23/02/2026
Ajali mbaya imeripotiwa katika eneo la Kwa Idd, wilayani Arumeru, mkoani Arusha, kufuatia basi la kampuni ya Dar Express kugongana na daladala lililokuwa likisafirisha abiria.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, watu kadhaa wamejeruhiwa, huku baadhi yao wakiwa katika hali mbaya na kuhitaji uangalizi wa haraka wa kitabibu. Magari yote mawili yamepata uharibifu mkubwa, hasa katika sehemu za mbele.
Mamlaka husika zinaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo.