11/04/2026
Chombo cha anga cha Marekani (Orion) kinapofika karibu na Dunia, hakishuki taratibu.
Kinaingia kwa kasi ya takriban 40,000 km/saa kasi ambayo akili ya kawaida haijaizoea.
Hebu tuiweke hii kwenye picha halisi:
Ndege ya abiria husafiri kwa 900 km/saa, hivyo;
Dar → Dodoma
Ndege: Saa 1
Dar → Dubai
Ndege: Masaa 5–6
Dar → Africa Kusini
Ndege: Masaa 3–4
Dar → New York
Ndege ya abiria: Masaa 15–18
Chombo cha anga (Orion) kinasafiri kwa kasi ya 40,000 km/saa: Hivyo;
Dar → Dodoma: chini ya dakika 1 (sekunde 40-50)
Dar → Dubai: karibu dakika 5–6
Dar → Africa Kusini: Dakika 4–5
Dar → New York, Marekani: chini ya dakika 20
Ndiyo tofauti ya kusafiri ndani ya Dunia, na kurudi kutoka anga za mbali.
KINACHOTOKEA KWENYE ANGA
Orion inapogusa anga la Dunia, haimaanishi imekutana na hewa laini bali ni k**a ukuta usioonekana.
Hewa inabanwa kwa nguvu, na joto linapanda hadi karibu 2,700°C.
Chombo kinaonekana k**a kimondo kinachowaka.
Ndani, wanaanga wanasukumwa chini kwa nguvu ya hadi 4G (4G maana yake mwili wako unahisi uzito mara 4 zaidi ya kawaida, k**a una wa kilo 70 utajihisi k**a kilo 280, hata kichwa kinakuwa kigumu kuinua)
USAHIHI WA HALI YA JUU UNAHITAJIKA
Sio kuingia tu duniani, ni kuingia kwa usahihi mkubwa.
Pembe/angle ya kuingia ikiwa ndogo sana, chombo kinaweza kuruka na kurudi angani kikapotea.
Ikiwa kubwa sana, joto na G-force vinaongezeka na kuwa hatari.
Hapa hakuna kubahatisha, tofauti ndogo tu ya angle inaweza kubadilisha kila kitu.
Na yote haya yanatokea ndani ya takriban dakika 10 hadi 20 tu, dakika chache, lakini ndizo zenye kuamua k**a safari inamalizika salama au la.
MWISHO WA SAFARI
Kutoka kasi ya 40,000 km/saa
hadi chini ya 30 km/saa ndani ya dakika chache.
Parachuti zinafunguka.
Kelele zinapotea.
Bahari inapokea chombo taratibu.
Imeandikwa na Jonalist