21/05/2025
Usipost ngoma youtube na picha umepiga na simu. Wasanii kujeni hapa tena. Kuna hii tabia ya kuchkua ngoma kwa producer na kueka youtube na picha ya simu. Hapo utakua unamwaga unga.
Kwanza kabisa acha kidogo ni waelimishe. Ngoma ikisha malizwa hua producer anatoa format mbili. Wav na Mp3. Mp3 na wav hazina utofauti mkubwa. Hata ukipewa uskize huezi ipi ni ipi. Lakini kuna tofauti kidogo. Wav ina information full ya mziki. Na ina quality nzuri. Lakini Mp3 iko compressed. Mp3 hua meant for listeners sio uploading.
Sasa hkikisha producer amekupa Wav. Sio mp3. Kwa sababu fans ndo wanadownload mp3. Sasa wewe ukieka mp3 youtube utakua umepotea.
Alafu pale kwa picha, Ukipiga picha na simu ueke youtube, mimi k**a fan ntajua wewe ndo unaanza. Na badala ya kukuskiza , ntaanza kuku judge. Imagine k**a diamond angeeka picha ya youtube iliyòpigwa na simu. Ingekua aje. Badala yake enda photo studio. Piga picha. Na uundiwe youtube thumbnail ya wimbo wako. Fan akikutana nayo. Hatajua wewe ni star ama unaanza. Na k**a audio ni smart. Ataipenda. Ùkitaka vizuri, fanya lyrics pia ùongeze juu ya hio picha.