BWorld Tv

BWorld Tv Ukurasa huu ni kwa ajili ya kupashana habari zote za ulimwengu, kubadilishana fikra na majadiliano kw

15/04/2024

Kwenye mashambulizi ambayo waliyafanya Iran kwenda nchini Israeli, takribani makombora 9 ya balistiki yalifanikiwa kuzifumua kambi kadhaa za kijeshi zilizopo nchini Israeli.
Shambulio moja lilitua kwenye kituo cha anga cha Nevatim kilichopo kwenye Mji wa Negev ambacho kilipigwa makombora 5 ya balestiki.
Makombora hayo yalifanikiwa kuharibu njia kuu ya ndege,
ndege ya usafirishaji ya C-130, na vifaa kadhaa vya kuhifadhi silaha.
Shambulio lingine lilifanyika kwenye kituo cha anga cha Ramon, ambacho pia kipo kwenye Mji wa Negev.
Kituo hiki Kilipigwa na angalau makombora 4 ya balestiki na
Kusababisha uharibifu ambao haujajulikana mpaka sasa.
Taarifa hizi zimetolewa na wachambuzi wa masuala ya kivita
wa Marekani kwa kupitia kituo cha habari cha ABC News.
Kwa upande wa Israeli,
Wizara ya Ulinzi imetoa picha na video za ukarabati wa sehemu iliyoharibika kwenye njia ya ndege iliyopo kwenye
kambi ya Nevatim ambayo ilipiga na makombora ya Iran.
Kwa lugha rahisi ni kwamba, ndege zisizo na rubani ambazo zilitumwa na Iran ndizo ambazo zilidunguliwa na Israeli,
Kwa upande wa Makombora machache ya Balestiki na Hypersonic ambayo waliyatuma, yalifanikiwa kugonga kwenye maeneo husika.
Huku Taifa la Israel wakiendelea kuficha uharibu zaidi ulio tokea lakini taarifa zimeanza kuvujishwa ndani ya maeneo husika.
Credit to siasa makini

Katika kuendeleza vita vya mahasimu wa Kirusi na Marekani mapema Wadukuzi wa Kirusi (KILLNET HACKERS) Wamedukua tovuti y...
18/11/2022

Katika kuendeleza vita vya mahasimu wa Kirusi na Marekani mapema Wadukuzi wa Kirusi (KILLNET HACKERS) Wamedukua tovuti ya Ikulu ya Marekani (WhiteHouse). Wadukuzi hao walifanikiwa kuchunguza baadhi ya nyaraka za SIRI za Ofisi Ya Rais wa Marekani (Tovuti hiyo ilipotea kwa muda wa dakika kadhaa).

Waandamanaji wamesema wataendelea kubaki katika Makazi ya Rais na Waziri Mkuu hadi Viongozi hao watakapojiuzulu rasmi. K...
11/07/2022

Waandamanaji wamesema wataendelea kubaki katika Makazi ya Rais na Waziri Mkuu hadi Viongozi hao watakapojiuzulu rasmi. Kwa mujibu wa Spika wa Bunge la Nchi hiyo, Rais Gotabaya Rajapaksa atajiuzulu Julai 13, 2022

Rais Rajapaksa hajaonekana na hakutoa kauli ya kujiuzulu mwenyewe moja kwa moja. Baadhi ya Ripoti zinadai yupo katika Meli ya Kijeshi

Utulivu umeonekana kurejea katika Mji Mkuu wa Colombo. Baadhi ya Maafisa wa Vyombo vya Usalama wenye silaha wameonekana nje ya Makazi ya Rais, lakini hawajazuia Wananchi kuingia

Vyanzo vya kijeshi vinasema kwamna Rais kwa sasa yuko kwenye meli ya Wanamaji katika maji ya Sri Lanka.
Kaka yake, Waziri Mkuu wa zamani Mahinda Rajapaksa, yuko kwenye kambi ya wanamaji nchini humo, duru zinasema.
Maelfu walifika Colombo Jumamosi wakimtaka ajiuzulu baada ya miezi kadhaa ya maandamano.

Rais amelaumiwa kwa usimamizi mbaya wa uchumi wa nchi, ambao umesababisha uhaba wa chakula, mafuta na dawa kwa miezi kadhaa.
Waziri Mkuu wa sasa Ranil Wickremesinghe pia alisema atajiuzulu kufuatia maandamano ya Jumamosi, ambapo makazi yake ya binafsi yalichomwa moto.

Nondo za Wazee wetu.
11/05/2022

Nondo za Wazee wetu.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeviagiza vyombo vyote vya utangazaji na mitandao ya kijamii nchini kutorusha vi...
06/05/2022

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeviagiza vyombo vyote vya utangazaji na mitandao ya kijamii nchini kutorusha video ya wimbo uitwao 'Mtasubiri Sana' ulioimbwa na msanii Nasib Abdul maarufu Diamond Platnumz kwa kushirikiana na Zuhura Othuman Soud maarufu Zuchu, hadi hapo wasanii hao watakaporekebisha sehemu ya video ya wimbo huo ambayo imeleta ukakasi.

Kwa mujibu wa TCRA, katika video ya wimbo huo kuna kipande kimeonesha wahusika wapo kanisani wanaimba kwaya lakini baadae wakaacha na kuelekea kwingine, kitendo kilicholeta ukakasi miongoni mwa waumini wa madhehebu ya dini na kuleta hisia kuwa ni dharau juu ya dini/madhehemu fulani.

Taarifa ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Jabiri Bakari imeeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya TCRA kupokea taarifa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ya kuzuia usambazaji wa video ya wimbo huo unaopigwa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya utangazaji.

Mahakama Kuu imemuachia huru aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili baa...
06/05/2022

Mahakama Kuu imemuachia huru aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili baada ya kubaini kulikuwa na mapungufu katika mwenendo mzima wa kesi, pamoja na kutofautiana kwa mashahidi.

Sabaya na wenzake walikata rufaa kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Mbali na Sabaya, wengine ni Sylvester Nyegu na Daniel Mbura.

Hata hivyo, Sabaya ataendelea kukaa mahabusu kutokana na kukabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

Address

Colombo

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when BWorld Tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category