Banza Media

Banza Media Gossip, Drama,News, Lifestyle
follow TV Banza Media Asante kwa sapoti yenyu
Bado kwa zidi kusonga mbele
(1)

17/07/2025

Mrembo aliyeonekana kwenye video ya Te Quiero ya Akiwa na Miaka 3 nyuma ,amemshukuru Rayvanny kwa mchango mkubwa kwenye mafanikio yake.

Kupitia Instagram, ameandika:
β€œKila nikikaa nakutafakari… bila kaka angu nisingekua hapa. Nakosa cha kumlipa. Mungu akubariki πŸ€β€

Leo ni Siku ya Emoji Duniani! 🌍😊Emoji zimekuwa sehemu muhimu ya mawasiliano ya kila siku β€” zinaongeza hisia, utani na ma...
17/07/2025

Leo ni Siku ya Emoji Duniani! 🌍😊
Emoji zimekuwa sehemu muhimu ya mawasiliano ya kila siku β€” zinaongeza hisia, utani na maana kwenye jumbe zetu.

Swali la leo:
Emoji ipi ni favorite yako? πŸ€”
Tuambie moja ambayo huwezi kuacha kuitumia!πŸ‘‡πŸ’¬

πŸ˜„πŸ“±

Leo Ndo nimeamini Duniani Wawili Wawili Nimetoka kusikiliza na kuangalia video ya nakupenda Yake Esther Mamy Daaah mdada...
16/07/2025

Leo Ndo nimeamini Duniani Wawili Wawili
Nimetoka kusikiliza na kuangalia video ya nakupenda Yake Esther Mamy
Daaah mdada anajuwa Sana k**a Nandy vile anakuja ana kataa

Meneno mengi haitoshi
Link πŸ”— below πŸ‘‡

Binafsi sijapenda alichofanyiwa Dogo Paten kwenye haya mahojiano, kwani kuna ulazima wa mtu kueleza maisha yake ya shule...
16/07/2025

Binafsi sijapenda alichofanyiwa Dogo Paten kwenye haya mahojiano, kwani kuna ulazima wa mtu kueleza maisha yake ya shule? Mnajuaje k**a amesoma au hakusoma?

Hawa watangazaji wana wivu na umaarufu wa Dogo Paten, Dogo kawa maarufu katika umri mdogo kuliko wao. Mbona Dogo alifanya mahojiano kwenye redio kibao na amefanya vizuri tu.

Video πŸ‘‡

Kutoka kwenye ukurasa rasmi wa Instagram wa msanii wa Bongo Fleva, , baada ya kutimiza miaka 3 ya ndoa na mume wake , Na...
16/07/2025

Kutoka kwenye ukurasa rasmi wa Instagram wa msanii wa Bongo Fleva, , baada ya kutimiza miaka 3 ya ndoa na mume wake , Nandy aliandika ujumbe wa hisia akielezea mapenzi yake kwa mumewe:

β€œMume wangu kipenzi...
Asante kwa miaka mitatu ya upendo, ushirikiano, na uthubutu wa kila tuliwezalo!

Neno nakupenda peke halitoshi kuelezea maana halisi ya mapenzi yangu kwako.
Upendo wangu kwako unaonyeshwa kupitia matendo yangu, heshima yangu, kujali kwangu, na sala zangu juu yako.

MUNGU aendelee kukupigania kwa ajili ya familia yetu,
Aendelee kukuimarisha kwa ajili yangu,
Aendelee kukupa afya kwa ajili ya Kenaya na mapacha wetu soon...!

Nikwambie kitu? πŸ₯°
You're so handsome – usoni mpaka mfukoni!
Sikuachi leo, kesho, wala kesho kutwa!
Na hata nikitangulia, ubaki kwa ajili yangu ili tuonane tena!

Usimuache Mungu, usiache kunipa sasampa, na MUNGU hatokuacha kamwe.

Let’s enjoy today sababu tuna mengi ya kufurahia.
Baraka ziwe juu yako, my love.

Happy Anniversary, roho yangu ❀️ ”

Tafiti zinaonyesha kuwa wanawake wanaolala na mbwa wanahisi faraja na usalama zaidi ikilinganishwa na wale wanaolala na ...
16/07/2025

Tafiti zinaonyesha kuwa wanawake wanaolala na mbwa wanahisi faraja na usalama zaidi ikilinganishwa na wale wanaolala na paka au binadamu wengine. πŸΆπŸ’€

Mbwa wana tabia ya kulinda na wana uwezo wa kugundua sauti za ajabu, jambo linalosaidia kuleta hali ya usalama wakati wa usingizi. Pia, mbwa hulala kimya kimya usiku kucha β€” takriban asilimia 75 ya muda β€” tofauti na paka ambao huwa na shughuli nyingi wakati wa usiku.

Cha kushangaza, wengi huripoti kuwa hulala vizuri zaidi wakijua tu mbwa wao yuko karibu, hata k**a halali nao kitandani. Paka waliorodheshwa wa mwisho katika kusaidia kupata usingizi au kuleta hali ya usalama.

Mwanamuziki wa Nigeria πŸ‡³πŸ‡¬ Ayra Starr ametangaza rasmi kusaini mkataba wa usimamizi na Roc Nation, kampuni ya burudani il...
16/07/2025

Mwanamuziki wa Nigeria πŸ‡³πŸ‡¬ Ayra Starr ametangaza rasmi kusaini mkataba wa usimamizi na Roc Nation, kampuni ya burudani iliyoanzishwa na Jay-Z.
Hatua hii inaashiria mafanikio makubwa katika safari yake ya kimataifa na kuthibitisha nafasi yake k**a mmoja wa nyota wakubwa wa Afrika. πŸŒπŸ’«

16/07/2025

Rapa maarufu kutoka Marekani, DaBaby, amewaacha mashabiki wengi na mshangao baada ya kusambaza teaser ya wimbo wake mpya ambao umetumia sauti za wanafunzi wa shule kutoka Afrika Kusini πŸ‡ΏπŸ‡¦. Hili ni tukio kubwa linaloonyesha jinsi muziki na sauti kutoka Afrika zinavyoendelea kuhamasisha wasanii wa kimataifa na kuvuka mipaka ya bara hili.

Kitendo hicho kinaongeza heshima kwa utamaduni wa Kiafrika katika muziki wa dunia, kikithibitisha kuwa Afrika sasa ni chanzo muhimu cha ubunifu wa kisauti na usanii.

DaBaby alishiriki kipande cha video ya wimbo huo mpya kupitia ukurasa wake wa Instagram, na mashabiki tayari wameanza kuonyesha furaha na kupongeza hatua hiyo.

Hata hivyo, si DaBaby pekee aliyefanya hivyo – Chris Brown naye aliwahi kutumia sauti ya binti mdogo wa Afrika Kusini aitwaye Naledi Aphiwe kwenye wimbo wake uitwao "Shooter". Chris Brown alimheshimu binti huyo kwa kumlipa kiasi cha dola 3,000 (zaidi ya Tsh milioni 7) kwa kutumia sampuli ya sauti yake. Aidha, Naledi anaendelea kunufaika kupitia mirabaha ya kudumu inayotokana na matumizi ya sauti hiyo katika wimbo huo.

Utafiti mpya umebaini kuwa baadhi ya chura wa k**e hujifanya k**a wamekufa ili kuepuka kujamiiana na chura wa kiume wasi...
15/07/2025

Utafiti mpya umebaini kuwa baadhi ya chura wa k**e hujifanya k**a wamekufa ili kuepuka kujamiiana na chura wa kiume wasiowapenda. Watafiti wamewaona chura hao wakielea juu ya maji kwa mgongo, wakiwa kimya kabisa na hata kushikilia pumzi zaoβ€”yote kwa ajili ya kuepuka tendo la kujamiiana.

Tabia hii ya kujifanya wamekufa inajulikana kisayansi k**a "tonic immobility", na awali ilidhaniwa hutumika tu kujilinda dhidi ya wanyama wanaowinda. Lakini sasa imegundulika pia hutumika na chura wa k**e k**a mbinu ya kuepuka madume wanaowasumbua.

πŸ” Chanzo: mindset.therapy
πŸ“² Fuata kwa zaidi πŸ‘‰

15/07/2025

Kuna msemo usemao, "Kila mtu anaweza kurap, lakini si kila mtu anaweza kuimba au kuandika mashairi yanayovutia."

Katika freestyle yake ya Hip Hop, Dvoice ameonyesha uwezo mkubwa wa flow na ubunifu wa maneno.

Unampa asilimia ngapi kwenye hili?

Address

Parklands

Telephone

+254774652712

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Banza Media posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Banza Media:

Share