Zanzibar Media

Zanzibar Media Mapya yanayojiri Zanzibar utayapata hapa, waandishi Mahiri na waandamizi kutoka Zanzibar. Tuwasiliane kupitia [email protected] na https://www.zenjibarza.net

Zanzibar Media Group ni ukurasa rasmi wa Blog ya Zenjibarza - Sauti ya Wazanzibari https://www.zenjibarza.net , Google Podcasts @ Zanzibar Media. Kwa khabari mbali mbali usikose kutembelea, na kwa maoni na ushauri tafadhali tuandikie kupitia [email protected]

28/10/2025

Kuna baadhi ya watu wanaoeneza taarifa za kukatisha tamaa, wakidai hakuna tofauti na miaka iliyopita. Tusikubali kuyumbishwa! Dosari ndogo ndogo ni jambo la kawaida katika kila uchaguzi duniani. Tusirudie makosa ya kuwasaidia CCM kwa maneno yetu au kwa kukata tamaa. Sisi ni washindi amini hilo, simama imara, na songa mbele kwa matumaini.

Asalaam alaykumAlhamdulillah Alhamdulillah, mtoto wetu aliyekuwa amepotea jana tumempata asubuhi ya leo, akiwa mzima Alh...
30/08/2024

Asalaam alaykum
Alhamdulillah Alhamdulillah, mtoto wetu aliyekuwa amepotea jana tumempata asubuhi ya leo, akiwa mzima Alhamdulillah.. tunakushukuruni kwa dua zenu.

Mtoto amepotea..Abdullah Mahmoud Abdullah Al Khatry, mwenye umri wa Miaka 15, amepotea maeneo ya Kariakoo DSM, mara ya m...
29/08/2024

Mtoto amepotea..

Abdullah Mahmoud Abdullah Al Khatry, mwenye umri wa Miaka 15, amepotea maeneo ya Kariakoo DSM, mara ya mwisho kuonekana alikuwa kwenye geti lq shule yake Azania Secondary School.. 29/08/2024.

Tunaomba ushirikiano wenu kwa atakayemuona au kujua taarifa zake.. Mawasiliano namba zifuatazo:

+255713210966
+255628989249
+255746 804 821
+255776777778
+255655176174

Na Ismail Jussa MZEE KARUME ALISEMA AKIMNUKUU SITTI BINT SAAD,  "MSIJITIE KIWEWE, ZANZIBAR INA WENYEWE."Leo tuwadokeze k...
08/02/2024

Na Ismail Jussa

MZEE KARUME ALISEMA AKIMNUKUU SITTI BINT SAAD, "MSIJITIE KIWEWE, ZANZIBAR INA WENYEWE."

Leo tuwadokeze kidogo kuhusu kisiwa kiitwacho Latham island (kwa Kiswahili wenyeji wa Zanzibar wanakiita Fungu Mbaraka) ambacho ni katika milki ya Zanzibar.

Kisiwa hicho kiliitwa Latham kutokana na meli ya kiingereza Latham ambayo ilitia nanga hapo mwaka 1878. Hadi mwaka 1898 kikiitwa Fungu Kizimkazi na hatimaye kiliitwa Fungu Mbaraka kwa jina la Ahmed Mbarak aliyepewa ruhusa na Sultan kuzamua mali katika meli iliyozama hapo na akapata utajiri mkubwa.

Latham ilifanywa rasmi kuwa sehemu ya Zanzibar kuanzia tarehe 19 October, 1898. Sir Lloyd Mathews ndiye aliyepewa kazi hiyo na Sultani na akaenda kupachika bendera ya Zanzibar na kuweka tangazo rasmi tarehe hiyo.

Sir Lloyd Mathews alikuwa ndiye First Minister (kwa lugha ya sasa ni k**a Prime Minister) wa mwanzo wa Zanzibar na anatajwa kuwa ndiye aliyeunda jeshi la mwanzo la Zanzibar. Ingawa riwaya nyengine inasema Sir John Kirk ndiye aliyeunda jeshi la mwanzo kukabiliana na Karl Peters (wa Tanganyika) hapo August 1885 lakini akazuiwa na Sir Salisbury, Foreign Secretary (Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza zama hizo) asipigane na Karl na akavunjika moyo sana.

Wajerumani waliwahi kukidai mwaka 1910 na kujibiwa rasmi na Serikali ya Uingereza tarehe 13 April, 1911 kuwa ni cha Zanzibar; tokea hapo hakijawahi kudaiwa tena na dola yoyote.

Mwaka 1959 kupitia Legal Notice No. 56 Zanzibar ilikitangaza Latham Island kuwa ni Bird Sanctuary chini ya Sheria ya Wild Bird Prorection.

https://youtu.be/1y8Id_DVBXs
22/07/2021

https://youtu.be/1y8Id_DVBXs

Siku ya Jumatatu ya tarehe 19 Julai 2021, siku moja tu baada ya uchaguzi mdogo wa Konde, wazee kisiwani Pemba walikutana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzi...

Mwonekano wa Msikiti wetu ambao umekwama ujenzi wake. Msikiti upo Chasasa, Wete. Mkabala na madrasa ya Maalim Hilal. +25...
02/05/2021

Mwonekano wa Msikiti wetu ambao umekwama ujenzi wake. Msikiti upo Chasasa, Wete. Mkabala na madrasa ya Maalim Hilal.

+255 776 494 975 Ali Ali(wasiliana na sisi)
+255 719 320 407 Ali Ali - Tigopesa
+255 772 818 181 Said Ali - Ezypesa

Ali Hilal
Zanzibar.

Masheikh   kesi haijakamilika ushahidi hii kweli ndio haki na usawa na ule utawala bora?!
09/04/2021

Masheikh kesi haijakamilika ushahidi hii kweli ndio haki na usawa na ule utawala bora?!

08/04/2021
Ramadhani ya Nane wanafungia gerezani, wapo waliofiliwa na wake zao, wapo waliofiliwa na watoto wao, na hadi leo kesi za...
07/04/2021

Ramadhani ya Nane wanafungia gerezani, wapo waliofiliwa na wake zao, wapo waliofiliwa na watoto wao, na hadi leo kesi zao haziendi... Hii ni dhuluma...

Address

18th November Street 3885
Muscat
130

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Zanzibar Media posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Zanzibar Media:

Share