NLFA MEDIA

NLFA MEDIA 📰 News | 🏆 Sports | 🎬 Entertainment
✨ Your trusted source for updates & stories

 : Ripoti mpya kutoka Global Statistics Wire imezitaja klabu 10 zenye thamani kubwa zaidi barani Afrika kwa kuzingatia w...
27/05/2026

: Ripoti mpya kutoka Global Statistics Wire imezitaja klabu 10 zenye thamani kubwa zaidi barani Afrika kwa kuzingatia wingi wa mashabiki pamoja na nguvu ya uwepo wa kidijitali (digital footprint).

Katika orodha hiyo, Al Ahly SC ya Misri imeongoza kwa kuwa na mashabiki takribani milioni 59, ikifuatiwa na Zamalek SC yenye mashabiki milioni 17.

Klabu ya Simba SC imek**ata nafasi ya tatu Afrika ikiwa na mashabiki takribani milioni 13.3, mbele ya Raja Casablanca ya Morocco yenye mashabiki milioni 12.1.

Kwa upande wa Young Africans SC, wao wameorodheshwa nafasi ya nane barani Afrika wakiwa na mashabiki takribani milioni 6.

Powered by Fian Security

Kutoka NLFA MEDIA,   🕌 njema.
27/05/2026

Kutoka NLFA MEDIA, 🕌 njema.

27/05/2026

: Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ashatu Kijaji, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, ili kuongeza idadi ya watalii na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa na kwamba Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi za utalii zinazostahili kutambulishwa zaidi katika masoko ya Kimataifa.

Kijaji amesema pamoja na kuendeleza kampeni za kutangaza maeneo yanayofahamika, kuna haja ya kuibua na kuvitangaza vivutio vingine ambavyo bado havijapata umaarufu mkubwa duniani, kwani hatua hiyo itasaidia kupanua wigo wa bidhaa za utalii na kuvutia wageni wengi zaidi kutoka mataifa mbalimbali.

Waziri Kijaji ametoa wito kwa wadau wa sekta ya utalii, vyombo vya habari na wananchi kushiriki kikamilifu katika kutangaza vivutio vya Tanzania kupitia majukwaa mbalimbali hivyo kuwezesha nchi kunufaika zaidi na fursa za kiuchumi zinazotokana na sekta ya utalii, ikiwemo ajira, mapato ya fedha za kigeni na maendeleo ya jamii.

Powered by

 : Mama Mzazi wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, Su...
26/05/2026

: Mama Mzazi wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, Suzana Magufuli, amefariki dunia, Chato mkoani Geita baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mtoto wa Hayati Magufuli, Jesca Magufuli amethibitisha kutokea kwa msiba huo akieleza kuwa Bibi Suzana amefariki Nyumbani kwake Chato na kwamba taratibu za msiba, familia itawajulisha.

Hii Yanga ikiamua jambo lake hakuna wakuwazuia, na ‘Star boy’ yupo kwaajili ya kuwapa wananchi  furaha 🔥FT’Young African...
25/05/2026

Hii Yanga ikiamua jambo lake hakuna wakuwazuia, na ‘Star boy’ yupo kwaajili ya kuwapa wananchi furaha 🔥

FT’
Young Africans 3️⃣-1️⃣ Namungo
⚽️Duke Abuya
Hassan Kabunda⚽️
⚽️⚽️Okello

Huyu OKELLO Msimfananishe na Wazee wenu kamwe🔥🙌🏽Allan Okello anafunga magoli mawili dhidi Yanga na kufikisha Goli 11.FT’...
25/05/2026

Huyu OKELLO Msimfananishe na Wazee wenu kamwe🔥🙌🏽

Allan Okello anafunga magoli mawili dhidi Yanga na kufikisha Goli 11.

FT’: Yanga SC 3-1 Namungo FC

  Ni mapumziko na tayari kila nyavu imeguswa; ‘No clean sheet’. HT: Yanga SC 1-1 Namungo FC
25/05/2026

Ni mapumziko na tayari kila nyavu imeguswa; ‘No clean sheet’.

HT: Yanga SC 1-1 Namungo FC

25/05/2026

: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, amerudishwa rumande leo Mei 25, 2026 baada ya shauri lake la maombi ya kuunganishwa katika kesi inayohusu mgawanyo wa mali za chama hicho, ambalo limeahirishwa mpaka Juni 2, 2026 kwa ajili ya usikilizwaji mbele ya Jaji David Ngunyale.

Akizungumza baada ya kuahirishwa kwa shauri hilo, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Dk Rugemeleza Nshala, amesema Mahak**a imeelekeza upande unaojibu maombi ya mwenyekiti kuwasilisha viapo vya kupinga maombi hayo ndani ya siku saba kuanzia leo kabla ya usikilizwaji wa kesi hiyo uliopangwa kufanyika Juni 2, 2026 saa 5:00 asubuhi.

Ameeleza kuwa hatima ya maombi ya Mwenyekiti wa Chadema itategemea uamuzi unaotarajiwa kutolewa Mei 28, 2026 katika kesi ya msingi iliyorejeshwa Mahak**a Kuu kutoka Mahak**a ya Rufani.

Kwa mujibu wa Dk Nshala, iwapo Mahak**a itaamua kesi hiyo inaendelea kuwa na nguvu kisheria, basi maombi ya mwenyekiti yataendelea kusikilizwa, lakini k**a kesi ya msingi itafutwa, hata maombi hayo yataathirika.

Powered by

🚨 MUDA WA HESABU, KILA MMOJA AANGALIE ALICHOKIPANDA!Simba na Yanga zatupwa nje ya 10 bora 😳🔥JE, UMERIDHIKA NA NAFASI YA ...
25/05/2026

🚨 MUDA WA HESABU, KILA MMOJA AANGALIE ALICHOKIPANDA!

Simba na Yanga zatupwa nje ya 10 bora 😳🔥

JE, UMERIDHIKA NA NAFASI YA CHAMA LAKO? 👀⚽

25/05/2026

JINI KATOKA MGANGA YUPO HOI | KAY MZIWAMDA AKUBALI MZIKI WA DODOMA JIJI.

Maoni ya shabiki wa Simba baada ushindi wa goli moja huku akimpongeza kocha wa Dodoma Jiji Amani Josiah
kutokana na mbinu zake.

25/05/2026

MWALIMU WA MASHUJAA MANENO MENGI VITENDO HAKUNA.

Maoni ya shabiki wa Simba baada ushindi wa goli moja huku akimpongeza kocha wa Dodoma Jiji Amani Josiah kutokana na mbinu zake.

Tittle Race 🏆
1. Simba Pts 58
2. Yanga Pts 57

Address

AICC
Arusha
23107

Website

https://www.instagram.com/nlfamedia?igsh=Nm9ydnk1dWx3Zmxt&utm_source=qr, https://www.instagram

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when NLFA MEDIA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share