
13/09/2025
SEHEMU YA SITA
"Ni mkesha wa aina gani huo?" Aliuliza. Catherine alichanganyikiwa.
"Mkesha wa kawaida huwa tunakuwa nao kanisani" alieleza.
"Hmm... Oooh! Unaweza kwenda," Mama yake alizungumza, huku macho yake yakiwa kwenye simu. Catherine kimya kimya akatoka.
Alishangaa kwa nini mama yake kila wakati alimfanyia hivyo. Alikuwa mtu mzima na alitakiwa kuwa na uhuru wake, lakini mama yake aliendelea kumtendea k**a mtoto. Julia aliweza kutoka na kuingia muda wowote anaotaka bila kuhojiwa lakini kwake, ilikuwa ni kesi tofauti.
Muda si muda, alifika kanisani na huzuni yake ikapotea.Hakuruhusu mtu yeyote kuharibu hisia zake. Mkesha ulikuwa umeanza, na kwaya ilikuwa inaeendelea na kusifu na kuabudu.
Alimuona rafiki yake Eva kwa mbali,akaelekea kwake.
"Helo Eva" alisalimia.
"Oooh... Catherine habari za jioni" alimkumbatia.
"Nilikuwa nakutafuta tangu nilipofika. Mbona umecehelewa?" Eva Aliuliza.
"Mpenzi wangu kidogo nisahau kuwa kulikuwa na mkesha leo oh...Namshukuru Mungu nilikumbuka ingawa muda ulikuwa umeenda,” Alijibu.
"Asante Mungu umefanikisha. Oya acha ngoma ianze" Eva alisema na wakacheka. Walijiunga na washirika wengine katika kusifu na kuabudu na kucheza.
Catherine na Eva walikuwa marafiki sana tangu utoto wao. Wazazi wao walikuwa washirika wazuri sana kanisani, kwa hiyo walikua pamoja, na kufanya mambo pamoja. Walikuwa na kutoelewana lakini mwishowe waliungana tena. Tangu wakati huo, wote wawili walipenda sana kuigiza.
Shauku hii iliwafanya wasomee sanaa ya maigizo katika chuo cha Bagamoyo. Mungu aliwatumia kweli katika huduma ya maigizo pale kanisani kwao na maisha yalikuwa yanabadilika.
Bro Syaga alikuwa kijana aliyejitolea sana, mwenye tabia njema na mcha Mungu. Pia alihudumu pia kwenye kitengo cha maigizo. Alikuwa kipenzi cha wasichana wengi wa kanisani na wengi wao hawakusita kujionyesha
"Ona eh, Bro Syaga ni mume wangu na hakuna wa kunichukulia" dada mmoja Glory alikuwa akimwambia mwenzake.
"Ahn ahn... Si yule kaka Syaga ambaye dada Faith alisema alimuona ndotoni akiwa amevaa suti na kumtembeza barabarani?" Mwingine aliuliza huku anacheka.
"Upuuzi gani, dada Faith? Huyo ambaye hajui hata kuvaa ndio alisema hivyo?
ITAENDELEA..