
07/09/2025
🌹 Alf Mabrouk 🌹
Alhamdulillah! Kwa neema na rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu, tumeshuhudia hatua hii tukufu ya maisha yako ya kuingia katika ndoa.
Mtume Muhammad (ﷺ) amesema: “Ndoa ni sehemu ya dini yangu, basi mwenye kuoa atimize nusu ya dini yake, na amche Mwenyezi Mungu katika ile nusu iliyobaki.” (Bayhaqi).
Kwa hivyo tunakuombea wewe na mke wako baraka tele, rehema na hidaya kutoka kwa Allah (SWT). Mwenyezi Mungu aibariki ndoa yenu, akufanyieni nyote wawili muwe mavazi kwa kila mmoja wenu, k**a alivyosema katika Qur’an Tukufu:
“Wao ni nguo kwenu, na nyinyi ni nguo kwao.” (Qur’an 2:187)
Tunamuomba Allah awajalie maelewano, upendo wa dhati, furaha isiyo na kikomo, na awajaalie kuwa pamoja katika kila hali hadi kheri ya Akhera. Ndoa yenu iwe chemchemi ya baraka kwa familia zenu na kizazi chenu, na iwe mfano wa kuigwa kwa wengine.
Hongera nyingi sana, ndugu yetu. Mwenyezi Mungu awafungulie milango ya kheri na awajaalie nyumba yenye amani, furaha na baraka daima. 🤲✨