
20/07/2025
Naibu Katibu Mkuu wa Makanisa ya Ufufuo na Uzima (GCTC), Askofu Maximilian Machumu Kadutu (Mwanamapinduzi), amesema akaunti zote za kifedha za kanisa hilo zimefungwa bila kufuatwa utaratibu, hatua ambayo imeathiri vibaya huduma za kiroho kwa mamilioni ya waumini nchini.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, siku ya Jumamosi tarehe 19 Julai 2025, Askofu Kadutu amesema akaunti hizo zimefungwa bila kuwahoji viongozi wa kanisa ambao ndio wateja wa benki, jambo linalokwenda kinyume cha haki za kisheria.
"Akaunti zote za kifedha za kanisa zimefungiwa (frozen) bila kufuata utaratibu wa kisheria wa kuulizwa kwa wateja wenyewe ambao ni wahusika wa kanisa hilo", ameeleza.
Aidha amesema mpaka sasa makanisa yote 2,112 ya GCTC yamefungwa nchini nzima, huku waumini zaidi ya milioni 6 wakinyimwa haki yao ya msingi ya kuabudu na miongoni mwao wakik**atwa wakiwemo wanawake, wazee na vijana.
"Waumini zaidi ya milioni 6 wamenyimwa haki ya kuabudu. Maaskofu, wachungaji, na wafanyakazi wa kanisa wamepoteza ajira, huduma na wito wa kazi ya Mungu", amesema Kadutu.
Askofu Kadutu amesema kuwa tangu kufungwa kwa makanisa hayo, tayari ni wiki ya saba waumini wa Ufufuo na Uzima hawajapata huduma za kiroho ipasavyo kwani kuna wakati walilazimika kukusanyika nje ya kanisa kwa ibada ambako huko nako hawakuabudu kwa amani kutokana na ulinzi mkali wa polisi.
"Baadaye, tarehe 4 Juni 2025, uongozi wa kanisa uliwasilisha shauri mahak**ani kuomba zuio dhidi ya barua hiyo, lakini mpaka leo mahak**a haijatoa uamuzi wowote, huku waumini wakiendelea kuteseka na kukosa ibada kila wiki, leo tunaingia wiki ya 7 bila waumini kupata huduma za kiroho, bila waumini kujua kustakabali wa jambo hilo, siyo kutoka kwa Waziri, siyo kutoka Mahak**ani", ameeleza.