
01/08/2025
"Vunjo tutatafuta namna gani tutakavyo komboa mtu mmoja mmoja hasa kwenye suala la ajira, elimu na mikopo mbalimbali inayotolewa na halmashauri zetu, inahitaji mtu makini wakufuatilia, mniamini mimi Prosper Daudi Tesha ninatosha kwenye nafasi ya ubunge...
..mimi nipo tayari kuwatumikia na nipo tayari kutumwa, wazee hampaswi kuhangaika tena, sasa hivi mnapaswa mtulie mnitume mimi kijana wenu niwatumikie." Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa, Mkurugenzi wa Kampuni ya RGI na Mwenyekiti wa madini ya vito Taifa (FEMATA), Ndugu Prosper Daudi Tesha akizungumza mbele ya wajumbe wa CCM katika Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro Agosti 01, 2025.