Maasai Channel

Maasai Channel 𝗠𝗮𝗮𝘀𝗮𝗶 𝗖𝗵𝗮𝗻𝗻𝗲𝗹
𝑻𝒆𝒏𝒆𝒃𝒐 𝑴𝒂𝒕𝒆𝒔𝒉𝒆𝒕 𝑶𝒍𝒐𝒔𝒉𝒐 𝑳𝒂𝒏𝒈

21/10/2025

ALAIGWANANI JACKSON OLE TETEYIO

RC MAKALLA AZINDUA MSIMU WA SHEREHE ZA MILA ZA KIMASAI*  _Awashukuru kwa kutoa fursa ya Ushiriki wa upigaji Kura Oktoba ...
20/10/2025

RC MAKALLA AZINDUA MSIMU WA SHEREHE ZA MILA ZA KIMASAI*

_Awashukuru kwa kutoa fursa ya Ushiriki wa upigaji Kura Oktoba 29_

_Sherehe hizo kuhusisha Tohara kwa Kundi rika la Vijana zaidi ya 2, 000_

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla leo Jumatatu Oktoba 20, 2025, amezindua sherehe za msimu wa tohara kwa jamii ya Kimasai nchini Tanzania, akiishukuru Jamii hiyo kwa kuheshimu sheria na Miongozo ya nchi kwa kusimamisha shughuli za Tohara Oktoba 29, 2025 ili kuruhusu Makundi rika mbalimbali kwenda kupiga kura kuwachagua Viongozi wanaowataka kuwaongoza kwa miaka mitano ijayo.

Sherehe hizo maarufu kama Enkipaata zimezinduliwa kwenye Kijiji cha Oldonyosapu Wilaya ya Arumeru zikitarajiwa kuhusisha zaidi ya Vijana 2,000 wa kundi rika la Irmegoliki litakalodumu mpaka Oktoba 2032, akiwahakikishia usalama na amani wakati wote kuanzia sasa, siku ya upigaji wa kura na baada ya upigaji kura pamoja na kuwahimiza wananchi wote kushiriki kuchagua Viongozi wanaowataka katika uchaguzi huo.

"Ninawashukuru kwanza kwa kunipa heshima ya kuzindua sherehe hizi na zaidi ni kwamba pamoja na kuwa na mila zenu bado mmeheshimu taratibu na ratiba nyingine za serikali niwaombe tarehe 29 Viongozi wote mpaze sauti katika maeneo yote watu wapate haki ya kupiga kura na sisi kama Serikali tuwahakikishie kuwa uchaguzi utakuwa salama na wenye amani." Amesema Mhe. Makalla.

Kwa upande wake Kiongozi Mkuu wa Jamii ya Kimasai Isack Meijo Ole Kisongo na Mlezi wa kundi rika hilo linaloingia kwenye msimu wa tohara wamesema sababu ya kuiheshimu Oktoba 29, 2025 ni kutokana na Jamii hiyo kutambua umuhimu wa upigaji wa kura, wakiahidi kuwa Jamii kinara katika kumpa kura nyingi zaidi Mgombea wa nafasi ya Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na mapenzi yao kwake na maendeleo mengi aliyowatendea jamii ya Kimasai nchini katika sekta ya jamii na ufugaji.

20/10/2025

JAMII YA KIMASAI NCHINI TANZANIA YAKATAA MAANDAMANO, WAKIAHIDI KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA

_Waahidi kuwachagua walinda amani na mshikamano wa Taifa_

Viongozi wa Jamii ya Kimasai nchini Tanzania maarufu kama (Malaigwanan) wametoa tamko lao rasmi kwa nchi nzima, la kuunga Mkono kufanyika kwa uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa Oktoba 29, 2025, wakilaani uwepo wa hamasa ya kufanyika kwa maandamano siku hiyo wakiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kuchagua Viongozi wanaowataka.

Viongozi hao wametoa tamko hilo katika eneo la Donyomorwak Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro kwenye Mkutano wao wa kawaida wa Orkiama ambapo akisoma tamko hilo kwaniaba ya Viongozi hao, Bw. Jeremia Laizer, Katibu wa Malaigwanani Tanzania, ameeleza pia kwamba Jamii hiyo itamuunga Mkono Kiongozi mwenye kutanguliza mbele maslahi ya wananchi pamoja na kulinda amani na utulivu wa Tanzania.

"Tunawahimiza wananchi wote kudumisha amani, mshikamano na utulivu, kuanzia ngazi ya shina, kijiji, kata, tarafa, wilaya, mkoa, kanda hadi Taifa zima, tukiepuka maneno ya uchochezi, migawanyiko, na fitina. Tuchague maendeleo, umoja, na mustakabali mwema wa vizazi vya sasa na vijavyo. Tuwe nguzo ya amani, nuru ya matumaini, na urithi wa thamani kwa Taifa letu. Tanzania kwanza, amani kwanza." Amesema Bwana Laizer.

Kwa upande wake mgeni rasmi wa Mkutano huo ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Namelok Sokoine amewapongeza malaigwanani hao kwa msimamo wao huo pamoja na kuonesha kuridhika na utendaji wa serikali ya awamu ya sita, akiwataka kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo Jumatano ya Oktoba 29, 2025.

Aidha baadhi ya Viongozi wengine wa jamii hiyo pia wameahidi kuwa mabalozi wa kueneza amani katika maeneo yao katika kipindi hiki cha uchaguzi Mkuu, wakisisitiza athari za maandamano yasiyofuata taratibu kuwa ni pamoja na uharibifu na uvunjifu wa amani ambapo waathirika wakubwa mara zote wamekuwa wanawake, watoto pamoja na wazee.

18/10/2025
TUPO LONGIDO KARIBUNI SANA
29/09/2025

TUPO LONGIDO KARIBUNI SANA

KAZI KAZI
20/09/2025

KAZI KAZI

KARIBU TUKUFANYIE KAZI BORA NA YA UHAKIKA
20/09/2025

KARIBU TUKUFANYIE KAZI BORA NA YA UHAKIKA

09/09/2025

아멘 🙏

04/09/2025

IRPASERENGO🔥🔥🔥

04/09/2025

ERETOTO ENKAI - LEAH MELITA

Emputoto Alaigwanani le nkaji oormamasita te Museregi
04/09/2025

Emputoto Alaigwanani le nkaji oormamasita te Museregi

Enkaji Emaa
04/09/2025

Enkaji Emaa

Address

Longido
Arusha
23501

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Maasai Channel posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category