
21/07/2025
Mahak**a Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam Julai 18,2025 imemuhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 jela na faini ya shilingi milioni moja Prince Deogratius Daniel mwenye umri wa miaka 45, mkazi wa Bamba Gezaulole Manispaa ya Kigamboni Dar es Salaam baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka binti mwenye umri wa miaka 15 mwanafunzi wa kidato cha kwanza
Akisoma hukumu hiyo Mh Nestory Baro amesema kuwa Mahak**a imeridhishwa na ushahidi uliowasilishwa Mahak**ani hapo ambapo pasi na chembe ya shaka umemuunganisha Mtuhumiwa huyo kutenda kosa hilo.
Awali imeelezwa kuwa Mtuhumiwa alimchukua binti huyo kijiji kwa mama yake Novemba 11,2023 na kuahidi kuwa yeye na mkewe ambaye yupo Dar es Salaam watamlea na kumsomesha binti yake ili kumsaidia ulezi kutokana na hali duni ya maisha aliyonayo.
Baada ya binti kufika kwenye nyumba ya huyo baba yake mlezi hakuwahi kumuona mke wake na badala yake mnamo mwezi Disemba 2023 tarehe asiyoikumbuka majira ya usiku alimbaka kwa mara ya kwanza binti huyo na kumkataza kuongea na majirani. Mei 20,2024 majira ya saa Prince Deogratious alimbaka tena binti huyo na baada ya hapo binti aliweza kuwahadithia majirani na kumfikisha kituo cha Polisi kwa hatua za kisheria na kupelekea kutiwa hatiani.