28/10/2025
MARUNGU YA BODI YA LIGI YATEMBEZWA
K**ati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), imeipa Pamba Jiji ushindi wa magoli matatu na alama tatu katika mchezo wake dhidi ya Dodoma Jiji.
Dodoma Jiji imepoteza mchezo huo ambao wao walikuwa wenyeji kutokana na kushindwa kuandaa mchezo huo kikamilifu jambo lililosababisha mtanange huo kuvunjika.
Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Ligi, mchezo huo ulivunjika dakika ya sita (6) wakati ambao Dodoma Jiji ilikuwa inaongoza kwa goli 1-0 baada ya taa za uwanjani kuzima na wenyeji kushindwa kufanya jitihada zozote za kurejesha mwanga.
Kwa upande mwingine, TPLB imeitoza faini ya shilingi milioni 20, klabu ya Mtibwa Sugar kwa kosa la kuanza msimu wa NBC Premier League na kucheza michezo minne (4) bila kuwa na kocha mkuu mwenye ujuzi stahiki.
Nao TRA United wametozwa faini ya shilingi milioni 15, kwa kosa la kuanza Ligi Kuu na kucheza michezo mitatu (3) bila kuwa na kocha mkuu wemye ujuzi stahiki.
Imeandikwa na kusambazwa na R Kay