28/06/2025
PACHA WA WAZIRI DKT BITEKO ACHUKUA FOMU YA UBUNGE JIMBO JIPYA LA KATORO
Kulwa Biteko, Muambata wa Balozi wa Tanzania nchini Uganda anayeshughulikia masuala ya fedha ametangaza nia na kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya ubunge jimbo jipya la Katoro wilayani Geita mkoani Geita
Kulwa Biteko ambaye ni pacha wa Dkt.Doto Biteko naibu waziri mkuu na waziri wa nishati nchini amechukua fomu ndani ya chama cha mapinduzi wilaya ya Geita
Biteko pia amewahi kuwa mgombea wa nafasi hiyo jimbo la Busanda ambalo ni jimbo mama kabla ya kukatwa kwa jimbo la Katoro na kuwa mshindi wa pili mwaka 2020 kwa kura 665
Zoezi la kuchukua fomu za ubunge ndani ya chama cha mapinduzi limeanza leo juni 28, nchini kote