Sunrise Radio Tz

Sunrise Radio Tz SUNRISE RADIO INAHAKIKISHA UNAPATA HABARI ZILIZO NA UHUAKIKA KUTOKA KILA KONA YA TANZANIA NA NJE YA TANZANIA

05/12/2025

Baada ya kuapishwa mstahiki Meya wa jiji la Arusha Maxmillian Mathle Iranqhe amehaidi kukamilisha viporo vya miradi iliyo baki wakati akiwa Meya wa baraza lililopita

05/12/2025
03/12/2025

*Dkt Samia :Wanaouwania urais 2030 wasituvurugie nchi*

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amesema kazi iliyopo ni kutibu majeraha yaliyotokana na vurugu za Oktoba 29, hivyo wanaosaka uongozi 2030, wasivuruge nchi.
Dkt Samia ameeleza hayo leo Jumanne Disemba 2,2025 akizungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.

“Nimesema kazi yetu sasa ni kutiba majeraha na hapa nataka nizungumze na watoto wangu ‘vijana’ wanaoangalia mbele hawa wengine waliopo nje. Wanaongalia mbele 2030 safari hiyo isiende kutuvurugia nchi yetu,”

“Nilizungumza na mawaziri wangu, nikamwambia namuangalia mmoja mmoja, una maslahi na huko, kaa nje kafanye huko usifanye ndani ya Serikali yangu.Nimekuweka hapo ukatumikie wananchi ‘interest’ yako utaikuta mbele, Mungu ndio anajua nani kiongozi,”

Amesema mtu anaweza kujipanga na kuwa na mikakati, lakini usifanikiwe, akitolea mfano wapo waliokuwa na uwezo ikiwemo nguvu za kifedha ila hawakufanikiwa, akisisitiza Mungu ndiye anayejua.

“Ile safari ya 2030 isiendea kutuharibia nchi,”amesisitiza Rais Dkt Samia.

02/12/2025

Rais Samia: Nyinyi ni nani? Msitupangie!
Rais Samia Suluhu Hasana amesema Tanzania ni nchi huru haitakubali kupangiwa namna ya kufanya mambo yake na mataifa mengine kwa kisingizio cha misaada au kitu kingine chochote kile, badala yake itaamua mambo yake kadiri ya mahitaji ya watu wake.
Akiongea na wazee wa Dar es Salaam, Desemba 02, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere Rais Samia alisema baadhi ya mataifa wamekuwa wakiunga mkono madai yasiyokuwa na msingi ya baadahi ya vyama vya siasa kwa malengo ya kuivuruga nchi.
Alisema baadhi vya vyama vya siasa vilijitoa vyenyewe kwenye Uchaguzi Mkuu, kwa kuogopa kushindwa na sasa wanatafuta visingizio kwa kusaidiwa na kufadhiliwa na watu wa nje.
“Katika ile aibu ya kuepuka kushindwa uchaguzi wanaweka visingizio. Visingizio vyote hivi vinaungwa mkono na nje (mataifa ya nje) hawana hata aibu, nje huko wanakaa wanasema Tanzania ifanye moja, ifanye mbili, ifanye tatu, halafu ndiyo itakuwa hivi, who are you?,” alihoji Rais Samia.
“Niwaulize ndugu zangu, kwao hayatokei? Tumenyanyua sauti kusema ya kwao? Wanadhania bado wao ni wakoloni kwetu? Kitu gani? ni fedha chache wanzotugawia, na fedha yenyewe sasa haipo, tunafanya biashara ili wao wapate na sisi tupate ndipo tunaposimamia.”
Alisema Tanzania ni k**a mwanake mzuri ambaye anapiganiwa na wanaume wawili na kwamba siasa ya kutofungamana na upande wowote ambayo haibagua mtu wa kushirikiana naye ndiyo inayowasumbua kwa kuwa kila mtu anavuta upande wake.
Aliwataka watanzania kutambua kuwa nchi ina utajiri mwingi wa rasilimali na hizo zimekuwa chanzo cha chokochoko za mataifa ya nje na hivyo kuwataka kushik**ana, kuwa imara na kulilinda taifa lao.

01/12/2025

Baada ya majina matatu kurejeshwa na kufanyika uchaguzi wa kumpata meya wa jiji la Arusha hatimaye Maxmillian Mathle Iranqhe aibuka mshindi na kuteuliwa kuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha

Ikumbukwe kuwa Ushindi huu aliupata akiwa akitetea kiti Nicho

27/11/2025

*Wahusika 1,736 wa vurugu za Oktoba 29 kuachiwa*

Msamaha wa Rais Dkt Rais Samia Suluhu Hassan kwa walioshiriki vurugu za Oktoba 29, mwaka huu unatarajiwa kuwaachia huru jumla ya vijana 1,736 kati ya 2,045 waliok**atwa kwa kosa la kushiriki tukio hilo.

Kwa mujibu wa Waziri wa Katiba na Sheria Jumaa Homera, hadi jana Novemba 25, 2025 jumla ya vijana 607 waliachiwa na kwamba kazi hiyo inaendelea.

Ukiacha idadi hiyo ya watakaoachiwa kupitia msamaha huo, watuhumiwa 309 wataendelea kushikiliwa kwa shughuli za upekuzi wa kina na kujiridhisha na makosa yao.

Rais Dkt Samia alitangaza msamaha huo Novemba 14, 2025 alipohutubia ufunguzi wa Bunge la 13, jijini Dodoma, akitaka walioshiriki kwa kufuata mkumbo wasamehewe

Homera ametoa kauli hiyo leo, Jumatano Novemba 26, 2025 alipozungumza baada ya kutembelea ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), jijini Dodoma.

Samsung kibingwa zaidi kwa kuanziakianzio cha 85,000 tuu.
04/10/2025

Samsung kibingwa zaidi kwa kuanziakianzio cha 85,000 tuu.

18/09/2025

KUANZIA KESHO MAZULIA KUUZWA KUANZIA ELFU 3

Address

P. O. Box 11064
Arusha

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sunrise Radio Tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Sunrise Radio Tz:

Share

Category

TANZANIA BILA CORONA INAWEZEKANA

TANZANIA SALAMA