10/01/2025
Bwana ni ijumaa mpya kwetu, asante Bwana kwa neema hii ya kuiona siku mpya. Bwana naomba siku hii ikawe ni siku iliyobeba baraka na shangilio la kufanikiwa, ikawe siku mpya ya kurejeshewa, kupata, kuinuka, iliyo ya furaha
Bwana hakika sisi na wanadamu ndani mwetu hatuishiwa mahitaji Bwana. Tunazo ndoto za maisha tuyatamaniyo kuyaishi Eee Bwana, tutendee wema wako na tunaomba utufanyie wepesi nasi katika kwikwi za matamanio yetu
Hakika wewe Bwana ni mwema kila wakati, ukuu wako hauchunguziki wala hauna mfano
Asante Bwana kwa zawadi ya maisha maana hii ndio zawadi kuu. Kuiona siku mpya huwa ni neema zako tu, si ujanja wetu umetustahilisha
Bwana onekana katika kila eneo la uhitaji wetu, tutendee wema wako katika maisha yetu haya tuombayo Eee Bwana ututende kwa ajili yetu