Lumen Media Tanzania

Lumen Media Tanzania Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Lumen Media Tanzania, Media/News Company, Arusha.

Lumen TV
TV channel
We are located Arusha Tanzania | Channel No.317
No.186 | 91.7fm | Braeking News| Sports |

05/07/2025

Je ulikuwa unalifahamu hili

Klabu ya simba imeandika hayo katika ukurasa wao wa instagram👇👇👇👇👇-Taarifa rasmi kuhusu uwanja wa mchezo wa marudiano wa...
15/05/2025

Klabu ya simba imeandika hayo katika ukurasa wao wa instagram👇👇👇👇👇
-
Taarifa rasmi kuhusu uwanja wa mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika itatolewa baada ya mchezo wa awali

Klabu ya Arsenal inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza imetambulisha jezi zao mpya za nyumbani zitakazotumika msimu uja...
15/05/2025

Klabu ya Arsenal inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza imetambulisha jezi zao mpya za nyumbani zitakazotumika msimu ujao wa 2025/26.
UNAUPA MAKSI NGAPI U*I HUU???

Maoni yako yatasomwa mda huu kwenye kipindi cha lango kuu kilichopo mbashara kupitia lumen redio 91.7 pamoja na youtube ...
15/05/2025

Maoni yako yatasomwa mda huu kwenye kipindi cha lango kuu kilichopo mbashara kupitia lumen redio 91.7 pamoja na youtube chanel yetu ya lumen online tv.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Makonda, ametoa wito kwa waandishi wa habari kubadilika na kuandika habari zenye kujen...
29/04/2025

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Makonda, ametoa wito kwa waandishi wa habari kubadilika na kuandika habari zenye kujenga jamii badala ya zile zenye kuchochea migogoro au kueneza hofu.
-
Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyofanyika leo katika Hoteli ya Gran Melia jijini Arusha, Mhe. Makonda amesema waandishi wa habari wana nafasi kubwa ya kuunda taswira na mwenendo wa jamii kupitia kazi zao.
-
"Waandishi wa habari wanaweza kuamua jamii iwe vipi kupitia kazi zao, k**a vile mavazi, chakula na mwenendo wote wa maisha." Amesema Mhe. Makonda mbele ya hadhira iliyojumuisha wanahabari, viongozi wa serikali na wadau wa sekta ya habari.
-
Aidha, Mhe. Makonda ametumia fursa hiyo kuwaalika wanahabari kushiriki kikamilifu kwenye jukwaa la kiuchumi7 litakalofanyika Mei 3, 2025, mkoani Arusha, akieleza kuwa hilo ni jukwaa muhimu kwa waandishi kupata taarifa sahihi na kuzifikisha kwa wananchi ili kuchochea maendeleo.
-
Maadhimisho hayo yamewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya habari, huku ujumbe mkuu ukiwa ni kulinda na kuendeleza uhuru wa vyombo vya habari kwa maendeleo ya taifa.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Tanzania imepiga hatua kubwa za Mae...
25/04/2025

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Tanzania imepiga hatua kubwa za Maendeleo ndani ya Miaka 61 ya Muungano Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii na kuwa kielelezo cha Mafanikio ya Muungano Barani Afrika.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipoweka jiwe la Msingi la Ujenzi Wa Barabara ya Kibada-Mwasonga Wilaya ya Kigamboni, Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Rais Dkt Mwinyi amesema Wananchi wa pande zote mbili wanaendelea kunufaika na matunda ya
Muungano tangu Kuasisiwa kwake na kufanikisha dhamira ya Waasisi wake
Ya Kuleta Uhuru,Umoja na Maendeleo ya Watanzania .

Rais Dkt, Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,Samia Suluhu Hassan kwa Kuendelea Kuimarisha Muungano kwa kuzipatia Ufumbuzi Changamoto za Muungano kwa kupitia vikao vya Pamoja vya Majadiliano k**a ilivyofanywa na Viongozi waliopita.

Halikadhalika Rais Dkt,Mwinyi amefafanua kuwa Amani ya kudumu na Umoja wa Watanzania ni Tunu Muhimu zinazopaswa kulindwa na kila Mtanzania..

Akizungumzia Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara hiyo aliyoiwekea Jiwe la Msingi na Miradi mingine ya Maendeleo ni matokeo ya kuwepo kwa Amani na kuiwezesha Serikali kutekeleza Mipango ya Maendeleo.

Ametoa Wito kwa Watanzania Kuendelea kulinda Amani Ili Taifa lipige hatua zaidi za Maendeleo na kwa kuwa huu ni Mwaka wa Uchaguzi amewataka kutumia haki yao kuchagua Viongozi na kuhakikisha Uchaguzi hauwi chanzo cha kuhatarisha Amani ya Nchi na kuweka Mbele Maslahi ya Taifa.

Akizungumza kwa Niaba ya Waziri wa Ujenzi , Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia Jerry John Silaa amesema Barabara Hiyo itaifungua Wilaya ya Kigamboni Kiuchumi na kuwaunganisha Wananchi katika harakati za Kijamii.

Barabara Hiyo itagharimu Kiasi cha Shilingi Bilioni 83.8 hadi kukamilika kwake inajengwa na Kampuni ya Estim Construction Limited.

Wahenga tukusanyike hapa !!!!!-Maoni yako yatasomwa kwenye kipindi cha lango kuu kilichopo mbashara mda huu kupitia lume...
24/04/2025

Wahenga tukusanyike hapa !!!!!
-
Maoni yako yatasomwa kwenye kipindi cha lango kuu kilichopo mbashara mda huu kupitia lumen redio pamoja na youtube chanel yetu ya lumen online tv
CC:

24/03/2025

“Unawahitaji watu wakati wote, uwe na cheo,usiwe na cheo unahitaji watu, uwe na fedha usiwe na fedha unahitaji watu; kwenye maisha. Mungu ametungenezea mazingira ya kuwategemea wengine, Hata daktari unapougua, unahitaji daktari mwingine wa kukutibu na hata siku ukifa hutajizika utazikwa na wengine unawahitaji watu” DKT. BITEKO

haahaha
14/03/2025

haahaha

14/03/2025
13/02/2025

Tuambie na wewe ni nini kiswahili cha neno password

Tusikilize na ututazame mbashara kesho majira ya saa kumi na nusu jioni hadi saa kumi na moja na nusu jioni katika kipin...
10/02/2025

Tusikilize na ututazame mbashara kesho majira ya saa kumi na nusu jioni hadi saa kumi na moja na nusu jioni katika kipindi cha evening trumpet ambapo tutakuwa na Bi. Margaret Mngumi ambae ni msuluhishi wa migogoro ya bima Tanzania akizungumzia Uanzishwaji wa Ofisi ya usuluhishi na majukumu yake

Address

Arusha

Telephone

+255683336379

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Lumen Media Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share