16/07/2025
"Mnajua vyema kwamba Chadema wamesema hawaingii kwenye uchaguzi mpaka tufanye Reforms na modality yao wanayoisema, wanasema watazuia uchaguzi. Nataka nitoa ushauri kwa unyenyekevu sana, ni kweli Sisi CCM tunaweza kuamua kuendelea na uchaguzi na tukafanya uchaguzi na tukashinda lakini kushinda uchaguzi sio jambo kubwa sana, kuitawala nchi ambayo imemegukameguka kwasababu ha makovu ya uchaguzi ndiyo jambo kubwa zaidi, kuiletea nchi maendeleo iliyomeguka kutokana na makovu na majeraha ya uchaguzi ni kazi ngumu sana.
Sisi k**a CCM tunaweza kuamua kwamba tuendelee- tutaendelea na tutashinda. Lakini ebu jaribu kuwaza tangu siku unapoapishwa kuna watu wanaendelea kukupinga mpaka utakapomaliza miaka yako mitano, yaani kuna watu hawakuingia kwenye uchaguzi, hawakushiriki, pengine hawakutambui halafu wanaanza kukupinga tangu siku unapoapishwa mpaka utakapotoka miaka mitano. Maendeleo utayaletaje? Utapata matatizo na Jumuiya za kimataifa na ndani ya nje utapata matatizo utashindwa kwenda kwa kasi kwa maendeleo yetu k**a inavyotakiwa na itakuwa sio vizuri.
Mimi nashauri kwamba, CCM ina wanachama zaidi ya milioni kumi na kitu, hatuhitaji kuogopa, tuamue kuwaruhusu hawa wa Chadema kuwapa reforms chache ambazo zinaweza kufanyika kwasasa, tuwape a minimal reform, haichukui muda. Tuwape, tuingie nao kwenye uchaguzi. Kwani wewe hufahamu kwamba CCM ina wanachama zaidi ya Milioni kumi na kitu?ambao wapo tayari? kwanini tuingine kwenye mchezo halafu tunayecheza naye hayumo? Ni sawasawa na kuingia kwenye mechi huku kuna Simba, huko inatakiwa iwe Yanga, halafu Yanga haipo, tunacheza wenyewe halafu tunapiga goli, si mechi.
Nashauri sana badala ya kuendelea na No Reforms, No election, CCM awepo mtu wa kutafakari. Mimi k**a mwanachama wa CCM na k**a Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM na pia Mtanzania, nashauri sana tungeamua kukubali kufanya hiyo reforms, najua shughuli za Bunge zimesitishwa lakini uhai wa Bunge bado upo mpaka mwezi wa nane, zitafutwe wiki mbili au tatu, zitengenezwe reforms wanazozihitaji hata k**a sio zote, lakini ziwe chache zitakazowafanya waingie kwenye uchaguzi halafu waingie tuwapige, reforms zimefanyika, wameingia, tunawapiga."-Askofu Josephat Gwajima