I.F tv Online

I.F tv Online Welcome to our Official Iraqw Foundation Television 📺 Online (I.F tv Online) FB Page Karibu kweny

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Kenan Laban Kihongosi amezindua Tamasha kubwa la Samia Connect Arusha 🔥🔥🔥
21/08/2025

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Kenan Laban Kihongosi amezindua Tamasha kubwa la Samia Connect Arusha 🔥🔥🔥

NGOs ZATAKIWA KUWAJIBIKANa WMJJWM-DodomaMashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs), yametakiwa kuwa wazi na kuwajabika katika...
11/08/2025

NGOs ZATAKIWA KUWAJIBIKA

Na WMJJWM-Dodoma

Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs), yametakiwa kuwa wazi na kuwajabika katika utekelezaji wa majukumu yao hasa kuwahudumia wananchi kupitia miradi mbalimbali wanayotekeleza kwa maendeleo ya jamii. 

Hayo yamesemwa leo Agosti 11, 2025 na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis wakati akifungua Kongamano la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa mwaka 2025 linalofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma kuanzia Agosti 11-13.

Naibu Waziri Mwanaidi ameeleza kwamba uwazi na uwajibikaji wa Mashirika hayo ndiyo msingi wa kutambuliwa kwa mchango wao katika maendelo ya Taifa. 

“Viongozi na wasimamizi wa miradi ya kimaendeleo ya uchumi katika mashirika yenu nawaomba kuzingatia uwajibikaji, pamoja na kuwa tayari kubadilishana uzoefu miongoni mwa Mashirika ili kuwa na maendeleo endelevu kwa nchi yetu” amesema Naibu Waziri Mwanaidi.

Aidha amesisitiza kwamba kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanapaswa kutoa elimu ya kiraia kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu ili kutimiza haki yao ya kidemokrasia. 

Awali, akimkaribisha mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju amesema Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ni nyenzo muhimu katika kutoa huduma kwa wananchi, hivyo ameyaasa Mashirika hayo kuendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine wa maendeleo kuhakikisha wananchi wananufaika na utekelezaji wa miradi mbalimbali. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mwantum Mahiza amesema Bodi hiyo inaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha NGOs zinafuata kanuni na taratibu zilizopo ili kufanikisha maono yao katika kuwahudumia wananchi.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Gasper Makala asema Baraza hilo limeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha Mashirika hayo yanashirikiana na Serikali na wadau wengine katika kuwahudumia wananchi kupitia utekelezaji wa miradi.

11/08/2025
MKURUGENZI MBULU TC KATIKA KILELE CHA MAONYESHO YA 8-8 KANDA YA KASKAZINI AGOSTI 8.📸 HABARI PICHA: Mkurugenzi wa Halmash...
08/08/2025

MKURUGENZI MBULU TC KATIKA KILELE CHA MAONYESHO YA 8-8 KANDA YA KASKAZINI AGOSTI 8.

📸 HABARI PICHA: Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Ndg. Rehema Said Bwasi akishiriki katika kilele cha Maonyesho ya 31 ya Kilimo mifugo na uvuvi na Sherehe za NANE NANE Kanda ya Kaskazini yanayofanyika katika Viwanja vya 88 Njiro Jijini Arusha Leo Agosti 8.2025.

KAULI MBIU
"Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025."

📸HABARI PICHA: Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na uzalishaji Mali Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mratibu wa Maonyesho ya Kil...
08/08/2025

📸HABARI PICHA: Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na uzalishaji Mali Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mratibu wa Maonyesho ya Kilimo mifugo na uvuvi na Sherehe za NANE NANE (8-8) Kanda ya Kaskazini Bw. Daniel Loiruck akishiriki katika kilele cha 8-8 Leo agosti 8.2025 katika Viwanja vya 88 Njiro Jijini Arusha.

KAULI MBIU "Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025."

📸 PICHA: Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Aboubakari Kuuli akishiriki katika kilele cha Maonyesho ya 31...
08/08/2025

📸 PICHA: Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndg. Aboubakari Kuuli akishiriki katika kilele cha Maonyesho ya 31 ya Kilimo mifugo na uvuvi 'Nane Nane' 2025 Kanda ya Kaskazini yanayofanyika katika Viwanja vya 88 Njiro Jijini Arusha Leo Tar 08.Agosti.2025.

KAULI MBIU "Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025."

*📸PICHA: Katibu Tawala Wilaya ya Mbulu Ndg. Paulo Bura akishiriki katika kilele cha Maonyesho ya 31 ya Kilimo, mifugo, n...
08/08/2025

*📸PICHA: Katibu Tawala Wilaya ya Mbulu Ndg. Paulo Bura akishiriki katika kilele cha Maonyesho ya 31 ya Kilimo, mifugo, na uvuvi Kanda ya Kaskazini ambayo yamenyika Leo Tar 08.08.2025 Jijini Arusha.*

**KAULI MBIU*
*_"Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025."_*

TUPO hapa sunrise  na meya  🔥🔥
08/08/2025

TUPO hapa sunrise na meya 🔥🔥

Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Maxmillian Matle Iranqhe amemkaribisha Jijini humo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk...
22/04/2025

Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Maxmillian Matle Iranqhe amemkaribisha Jijini humo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Mashaka Biteko wakati wa Ziara yake ya Siku tano Mkoani Arusha.

LEOPARD TOURS WAKABIDHI PIKIPIKI 20 KWA JESHI LA POLISI ARUSHATaasisi ya Leopard Tours imekabidhi pikipiki 20 kwa Jeshi ...
24/01/2025

LEOPARD TOURS WAKABIDHI PIKIPIKI 20 KWA JESHI LA POLISI ARUSHA
Taasisi ya Leopard Tours imekabidhi pikipiki 20 kwa Jeshi la Poslisi Mkoani Arusha ikiwa. Ni sehemu ya kuunga Mkono juhudi za kuimarisha Ulinzi na usalama Mkoani humo, hafla fupi iliyofanyika Leo Januari 24, 2025 kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Akizungumza wakati akikabidhi pikipiki hizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa Leopard Tours, Zuher Lazal amesema kuwa hatua hiyo ya kugawa pikipiki imetokana na juhudi zilizowekwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Siluhu Hassan kwenye Sekta ya utalii ambayo inaweesha kutoa michango kwa jamii kupitia Jeshi la Poslisi.

Pia amemshukuru Mhe paul Christian Makonda ambaye amekuwa nguzo kubwa kwa kuendeleza juhudi hizo kwenye Sekta ya Utalii kwa kuzingatia kuwa Arusha ndio Kitovu cha Utalii ambapo Jeshi la Polisi ndio ndio msingi wa kuimarisha Usalama.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameishukuru Taasisi hiyo kwa uthubutu wake wa Kutoa ajira kwa vijana wa Kitanania na faida inayotokana na shughuli za utalii kurejeshwa kwa jamii kupitia kwa jeshi la polisi ili kutekeleza majukumu yao kwa wepesi.

“Nafasi yangu katika Mkoa huu ni Pamoja na kuweka mazingira mazuri kwa kila Mwananchi wa Mkoa huu kutekeleza majukumu yake bila changamoto yoyote ikiwemo jeshi letu la Polisi”. Amesema Mhe. Makonda.

Hata hivyo amelitaka Jeshi la Polisi kuongeza kasi ya kuimarisha Ulinzi na Usalama ili kuhakikisha kuwa Mkoa wa Arusha unakuwa kitovu cha Amani Duniani.

Address

East Africa Community Road
Arusha
P.O.BOX7302

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when I.F tv Online posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to I.F tv Online:

Share