
28/07/2025
Naibu Kiongozi wa Chama cha Justice and Freedom Party (JFP), Reuben Kigame, ametangaza nia yake ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Akizungumza katika mahojiano na runinga ya kitaifa siku ya Jumatatu, Julai 28, 2025, mwanamuziki huyo wa nyimbo za injili alisema kuwa kampeni yake itajengwa juu ya misingi ya uongozi wa maadili, uadilifu na tabia bora.