
18/08/2025
Kwa masikitiko makubwa, The Jomo Kenyatta Foundation ingependa kuungana na familia, marafiki, na jamii ya wanataaluma wa Kiswahili kuomboleza kifo cha Profesa John Habwe.
Profesa Habwe alikuwa nguzo kuu katika kukuza na kuendeleza Fasihi na Lugha ya Kiswahili nchini na katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Alishirikiana nasi katika kuchapisha vitabu vingi vilivyotunukiwa tuzo mbalimbali, ambavyo vimewasaidia maelfu ya wanafunzi na walimu kote nchini.
Mchango wake hautasahaulika kamwe. Ulimwengu wa Kiswahili umepoteza mwanga, lakini urithi aliouacha utaendelea kung’aa vizazi na vizazi.
Pumzika kwa amani Profesa. Kazi yako njema itadumu milele.