Arusha District Council

Arusha District Council Government Institution

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Viongozi pamoja na wageni mbalimbali wakiwa kweny...
24/01/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Viongozi pamoja na wageni mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya Tuzo za Mlipakodi Bora wa mwaka 2023/24 iliyofanyika katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Januari, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Tuzo ya mlipa kodi binafsi mwenye hadhi...
24/01/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikabidhi Tuzo ya mlipa kodi binafsi mwenye hadhi ya juu, Mmiliki wa Kampuni za Bakhresa Group, Said Salim Bakhresa kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa The Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Januari, 2025.

24/01/2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Mjumbe Maalum wa Rais w...
23/01/2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Mjumbe Maalum wa Rais wa Djibouti Mhe. Ismail Omar Guelleh ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Mahmoud Ali Youssouf mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Januari, 2025.

*“Arusha ndio mkoa pekee ambapo mwananchi akitaka kutoboa kimaisha anapaswa kuishi. Naomba kurudia tena hata kwa wageni ...
23/01/2025

*“Arusha ndio mkoa pekee ambapo mwananchi akitaka kutoboa kimaisha anapaswa kuishi. Naomba kurudia tena hata kwa wageni mliokuja—wenyeviti wa bodi, Dada yangu Ditopile, pamoja na wengine wote ukitaka kutoboa kimaisha na kuishi na pesa k**a hauishi Arusha umasikini ni sehemu yako. Ndiyo maana hata viwanja vya Mkoa wa Arusha vinapanda bei".amesema Makonda*
> Mkuu huyo wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema hayo wakati wa zoezi la ulipaji fidia katika mradi wa magadi soda eneo Engaruka, Monduli.
https://www.instagram.com/p/DFKpqyhtw1o/?igsh=MWdscWFtd2I5MmdzOQ==

23/01/2025

New life begins in the heart of Ndutu, Ngorongoro Conservation Area (NCA). The nutrient-rich plains become a nursery as thousands of wildebeest calves take their first steps, marking the start of the Great Migration.

Waziri Afya Mhe. Jenista Mhagama leo Januari 23,2025 amekutana na uongozi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya huduma za Afya ...
23/01/2025

Waziri Afya Mhe. Jenista Mhagama leo Januari 23,2025 amekutana na uongozi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya huduma za Afya ya nchini Korea na kuuelezea kuwa katika kipindi cha miaka mitano (5), Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imenufaika na ushirikiano wa pamoja kati yake na Korea kupitia utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Nne wa Sekta ya Afya (HSSP-IV) pamoja na Mpango Mkakati wa Tano.

Pia wamejadili mambo yanayohusu Sekta ya Afya ikiwemo kuimarisha huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto katika mikoa ya Pwani na Dodoma.

Tanzania na Korea zimeazimia kuendelea kujenga uwezo kwa Maabara ya Kitaifa ya Afya ya Umma juu ya udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza, mpango wa kiufundi wa usimamizi wa hospitali sambamba na ukarabati na ujenzi wa wodi maalum za watoto wachanga wagonjwa (NICU).

"Kwa sababu hiyo, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Serikali ya Korea pamoja na taasisi ya (Korea Foundation for International Healthcare, KOFIH) kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Tanzania, hususan katika sekta ya afya," amesema Waziri Mhagama

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania(NECTA) Dkt. Said Mohamed amesema watahiniwa wa shule waliopata ubora w...
23/01/2025

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania
(NECTA) Dkt. Said Mohamed amesema watahiniwa wa shule waliopata ubora wa ufaulu katika madaraja ya 1 - III kwa mwaka 2024 ni 221,953 sawa na asilimia 42.96.

Amesema mwaka 2023 watahiniwa waliopata ufaulu wa madaraja ya | - III walikuwa 197,426 sawa na asilimia 37.42, hivyo ubora wa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 5.54 ikilinganishwa na mwaka 2023.

Akitangaza matokeo hayo mkoani Dar es Salaam, Dkt. Said Mohammed amesema ubora wa ufaulu wa madaraja ya I - Ill ni mzuri zaidi kwa wavulana ikilinganishwa na wasichana ambapo wavulana ni 119,869 sawa na asilimia 48.90 ya wavulana wote wenye matokeo na wasichana ni 102,084 sawa na asilimia 37.59 ya wasichana wote wenye matokeo.

Picha ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha akizungumza na mmoja wa Wawakilishi wa Taasisi ya Bill & Melinda Gates Foun...
23/01/2025

Picha ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha akizungumza na mmoja wa Wawakilishi wa Taasisi ya Bill & Melinda Gates Foundation,walipomtembelea Ofisini kwake leo tarehe22/01/2025.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Arusha,Bwana Suleiman Msumi leo tarehe 23/01/2025  amekutana na kufanya mazungumzo w...
23/01/2025

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Arusha,Bwana Suleiman Msumi leo tarehe 23/01/2025 amekutana na kufanya mazungumzo wawakilishi wa Taasisi ya Bill & Melinda Gates Foundation toka Nchini Marekani.

Lengo la ziara ya Taasisi hiyo ya Bill & Melinda Gates Foundation ni kufanya tafiti za mazao ya Kilimo kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania ( TARI-SERIAN) kwenye Halmashauri ya Arusha kwa kubainisha changamoto zinazowakabili wakulima na kuona namna bora ya kuzitafutia ufumbuzi.

Baadhi ya changamoto zilizoainishwa kwa wakulima katika Halmashauri ya Wilaya ya Arusha ni pamoja na uzalishaji duni wa mazao ya kilimo, wakulima kukosa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea,Viuatilifu, mbegu pamoja na changamoto za mabadilko ya Tabia Chini.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha bw.Suleiman Msumi amewashukuru na kuwahakikishia wageni hao toka Taasisi ya Melinda and Bill Gates Marekani kwa kuichagua Halmashauri ya Arusha kutekeleza miradi ya utafiti ambayo itasaidia na kuongeza ufanisi katika kuzalisha mazao ya kilimo.

*NOTI MPYA*Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba amesema kuwa Noti Mpya za Tanzania zenye Saini ya Waziri...
22/01/2025

*NOTI MPYA*

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba amesema kuwa Noti Mpya za Tanzania zenye Saini ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na yeye mwenyewe, za toleo la mwaka 2010, zitaingia kwenye mzunguko kuanzia tarehe mosi Februari mwaka huu.

Gavana Tutuba amesema hayo wakati akimkabidhi Mhe. Dkt. Nchemba, Noti kifani za shilingi elfu kumi, elfu Tano, Elfu Mbili na Shilingi Elfu moja, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, kwa mujibu wa Sheria na Taratibu zinazosimamia masuala ya fedha nchini.

“Mheshimiwa Waziri, ninayofuraha kukujulisha kuwa zoezi letu la uchapaji upya wa Noti kwa marejeo ya toleo la mwaka 2010, limekamilika na tayari tumewajulisha wananchi kupitia taarifa niliyoitoa kupitia Gazeti la Serikali” alisema Bw. Tutuba.

Gavana Tutuba alifafanua kuwa Noti hizo zitatumika sambamba na Noti zilizopo hivi sasa, zinamwonekano wa Noti zinazotumika hivi sasa zilizotolewa Mwaka 2010, ikiwemo alama za usalama, ukubwa, rangi na mambo mengine, isipokuwa ina marekebisho kwenye saini ya Waziri wa Fedha, na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

“Saini ya aliyekuwa Waziri wa Fedha ambaye hivi sasa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango imebadilishwa na kuwekwa Saini yako Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Saini ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania aliyestaafu, Prof. Florens Luoga, imebadilishwa na kuwekwa Saini ya Gavana wa Benki Kuu wa sasa, Bw. Emmanuel Tutuba” aliongeza Bw. Tutuba.

Akizungumza baada ya kupokea sampuli za Noti hizo mpya, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, alimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu jambo hilo kufanyika na kumpongeza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, kwa kusimamia mchakato wa uchapaji wa Noti hizo kwa weledi na uadilifu mkubwa.

“Mpaka kufikia hatua hii ni heshima kubwa kwa Taifa letu na inaendeleza heshima ya wataalam wetu mnavyoweza kusimamia kwa umakini mambo yenye maslahi mapana kwa nchi yetu” Alisema Dkt. Nchemba.

Mhe. Dkt. Nchemba aliridhia Noti hizo ziingizwe kwenye mzunguko na kuanza kutumika k**a ilivyopangwa tarehe moja Februari mwaka huu.

Address

Arusha, T
Arusha

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Arusha District Council posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share