04/12/2025
Mungu ni Ukweli, hili jambo limekuwa likitumika k**a hoja ya msingi kwa waislamu kwa miaka mingi, wengi wetu tuliamini kuwa serikali haikufanya usawa kuingia mkatababa "MOU" na makanisa.
Na kwa wakati huo tulikuwa sahihi kuamini hivyo kwa sababu ya kutokuwa na taarifa za kina na zenye kujitosheleza.
Leo hii baada ya kusikiliza maelezo yanayotolewa na katibu mkuu Baraza la Maaskofu Tanzania Fr Kitima.
Imetuwezesha kulielewa suala hili vizuri zaidi na kwa upana unaostahili.
Hakuna hata moja alilosema linapingana na ukweli halisi kuwa dhamira ya kanisa ni kusaidia ustawi wa jamii kwa mtizamo malengo na maono ya kanisa.
Hii inamaanisha:
Moja kanisa ni taasisi yenye malengo yake k**a zilivyo taasisi nyingine kwa msingi huo taasisi yeyote ile inasimamia malengo yake kwa mujibu wa sheria na mamlaka za nchi.
Pili: Suala la kuingia makubaliano maalumu na serikali ni jambo na fursa inayotolewa na sheria zetu, ikiwa taasisi fulani imeamua kutumia fursa hiyo haimaanishi taasisi nyingine yeyote haiwezi kutumia fursa hiyo.
Kwa maana hiyo, na hii ni kwa ndugu zangu waislamu hasa wale ambao wamekuwa wakiisikia propaganda hii kwa muda mrefu juu ya kanisa kuingia makubaliano maalumu na serikali wajue kulilaumu kanisa ni kutojitendea haki kwa namna moja au nyingine kwa sababu tu wameitumia fursa hiyo ambayo hata taasisi za kiislamu zingeweza au zinaitumia hivyi sasa, changamoto huwenda zikawa ni ukubwa na umahiri wa matumizi husika.
Ukweli huu lazima uzingatiwe, historia za kikoloni ziliweka mazingira mazuri ya kanisa kuweza kuwa na uwezo wa kutumia fursa hizi kwa ufanisi zaidi jambo ambalo kwa waislamu historia hiyo hiyo haikuweka mazingira mazuri kwao kuweza kuzitumia fursa hizo kwa ufanisi na hii haitufanyi sasa kulilaumu kanisa kwa kushindwa kwetu kutumia fursa hizo.
Ningependa ndugu zangu waislamu kutafakari kidogo suala hili, je uwezo wa mashirika yetu ya kiislamu unaweza kuyalinganisha na uwezo wa mashirika ya kikatoliki na kiprotestanti?
Na hasa kwenye suala zima la Organization, Structural, Management and Professionalism? Je kushindwa kwetu juu ya haya tunaweza kulilaumu Kanisa?
Masheikh wetu wanaoshikilia kulilaumu kanisa je walikuwa wanafanya nini wakati wote huo kuji organize ili kupigania maslahi ya waislamu ambayo leo hii wanataka kutuaminisha kuwa kanisa lina agenda ya siri na waislamu?
Je kushindwa kuwa na chombo chenye nguvu k**a TEC, ELCT ni kwa sababu ya kanisa?
Nani alituaminisha waislamu kuwa serikali yetu inaendeshwa kwa misingi ya udini? Nani alituuzia hii propaganda iliyo maarufu "mfumo kristo" miongoni mwa waislamu?
Wakati wote huo masheikh wakiilamu serikali hawatendei haki walikuwa wanailaumu serikali gani?
Jana nimesikia sheikh mmoja anasema huwenda kanisa lina mpango wa kujipanga kwa ajili ya uongozi au kushika mamlaka ya nchi ikiwemo kupachika viongozi wa nafasi za juu wakati ujao, Ni lipi kosa la wenzetu kujipanga kuwa na watu wao kwenye nafasi za uongozi?
Na nini kinazuia umoja huu tunaouona hivyi sasa wa kuitetea serikali unaofanywa na masheikh pia usitumike kutengeneza dira ya waislamu na wao kuwa viongozi wa juu kwenye serikali?
Na ikiwa masheikh wamekubaliana kuitetea serikali kwa msingi kuwa inaendeshwa na muislamu jambo moja kuu na la msingi kujiuliza je msimamo huu ni kwa maslahi ya umma au ya watu au kikundi? Je kuna plani inayofuatia?
NB: Kutoka kwa Mdau wetu
K**a una maoni usisite kupanua mjadala
Admin