
13/07/2025
HUYU NDIYE SEMIO SONYO (UNCLE SONYO) – RADIO 5 FM ARUSHA
Baada ya kuonekana k**a Miongoni mwa Watangazaji BORA wa mikoani kupitia Platform ya nina haya yakusema.
Katika anga ya redio nchini Tanzania, vipaji vingi vinaibuka, lakini ni wachache sana wanaoweza kusimama imara kwa muda mrefu na kudhihirisha ubora wa hali ya juu katika utangazaji na uzalishaji wa vipindi. Moja ya majina hayo machache ni Semio Sonyo, anayejulikana zaidi k**a Uncle Sonyo wa Radio 5 FM ya Arusha.
Uncle Sonyo si mtangazaji wa kawaida. Ni kipaji kinachoweza kuibua hisia, kuelimisha, kuburudisha na kuchochea fikra za wasikilizaji kwa wakati mmoja. Kutoka kwenye vipindi vya habari, burudani, michezo hadi vipindi maalum vya kijamii na kitaifa — Sonyo amekuwa akidhihirisha uwezo mkubwa wa kitaaluma na ubunifu wa hali ya juu huyu ni Kiraka (Mult Purpose Presenter).
Ni moja kati ya watangazaji nchini Tanzania wenye uwezo mkubwa katika kufanya Mahojiano katika nyanja zote,Elimu,Siasa,Uchumi Afya Mazingira,Kilimo,michezo na hata Burudani.
Sauti yake ya kuvutia, uchambuzi makini, maandalizi ya kina na namna anavyomiliki hewani ni vitu vinavyomtofautisha. Hata katika mazingira ya ushindani mkubwa, Uncle Sonyo ameendelea kuwa chaguo la wengi, si tu katika Jiji la Arusha, bali pia mikoa mingine na hata wasikilizaji wa mtandaoni kote nchini.
Katika ulimwengu wa redio unaohitaji ubunifu wa kila siku, Sonyo ameweza kudumu kwa ubora usiopungua. Anaeleweka, anakubalika, anaheshimika na zaidi ya yote, anastahili tuzo ya kitaifa, si kwa upendeleo, bali kwa haki inayotokana na kazi yake ya kipekee.
Uncle Sonyo ni alama ya vipaji vya mikoani vinavyostahili kung’ara kitaifa. Ni wakati sasa mchango wake utambuliwe rasmi – kwa jina, kwa kazi, na kwa tuzo.
Ahsante Radio Doctor kwa Jicho makini la kumuona