
18/05/2025
Chelsea Women imepata ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Man utd kwenye fainali ya Kombe la FA kwa soka la wanawake, ushindi ambao unaifanya Chelsea kutwaa taji lake la sita la michuano hii na kukamilisha idadi ya mataji matatu ndani ya msimu huu ambapo ilitwaa taji la Kombe la Ligi ikiifunga Man city Women, kisha ikatwaa taji la Ligi kuu Uingereza kwa rekodi ya kutokufungwa kwenye mechi 22 na leo inabeba ubingwa wake mwingine wa Kombe la FA.
Magoli ya mchezo wa leo yamefungwa na Sandy Baltimore ambaye ni mchezaji mpya ndani ya Chelsea huu ukiwa ni msimu wake wa kwanza akifunga magoli mawili kwenye mchezo wa leo, na goli jengine likifungwa na Catarina Macario.
Hongera sana Chelsea Football Club Women