwenyezi Mungu pale unapozidiwa na dunia.

Mwanaume, acha kuzembea.
Wewe ndiye unatafuta riziki.
Wewe ndiye unaongoza familia.
Wewe ndiye nguzo ya nyumba.
Usijifanye dhaifu kisa mitindo ya dunia au starehe za muda.

👉 K**a kweli unataka furaha ya dunia na akhera, tafuta kwa juhudi, chagua kwa busara, na usijidanganye na macho.
👉 Familia bora hujengwa juu ya heshima, subira, upendo na imani – si juu ya figure, sura au chakula cha siku moja.

Mwisho wa siku, mwili utazeeka, mali itaisha, sura itabadilika… lakini mke mwema wa dini ndiye ataendelea kuwa nuru yako hata kaburini.

USISAHAU KUFOLLOW PAGE HII.

28/08/2025

Qur'an memorization
Chapter 108: surah al-kawthar
Kawthar means plenty
It has three verses. Listen carefully and repeat after the reciter to enhance memorization.

“Hunger and Attraction: When a Man’s Stomach Controls His Desire”Listen closely, brother. Because what I’m about to tell...
28/08/2025

“Hunger and Attraction: When a Man’s Stomach Controls His Desire”

Listen closely, brother. Because what I’m about to tell you will sound strange, but it’s a fact backed by science, by psychology, and by human nature itself.

Men who are hungry… prefer women with higher weight.
Yes, you heard me right. When a man’s stomach is empty, his eyes see differently.

Survival Mode

Here’s why. Hunger is not just a feeling in your stomach. Hunger changes your brain. When you are hungry, your body shifts into survival mode. Every choice you make — even attraction — is influenced by that survival instinct.

In survival mode, beauty standards don’t matter. Fashion doesn’t matter. Instagram filters don’t matter.
What matters is survival. Strength. Nourishment. Stability.

And so, when a man is hungry, he is drawn to women with more weight, more flesh, more signs of food security. Subconsciously, he sees safety. He sees survival. He sees a partner who could endure, who could carry life, who could represent abundance in a time of scarcity.

Full vs Hungry

Now compare that to a man who is full.
A man who just ate, who is satisfied, who is not worried about his next meal — he has the luxury to chase society’s ideals. He can desire slimness, fashion, or whatever his culture has trained him to see as beautiful.

But hunger strips that away. Hunger is primal. Hunger doesn’t care about magazines or social media. Hunger takes you back to your roots.

And this is the truth most men don’t realize: a man’s desire can shift with his stomach.

The Stomach’s Influence

Think about it.
When you’re hungry, every commercial about food looks irresistible. Foods you normally ignore suddenly look delicious. The same brain shift happens with attraction.

When you’re well-fed, you might say: “I prefer this type of woman.”
But when you’re hungry, your stomach reprograms your eyes. It whispers to your mind: “Look for survival. Look for nourishment. Look for abundance.”

And suddenly, the same man who thought he preferred slimness finds himself drawn to curves, to fullness, to signs of health. Not because he changed as a person, but because his stomach changed his desires.

History and Evidence

This is not new. History has shown it.
In times of famine, men praised heavier women. In times of abundance, they praised slimness. When survival was uncertain, weight meant wealth, stability, and life.

Even in different cultures today, you see this shift. In societies where food is scarce, heavier women are admired. In societies drowning in abundance, thinness is celebrated.

So again, brother, desire is not fixed. Desire can shift — and sometimes, it shifts with nothing more than an empty stomach. And here’s the harsh truth:
Many men believe they are in control of their desires. They think attraction is purely about “preference.” But the reality is, your body is influencing you more than you know.

Your hunger can change your taste. Your environment can shape your standard. Your survival needs can bend your attraction.

So the next time you hear a man boldly declare, “I only like this type of woman” — ask him, “Are you full, or are you hungry?”
Because what he desires today might not be what he desires tomorrow… depending on the state of his stomach.

Remember this lesson, brother:
Attraction is not just about the eyes. It’s about the body. It’s about survival. It’s about the mind adapting to the circumstances.

And the man who is truly self-aware understands that even his desires are not always his own — they can be shaped by hunger, by need, by the deep voice of survival within him.

So don’t ever forget: a man’s desire can shift with his stomach.
That is not just science. That is life.
Follow for more educative posts like this.

👉 Wengi wetu tunalea wavulana, si wanaume.Mwanaume wa Kiislamu hakai tu akingoja kila kitu kiletwe kwake.Mwanaume wa Kii...
22/08/2025

👉 Wengi wetu tunalea wavulana, si wanaume.

Mwanaume wa Kiislamu hakai tu akingoja kila kitu kiletwe kwake.
Mwanaume wa Kiislamu ni kiongozi, ni mlinzi, ni mtoaji, ni mwenye kusimama na haki.

Lakini ukimuangalia kijana wa leo – mara nyingi anakimbia majukumu, anajificha nyuma ya wazazi, anashinda kwenye simu, michezo, au anajua tu kudai haki bila majukumu.
Huo sio Uislamu.

⚡ Uislamu unahitaji wanaume, si wavulana waliokomaa kimwili ila moyo na akili bado watoto.
⚡ Wanaume wanaosimama kuswali alfajiri, wanaofunga, wanaojua taabu za dunia na bado wanabeba familia zao kwa saburi.
⚡ Wanaume wanaojua heshima ya wake zao, wazazi wao na jamii.

Mama, Baba, Mwalimu, Jamii – tusijidanganye: Tukiwalea wavulana bila kuwafundisha majukumu, tutapata wanaume dhaifu, na familia dhaifu.

👉 Mwanaume wa Kiislamu si hadithi ya vitabu – ni jukumu la kila siku.
Na k**a wewe ni kijana, kumbuka: Wewe ndiye nguzo ya kesho. Usiridhike kuwa mvulana milele, wakati Uislamu unakuhitaji uwe mwanaume.

Unadhani nini kimechangia zaidi wavulana wengi kushindwa kukua kuwa wanaume wa kweli katika jamii ya Kiislamu?

Watch full video: https://youtu.be/kyxLyLVo1L8

💔 WAKATI NDOA INAFIKA HAPO HAKUNA KURUDI TENAKila ndoa huwa na changamoto. Kuna mabishano, migongano, na makosa ya kawai...
18/08/2025

💔 WAKATI NDOA INAFIKA HAPO HAKUNA KURUDI TENA

Kila ndoa huwa na changamoto. Kuna mabishano, migongano, na makosa ya kawaida ambayo husamehewa. Lakini pia kuna makosa na mienendo inayovunja ndoa kabisa—mambo ambayo yakifanyika, moyo wa mwenzi wako unavunjika kiasi cha kutokuweza kuunganishwa tena.

👉 Kuna wakati maumivu yanakuwa makubwa mno, hadi heshima na imani vinapotea.
👉 Kuna hatua ambapo kila neno la msamaha halina maana tena.
👉 Kuna nyakati ambapo moyo unasema “basi” – na huo ndio mwisho wa safari.

Ndiyo maana ni muhimu sana kujua:

Ni mambo gani huua ndoa kimya kimya?

Ni mipaka ipi usiyovuke?

Ni ishara zipi za hatari ambazo ukizipuuzia, kesho utajuta?

Ndoa sio mchezo. Ukiwa nayo, ilinde. Usisubiri mpaka ifikie pale ambapo hakuna kurudi tena. Bonyeza hiyo follow na like button k**a umefaidika.

✍️ Swali kwako leo: Unadhani ni jambo gani likitokea kwenye ndoa, hakuna tena kurudi nyuma?

18/08/2025

Qur'an memorization
Chapter 109: surah al-kafirun
Kafirun means disbelievers
It has 6 verses. Listen, repeat after the reciter to enhance memorization.

🌿 NEEMA YA MACHO 🌿Kila siku tunafungua macho yetu, tunaona anga la asubuhi, nyuso za wapendwa wetu, tunasoma Qur’an, tun...
14/08/2025

🌿 NEEMA YA MACHO 🌿

Kila siku tunafungua macho yetu, tunaona anga la asubuhi, nyuso za wapendwa wetu, tunasoma Qur’an, tunashuhudia rangi na uzuri wa dunia… lakini je, tunakumbuka kuwa hii ni neema kubwa kutoka kwa Allah?

Wapo waliolala jana wakiwa na macho yao, lakini leo hawaoni. Wapo waliokaa giza la maisha kwa miaka mingi, wakitamani hata dakika moja tu waone uso wa mama, mtoto, au hata rangi ya maua.

Macho yako yanaweza kuwa njia ya kukusogeza karibu na Allah au yakawa sababu ya hasara. Ni juu yako kuamua unayatazama nini, unayaepusha na nini.

Shukuru kwa macho yako — kwa kuyaepusha na haramu, na kuyaelekeza katika mema.
Maana kesho mbele ya Allah, macho yako yatazungumza na kutoa ushahidi wa yale uliyoyatazama.

📌 Tazama video hii kuelewa zaidi ukubwa wa neema hii na jinsi ya kuilinda.
https://youtu.be/BuVwLBkqlYQ

Mtume Muhammad ﷺ alitumwa na Allah ﷻ si k**a kiongozi wa Waislamu pekee, bali k**a rehema kwa ulimwengu mzima. Rehema ya...
13/08/2025

Mtume Muhammad ﷺ alitumwa na Allah ﷻ si k**a kiongozi wa Waislamu pekee, bali k**a rehema kwa ulimwengu mzima. Rehema yake ilienea kwa kila kiumbe — maskini na tajiri, rafiki na adui, wanyama na hata mazingira.
Alisamehe waliomkosea, aliwafariji walioumizwa, aliwasaidia wasio na msaada, na aliwafundisha watu heshima na upendo. Katika kila hatua ya maisha yake, aliweka mfano wa subira, haki na uadilifu usio na upendeleo.
Hata wale waliokuwa maadui wakubwa walishangazwa na upole na wema wake, na wengi walikubali ukweli kwa sababu waliona mfano wake wa maisha.

Huu ni mwaliko kwetu sote kuiga mwenendo wake — kueneza amani, kuondoa chuki, na kuishi kwa huruma kwa kila mtu.

Ili kuelewa zaidi tazama video hii.
https://youtu.be/q_oFQJF6Rrw

12/08/2025

Qur'an memorization
Chapter 110: surah al-nasr
Nasr means victory/ help
It has 3 verses. When the Prophet (SAW) was revealed this surah, he knew his life was coming to an end and his mission is over. Islam is complete.

Je, unataka kufaulu maishani?Wengine wanakimbia mali, wengine madaraka, wengine heshima ya watu — lakini cha ajabu, hata...
11/08/2025

Je, unataka kufaulu maishani?
Wengine wanakimbia mali, wengine madaraka, wengine heshima ya watu — lakini cha ajabu, hata baada ya kuyapata yote, bado hawana utulivu wa moyo. Unawahi kujiuliza kwa nini baadhi ya Waislamu wanazidi kutajirika na kufanikwa, huku wengine wakihangaika miaka mingi bila mabadiliko?

Pengine tatizo si juhudi zako… pengine ni njia unayotumia. Kuna siri kubwa ambayo wengi wanapuuzia — na mara unapoiweka kwenye maisha yako, mafanikio yanakuwa sehemu yako bila hata kuyakimbiza.

Tazama video hii ujue ni vipi watu hufaulu.
https://youtu.be/DAh2z7Z0Fos?si=14KY86QZ9HmD5Lfr

Address

Nairobi

Website

https://www.youtube.com/@Ibnummarclips

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when IBN UMMAR CLIPS posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Featured

Share