KOCH FM Radio

KOCH FM Radio Koch FM is a Community Based Organization in the peoples' settlement of Korogocho, Nairobi, Kenya.

The Gunners wamepata ushindi siku ya ufunguzi wa msimu! ๐Ÿ’ช๐Ÿพโšฝ Arsenal 3-0 Coventry CityGame ilikua aje?
21/08/2026

The Gunners wamepata ushindi siku ya ufunguzi wa msimu! ๐Ÿ’ช๐Ÿพโšฝ

Arsenal 3-0 Coventry City

Game ilikua aje?

Greatings my country my people!! Ni Friday Leo tukona guest wetu wa nguvu Tom Dola.
21/08/2026

Greatings my country my people!! Ni Friday Leo tukona guest wetu wa nguvu Tom Dola.

21/08/2026

Kiongozi wa DCP, Rigathi Gachagua, ameitaka serikali kutoa majibu kuhusu mazingira ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Emurua Dikirr, Johana Ngeno, aliyefariki katika ajali ya ndege mwezi Februari. Akiwa katika mkutano wa Mogondo, Gachagua alidai mama wa Ngeno bado hajapata majibu ya kutosha kuhusu kifo cha mwanawe na akamtaka Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen kueleza anachojua kuhusu tukio hilo.

Gachagua aliibua maswali kuhusu mtu aliyedaiwa kuhojiwa baada ya ndege kufika Endebes na baadaye kuachiliwa kufuatia simu, pamoja na madai ya ndege kubadilishiwa mafuta kabla ya safari yake ya mwisho. Pia alihoji kwa nini Ngeno alizikwa kwa haraka na kwa nini mama yake bado anadaiwa kuhangaika kupata mahitaji ya msingi licha ya kuahidiwa msaada.

Kiongozi wa DCP, Rigathi Gachagua, amekataa kufika mbele ya NCIC Agosti 27, akisema atakuwa nje ya nchi kwa safari iliyo...
21/08/2026

Kiongozi wa DCP, Rigathi Gachagua, amekataa kufika mbele ya NCIC Agosti 27, akisema atakuwa nje ya nchi kwa safari iliyopangwa mapema kuanzia Agosti 26 hadi Oktoba 20. NCIC ilimuita kutoa maelezo kuhusu matamshi aliyodaiwa kutoa katika mikutano mbalimbali ya kisiasa.

Lakini mawakili wake wameibua maswali mazito, wakitaka NCIC kutoa video kamili, sauti na nakala rasmi za matamshi hayo ili kuyaweka katika muktadha. Gachagua hata hivyo amesema yuko tayari kushirikiana na tume hiyo.

Polisi wameimarisha usalama katika Kituo cha Mogondor, Narok, kabla ya mkutano wa hadhara wa kiongozi wa DCP, Rigathi Ga...
21/08/2026

Polisi wameimarisha usalama katika Kituo cha Mogondor, Narok, kabla ya mkutano wa hadhara wa kiongozi wa DCP, Rigathi Gachagua. Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya msafara wake kushambuliwa Nakuru, huku Gachagua akidai kuwa kuna njama ya maafisa wa serikali kuvuruga mikutano ya upinzani.

Wabunge wamemuita Waziri wa Usalama wa Ndani, Kipchumba Murkomen, mbele ya Bunge Jumanne, Agosti 25, kujibu kuhusu ongez...
21/08/2026

Wabunge wamemuita Waziri wa Usalama wa Ndani, Kipchumba Murkomen, mbele ya Bunge Jumanne, Agosti 25, kujibu kuhusu ongezeko la vurugu za kisiasa, uhalifu na makundi ya wahuni katika mikutano ya kisiasa. Mbunge wa Gilgil, Martha Wangari, anataka Murkomen kueleza idadi ya visa vya vurugu, vifo na majeruhi vilivyoripotiwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, hatua zilizochukuliwa na maendeleo ya uchunguzi dhidi ya waliohusika.

Mjadala huo ulizidi kuwa mkali baada ya wabunge kuibua madai ya mauaji, mashambulizi dhidi ya raia na wanahabari, unyanyasaji wa kingono na uharibifu wa maeneo ya ibada, hasa kufuatia vurugu za Homa Bay. Baadhi ya wabunge wameonya kuwa uhuni wa kisiasa unaweza kuenea nchini kote kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027, huku wakitaka viongozi wanaochochea vurugu wawajibishwe na wahusika wote wakabiliwe kisheria.

ALIKUWA PADRI FEKI? Mwanamume mmoja amek**atwa kwa tuhuma za kujifanya kuwa padre wa Kanisa Katoliki, huku akidaiwa kuen...
21/08/2026

ALIKUWA PADRI FEKI?

Mwanamume mmoja amek**atwa kwa tuhuma za kujifanya kuwa padre wa Kanisa Katoliki, huku akidaiwa kuendesha ibada, kutoa sakramenti na kutekeleza majukumu ya upadre bila idhini. Dayosisi Katoliki ya Lodwar imesema haimtambui k**a padre na inadaiwa pia alitumia nyaraka za Kanisa zilizoghushiwa.

Inadaiwa mwanamume huyo, ambaye ana mke na watoto wawili, alikuwa akiendesha shughuli hizo kwa jina la Kanisa.

Mazishi yaliyokuwa yakiendelea Mulili, Makindu, Makueni County, yaligeuka kuwa tukio la kusikitisha baada ya upepo mkali...
21/08/2026

Mazishi yaliyokuwa yakiendelea Mulili, Makindu, Makueni County, yaligeuka kuwa tukio la kusikitisha baada ya upepo mkali kuvuruga hema na kujeruhi waombolezaji wengi. Mtu mmoja, anayeaminika kuwa mwanamke mzee wa miaka sitini, amefariki katika vurugu hizo huku wengine wakikimbizwa hospitalini.

Shughuli ya mazishi ililazimika kusitishwa huku waombolezaji wakikimbia kuokoa maisha yao kutokana na mahema yaliyokuwa yakiporomoka na vifusi kurushwa na upepo.

Good Morning,Unajua group  doing amazing work on climate change hapa mtaani? ๐ŸŒฑโ™ป๏ธMaybe wako busy na:๐ŸŒฑ Tree planting & urb...
21/08/2026

Good Morning,
Unajua group doing amazing work on climate change hapa mtaani? ๐ŸŒฑโ™ป๏ธ
Maybe wako busy na:
๐ŸŒฑ Tree planting & urban farming
โ™ป๏ธ Waste management & recycling
๐Ÿšฎ Community clean-ups
๐Ÿ’ก Green energy solutions
๐ŸŒ Ama any other creative project helping our community fight climate change?

๐Ÿ‘‰ NOMINATE THEM! Tuma jina zao kwa 0798 812 522

Koch FM tunataka kusikia kuhusu young people wanaotake action na kufanya real change hapa mtaani. ๐Ÿ’ช๐Ÿพ

๐Ÿ† youth group with more votes will get 2 radio Interview programmes FREE on Koch FM! ๐ŸŽ™๏ธ๐Ÿ”ฅ

Unajua group  doing amazing work on climate change hapa mtaani? ๐ŸŒฑโ™ป๏ธMaybe wako busy na:๐ŸŒฑ Tree planting & urban farmingโ™ป๏ธ ...
20/08/2026

Unajua group doing amazing work on climate change hapa mtaani? ๐ŸŒฑโ™ป๏ธ
Maybe wako busy na:
๐ŸŒฑ Tree planting & urban farming
โ™ป๏ธ Waste management & recycling
๐Ÿšฎ Community clean-ups
๐Ÿ’ก Green energy solutions
๐ŸŒ Ama any other creative project helping our community fight climate change?

๐Ÿ‘‰ NOMINATE THEM! Tuma jina zao kwa 0798 812 522

Koch FM tunataka kusikia kuhusu young people wanaotake action na kufanya real change hapa mtaani. ๐Ÿ’ช๐Ÿพ

๐Ÿ† youth group with more votes will get 2 radio Interview programmes FREE on Koch FM! ๐ŸŽ™๏ธ๐Ÿ”ฅ
Thanks Pulitzer Center for supporting us

Address

Kamunde Road
Nairobi
00100

Telephone

+254745608505

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when KOCH FM Radio posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to KOCH FM Radio:

Shortcuts

Share

Category