NLFA MEDIA

NLFA MEDIA 📰 News | 🏆 Sports | 🎬 Entertainment
✨ Your trusted source for updates & stories

27/08/2026

"Naomba uniruhusu nitumie jukwaa hili kumpongeza sana Mhe.Deogratius Ndejembi kwa kuaminiwa na Mhe.Rais...na kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na pili nimpongeze sana Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jicho lake la Mwewe la kuweza kumuona Mhe.Ndejembi.."-Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu Nchemba

27/08/2026

Halmashauri Kuu ya CCM iliyoketi leo chini ya Mwenyekiti wake Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeadhimia kumfukuza uanachana aliyekuwa Makamu wa Rais Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi.

Akiongea leo Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Asha Roze Migiro amesema ““Kamati Kuu imejadili kuhusu suala la nidhamu na maadili ambalo lilikuwa linamkabili Emmanuel Nchimbi, na baada ya kuzingatia taarifa zote zilizokuwepo ilithibitika kwamba katiba ya CCM na kanuni zake zilikiukwa, na hivyo Nchimbi amefukuzwa uanachama”

 : Halmashauri Kuu ya CCM chini ya uenyekiti wa Rais Samia Suluhu Hassan imempendekeza Deogratius Ndejembi (43) kuwa Mak...
27/08/2026

: Halmashauri Kuu ya CCM chini ya uenyekiti wa Rais Samia Suluhu Hassan imempendekeza Deogratius Ndejembi (43) kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Asha-Rose Migiro, ametangaza uamuzi huo usiku wa leo, Jumatano, Agosti 26, 2026, katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam.

Dkt. Migiro amesema jina la Ndejembi litapelekwa Bungeni kwa hatua zinazofuata.

Mkuu wa Majeshi wa Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye pia ni mtoto wa Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni, anasem...
26/08/2026

Mkuu wa Majeshi wa Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye pia ni mtoto wa Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni, anasema kuwa atagombea Urais mwaka 2031.

Kainerugaba, 52, mara nyingi ametajwa kuwa mrithi wa baba yake.

Kainerugaba, ambaye anaongoza vuguvugu la kisiasa linaloitwa 'Patriotic League of Uganda', aliwahi kutangaza kuwa angegombea katika uchaguzi uliopita mwezi Januari lakini hakutimiza hilo.

26/08/2026

:Serikali imetoa kauli juu ya suala la upotevu wa watoto ambao umekua ukiripotiwa katika Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii ambapo imewaasa wazazi kuwa makini na kushiriki ipasavyo ulinzi wa watoto katika maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo ya elimu na michezo.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobass Katambi akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kaskazini Unguja ,Mheshimiwa Shadia Haji Omar aliehoji upotevu wa watoto na hatua zinazochukuliwa na Jeshi la Polisi na upatikanaji wa taarifa zitakazosaida upatikanaji wa watoto hao.

Waziri Katambi amesema pia serikali iko mbioni kuwa na mifumo maalumu ya kiusalama ya kufuatilia matukio mbalimbali ikiwemo kamera maalumu kwenye maeneo mbalimbali ambazo zitasaidia upatikanaji wa watoto hao pamoja na Mali zilizopotea.

Nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes, ametangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA nchini England, baada ya k...
26/08/2026

Nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes, ametangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA nchini England, baada ya kuchaguliwa na wachezaji wenzake kufuatia msimu wake bora wa 2025/26.

Bruno alikuwa mhimili muhimu wa Manchester United msimu uliopita, akivunja rekodi ya Ligi Kuu ya England kwa kutoa assist 21, na kusaidia timu yake kumaliza katika nafasi ya tatu na kufuzu kushiriki katia Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Tuzo hii ina uzito wa pekee kwa sababu Mchezaji Bora wa PFA huchaguliwa kwa kura za wachezaji wenyewe, hivyo Bruno ametambuliwa na wataalamu wenzake aliokutana nao uwanjani msimu mzima.

Hii ni tuzo nyingine kubwa kwa Bruno baada ya kutangazwa mchezaji bora wa ligi ya EPL msimu wa 2025/26.

Klabu ya Manchester United imethibitisha rasmi kumsajili Carlos Baleba kutoka Brighton & Hove Albion, kwa dili lenye tha...
25/08/2026

Klabu ya Manchester United imethibitisha rasmi kumsajili Carlos Baleba kutoka Brighton & Hove Albion, kwa dili lenye thamani ya hadi Pauni 70.

Baleba, ambaye ni kiungo wa Cameroon, amejiunga na United na kusaini mkataba wa miaka mitano, huku klabu hiyo ikiwa na chaguo la kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Rais Samia Suluhu Hassan amepokea na kuridhia ombi la kujiuzulu kwa Makamu wa Rais, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, k...
25/08/2026

Rais Samia Suluhu Hassan amepokea na kuridhia ombi la kujiuzulu kwa Makamu wa Rais, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, kuanzia tarehe 4 Septemba 2026.

Taarifa iliyotolewa leo, Agosti 25, 2026 imeeleza kuwa Rais Samia amepokea barua ya ombi hilo na kuliridhia, huku hatua hiyo ikimaanisha kuwa nafasi ya Makamu wa Rais itakuwa wazi kuanzia tarehe iliyotajwa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Serikali itafuata taratibu za kikatiba za kumpata Makamu wa Rais mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Uamuzi huo unafuatia Nchimbi kuwasilisha ombi la kujiuzulu nafasi hiyo, huku taratibu za kumpata mrithi wake zikitarajiwa kuanza kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Emmanuel Nchimbi, ametangaza uamuzi wa kustaafu siasa na utumish...
25/08/2026

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Emmanuel Nchimbi, ametangaza uamuzi wa kustaafu siasa na utumishi wa umma.

Nchimbi amesema leo, Agosti 25, 2026, amemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kumjulisha kuhusu uamuzi huo pamoja na nia yake ya kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais.

Amesema kujiuzulu kwake kutaanza rasmi tarehe 4 Septemba 2026, akieleza kuwa amefanya uamuzi huo kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nchimbi ameeleza kuwa tarehe 27 Agosti 2025 alimuahidi Rais Samia kuwa angemsaidia yeye na taifa kwa uwezo wake wote na kwa uaminifu, huku akiahidi pia kuachia nafasi hiyo endapo Rais angeona anahitaji Makamu mwingine wa Rais.

“Nimejiridhisha pasipo shaka kuwa Mhe. Rais anatamani mabadiliko, hivyo nimeamua kutimiza ahadi yangu”, amesema Nchimbi.

Aidha, amemshukuru Rais Samia pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa imani waliyoonyesha kwake, huku akiwashukuru Watanzania kwa ushirikiano waliompa wakati wote aliokuwa katika utumishi wa umma.

Nchimbi amesisitiza kuwa pamoja na kustaafu siasa na utumishi wa umma, ataendelea kuwa raia mwema wa Tanzania.

NBC PREMIERE LEAGUE | FULLTIME YANGA SC 4-0 JKT TANZANIA⚽ 28’ Kangwanda⚽ 34’ Bacca⚽ 39’ Boka⚽ 64’ Shalulile P.GOLI LIPI ...
24/08/2026

NBC PREMIERE LEAGUE | FULLTIME

YANGA SC 4-0 JKT TANZANIA
⚽ 28’ Kangwanda
⚽ 34’ Bacca
⚽ 39’ Boka
⚽ 64’ Shalulile P.

GOLI LIPI LIMEKUVUTIA SANA KWENYE USHINDI HUU WA YANGA?

Address

AICC
Arusha
23107

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when NLFA MEDIA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share