LangMedia Tz

LangMedia Tz LANG MEDIA TZ:karibu uwe Wa Kwanza kila siku kuhabarika kwa Habari Mbalimbali za Michezo, Burudani, story na mambo mengine kem kem ya kufurahisha.

KWA MAHITAJI YA VIFARANGA BORA WA KUROILER KARIBU SUPER BRAND KEY STONE KUKU FARM BEI -@1800/=  PITA UTAJIPATIA VYUNGU V...
09/09/2019

KWA MAHITAJI YA VIFARANGA BORA WA KUROILER KARIBU SUPER BRAND KEY STONE KUKU FARM BEI -@1800/=
PITA UTAJIPATIA VYUNGU VYA JOTO-@12000/=INCUBATORS,NIPPLE@3000/= NA VIFAA VYAKUTENGENEZEA INCUBATORS
TUPO ARUSHA NA BIDHAA INAKUFIKIA POPOTE ULIPO TANZANIA NZIMA KWA USALAMA NA UAMINIFU MKUBWA 0715 064 992 -/- 0754 064 992

06/05/2017

Ajali mbaya ya gari imetokea kaskazini mwa Tanzania , ambapo basi aina ya Costa mali ya shule ya Lucky Vincent iliyoko eneo la kwa Mrombo ,l...

DOWNLOAD NEW SONG: NJOO UPONE BY GANSOO
23/02/2017

DOWNLOAD NEW SONG: NJOO UPONE BY GANSOO

DOWNLOAD NJOO UPONE_GANSOO

WADUDU NI CHAKULA BORANa Baraka KaayaSenene.Wadudu ni chanzo kikubwa cha protini, mafuta mazuri kiafya, madini na kamba ...
05/02/2017

WADUDU NI CHAKULA BORA

Na Baraka Kaaya
Senene.
Wadudu ni chanzo kikubwa cha protini, mafuta mazuri kiafya, madini na kamba lishe. Aidha, wadudu wameelezwa kuwa ni rafiki wa mazingira na ni rahisi kuwafuga au kuwak**ata.

Inakadiriwa kuwa kiasi cha watu bilioni 2 duniani wanatumia wadudu k**a sehemu ya milo yao ya kila siku. Imeshauriwa watu kupendelea kula wadudu kutokana na ukweli kwamba protini inayopatikana kwenye wadudu hao ni bora zaidi kuliko ile inayopatikana kwenye nyama ya kuku, ng’ombe, nguruwe na samaki.

Mbali ya wadudu kuwa ni chanzo kikuu cha protini na mafuta mazuri k**a ya samaki (fish oil), lakini pia ni chanzo kizuri cha madini ya kashiamu (calcium), chuma (iron), seleniamu (selenium), zinki (zinc) na Vitamini B

WADUDU WA TANZANIA

Bwa Alex Bulugu alisema Kuna aina zaidi ya elfu tisa ya wadudu wanaoliwa sehemu mbalimbali duniani. Lakini kwa nchini Tanzania, kuna aina kuu mbili za wadudu ambao wanajulikana na kutumiwa k**a sehemu ya kitoweo katika familia nyingi nchini, hasa vijijini.

Aina hizo mbili maarufu nchini Tanzania ni Senene na Kumbikumbi, ambao hupatikana kwa wingi zaidi nyakati za masika sehemu za vijijini. Senene na Kumbikumbi ni miongoni mwa vyakula vyenye faida nyingi mwilini na ni vitamu pia.

Kutokana na kuwa na faida nyingi za kiafya mwilini, ndiyo maana wamekuwa wakiliwa tangu enzi na enzi na mababu zetu. Ingawa idadi kubwa ya wadudu hao wanaoliwa hupatikana kwa kuwak**ata kwenye makazi yao porini, lakini katika siku za hivi karibuni, mifumo ya kisasa ya kuwak**ata wadudu hao imebuniwa na hivyo kurahisisha ukusanyaji kwa idadi kubwa na kwa mara moja.

Kwa kuona umuhimu na faida za kiafya zinazoweza kupatikana kwa kula wadudu, Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa nchi zote duniani kufuga wadudu hao kwa wingi kibiashara, shirika linaamini nchi nyingi zikitilia mkazo suala hili, zinaweza kupunguza tatizo la njaa kwa kiasi kikubwa na wakati huo huo kuboresha afya za watu wengi.

Bila shaka hii ni habari njema na ya kutia moyo kwa watu ambao tayari wanafuga na kuvuna Senene kibiashara, k**a ambavyo tunavyoona wakiuzwa baadhi ya sehemu za mijini. Nitoe wito kwa watu wengine ambao hawajawahi kuonja Senene au Kumbikumbi kufanya hivyo, kwani siyo tu wana faida kiafya mwilini, bali ni watamu sana. (so delicious)!-GPL

Fahamu kuhusu Ng'e na Hatari zake.Na Baraka kaayaNg'e ni mdudu mweusi au kahawia mwenyemiguu minane na mkia mrefu wenyes...
04/02/2017

Fahamu kuhusu Ng'e na Hatari zake.

Na Baraka kaaya
Ng'e ni mdudu mweusi au kahawia mwenye
miguu minane na mkia mrefu wenye
sumu kali

Tafsiri ya majina haya kibaolojia
Kiingereza: scorpion
Kipoland: skorpion

Huduma ya kwanza kwa aliyeng'atwa na ng’e

Bw Elias Manase mtaluma Wa sayansi ya viumbe hai amesema nnge Ingawa wanaweza kusababisha maumivu makali, matukio mengi ya kuumwa na ng’e hayasababishi madhara makubwa au madhara ya muda mrefu.
Usiitikise sehemu iliyoumia na tumia barafu au maji baridi kupunguza maumivu.Usikate au kuchana wazi sehemu ya jeraha au kufunga sehemu hiyo kwa kutumia toniketi au bandeji. Joto halisaidii, lakini kutoitikisa sehemu ya jeraha husaidia. K**a unajua kuwa aina ya buibui au ng’e aliyemuuma ni hatari, au k**a baada ya kuuma kuna dalili za matatizo k**a vile maumivu ya tumbo, mwasho, kutokwa jasho, na shida katika kupumua, basi tafuta msaada wa kitabibu. Huenda kukawa na dawa dhidi ya sumu hiyo.
Kwa ajili ya matukio ya kunga’twa na ng’e hatari, unaweza kumpa majeruhi diazipamu kuzuia misuli kukak**aa na pia kumtuliza mgonjwa wakati mnafanya maandalizi ya kwenda hospitali au kituo cha afya.

Buibui na ng’e
Ingawa wanaweza kusababisha maumivu makali, matukio mengi ya kuumwa na buibui na ng’e hayasababishi madhara makubwa au madhara ya muda mrefu. Usiitikise sehemu iliyoumia na tumia barafu au maji baridi kupunguza maumivu.Usikate au kuchana wazi sehemu ya jeraha au kufunga sehemu hiyo kwa kutumia toniketi au bandeji. Joto halisaidii, lakini kutoitikisa sehemu ya jeraha husaidia. K**a unajua kuwa aina ya buibui au ng’e aliyemuuma ni hatari, au k**a baada ya kuuma kuna dalili za matatizo k**a vile maumivu ya tumbo, mwasho, kutokwa jasho, na shida katika kupumua, basi tafuta msaada wa kitabibu. Huenda kukawa na dawa dhidi ya sumu hiyo.
Kwa ajili ya matukio ya kunga’twa na buibui na ng’e hatari, unaweza kumpa majeruhi diazipamu kuzuia misuli kukak**aa na pia kumtuliza mgonjwa wakati mnafanya maandalizi ya kwenda hospitali au kituo cha afya.

FAHAMU KUHUSU MAISHA YA MDUDU MENDE NA FAIDA ZAKENa Baraka Kaaya 1.Ni mdudu anayeweza kuishi zaidi ya mwezi bila ya kula...
02/02/2017

FAHAMU KUHUSU MAISHA YA MDUDU MENDE NA FAIDA ZAKE

Na Baraka Kaaya
1.Ni mdudu anayeweza kuishi zaidi ya mwezi bila ya kula chakula chochote.
2.Ni mdudu anayeweza kuishi wiki mbili bila ya kunywa maji.
3.Wakati moyo wa mwanadamu nu mmoja wenye chemba nne mende ana moyo mmoja wenye chemba kumi na tatu.
4.Baadhi ya mende wa k**e hawaitaji wanaume kuweza kuzalisha mayai hupandana wao kwa wao na kutaga mayai katika kipindi chote cha maisha yao.
5.Mende ana uwezo wa kukaa kwa zaidi ya dakika 40 bila ya kupumua.
6.Mende ana uwezo wa kuishi zaidi ya wiki mbili akiwa amekatwa kichwa.
7.Ana uwezo wa zaidi ya mara 15 ya binadamu wa kuzuia miale mikali ya nuklia isimdhuru na kubaki hai
8.Mende ni mdudu asiye na mapafu.
9.Ana uwezo wa kuruka maili 3 kwa saa.

FAIDA ZA MDUDU MENDE KIAFYA NA KIJAMII
Mende wana manufaa mengi sana kwa binadamu
Mende huchukiwa sana na watu na huhusishwa na uchafu na maradhi. Lakini wajua kwamba wadudu hawa wana manufaa makubwa sana kwa binadamu?
Mjini Havana, nchini Cuba kuna aina ya mende ambao hufugwa k**a wanyama vipenzi na hata visa vyao husimuliwa kwenye hadithi, anasimulia Mary Colwell.
Kwenye kisa kimoja, mende kwa jina Martina huwafanyisha mtihani wanaotaka kumchumbia kwa kuwaudhi kila wanapomtembelea.

"Mwaga kahawa kwenye viatu vyao uone watalichukulia vipi hilo,” anapendekeza nyanyake Martina. "Ni muhimu sana kujua mumeo mtarajiwa hufanya nini anapokasirika – mtihani wa kahawa hufanikiwa.”
Kuna aina 4,500 ya mende, na ni aina nne pekee ambao huwa waharibifu.
Wengi hawaishi karibu na nyumba za watu na hutekeleza jukumu muhimu katika ikolojia kwa kula vitu vilivyokufa na vinavyooza.

Baadhi ya mende huishi pamoja na kusaidiana
Baadhi wana sifa nzuri na huishi pamoja na kusaidiana katika kutafuta chakula na makazi. Wana uwezo wa kuishi katika mazingira magumu. Aina moja kwa jina Eublaberus posticus wanaweza kuishi mwaka mmoja kwa kunywa maji pekee.
Wale wazito zaidi, huwa na uzani wa gramu 35, na urefu wa sentimeta 8 na huishi Australia. Wale wadogo zaidi huishi Ulaya na Amerika Kaskazini na wana urefu wa sentimeta moja pekee.
Badala ya kuwachukia, wanasayansi huwafurahia sana na kuwatumia kwa manufaa ya binadamu. Mwaka 1999, mende walitumiwa na Prof Robert Full katika Chuo Kikuu cha California, Berkley, kumpa wazo la kuunda roboti ya miguu sita iliyosonga upesi na kwa urahisi.
Mende huwa thabiti sana, na wakianguka huwa wanainuka upesi na kwa urahisi kwa kutumia mabawa.

Miguu ya mende pia imekuwa ikitumiwa na wavumbuzi wanaotengeneza miguu bandia ya kutumiwa na binadamu.
Kuna pia mende ambao wamekuwa wakiunganishwa na kompyuta ndogo inayowekwa mgongoni na kuongozwa kufika maeneo ambayo mwanadamu hawezi kufika.
"Nilipoona hili mara ya kwanza, nilishangaa sana,” mtafiti mkuu katika mradi huo unaoendeshwa katika Chuo Kikuu cha A&M cha Texas, Hong Liang anasema.

Mende wanatumiwa pia katika matibabu. Wanasayansi kwa miaka mingi wamekuwa wakishangazwa na uwezo wa mende kukaa muda mrefu maeneo yenye sumu na uchafu bila kudhurika. Wamegundua kwamba huwa wanatoa kemikali za kupigana na sumu.
Wanaweza kusaidia katika kutengeneza dawa za kusaidia binadamu kukabiliana na bakteria zinazohangaisha sana watu kwa mfano E. Coli na MRSA ambazo zimekuwa hazisikii dawa.

Hii si mara ya kwanza mende ktumiwa kwa sababu za kimatibabu. Mwanahabari Lafcadio Hearn karne ya 19 alipitia maeneo ya kusini mwa Marekani na kuripoti jinsi watu wenye pepopunda walikuwa wakipewa chai iliyotengenezwa kwa kutumia mende.
“Sijui ni mende wangapi hutumiwa hadi upate kikombe cha chai, lakini wakazi wa New Orleans wana Imani sana na tiba hii,” aliandika.
hospitali moja ya Uchina, krimu inayotengenezwa kwa kutumia ungaunga wa mende waliosiagwa hutumiwa kitibu vidonda vya moto na pia humezwa kutibu vidonda vya tumbo.

Mende wanahitaji sana hivi kwamba Wang Fuming aliamua kuanza biashara ya ufugaji mende eneo la Shandong, mashariki mwa Uchina. Huwa anafuga mende 22 milioni kwa wakati mmoja. Anasema tangu 2010, bei ya mende waliokaushwa imepanda mara kumi.
Mende hupikwa na kuliwa nchini

FAHAMU ZAIDI KUHUSU NYIGUNa Baraka Kaaya.Karibu katika mwendelezo wa makala zetu za wadudu na Leo hii utafahamu zaidi ku...
01/02/2017

FAHAMU ZAIDI KUHUSU NYIGU

Na Baraka Kaaya.
Karibu katika mwendelezo wa makala zetu za wadudu na Leo hii utafahamu zaidi kuhusu nyigu.
Nyigu ni wadudu wa jamii nusuoda Apocrita katika katika kundi la Hymenoptera ambao sio nyuki au
sisimizi. Wadudu hawa wote ni mbuai au vidusia lakini ni lava tu ambao hula mawindo kwa aina tofauti. Wadudu wapevu hula mbochi, mbelewele au vitu vyingine vyenye sukari. Nyigu mbuai huk**ata wadudu (viwavi mara nyingi) au wadudu wengine.

Huwaweka katika tundu ardhini au katika tundu lililoundwa kwa matope au kwa aina ya “ karatasi ” baada ya kuwapooza kwa sumu katika ganglioni kuu. Halafu nyigu hulitaga yai juu ya mdudu aliyek**atwa. Huyu aendelea kuwa hai na kwa hivyo lava wa nyigu akitoka kwenye yai anapata chakula kisichooza. Hata mdudu bila bahati afa tu akiwa ameliwa takriban kabisa. Jambo la nyigu vidusia linafanana lakini nyigu hawa huacha mwathirika ambapo alimpata. Hutaga yai au mayai juu au ndani yake na lava wakitoka kwenye mayai wanaanza kula mwathirika. Kwa sababu ya mwenendo huu nyigu vidusia hutumika sana kwa kufanya udhibiti wa kibiolojia dhidi ya visumbufu.

Kinyume na nyigu wengine spishi za
familia Chalcidae (Pic-kidutu ) husababisha vidutu kwa majani ya
mimea na lava hula tishu yao. Spishi jamaa za familia Agaonidae (nyigu-makuyu) huyataga mayai yao katika
ovari za maua ya mikuyu.
Kuna majina mbalimbali kwa makundi ya nyigu, k**a vile: bunzi , dondora ,
mavu, nyigu-kidutu , nyigu-makuyu na
uvi .

Nyigu Kimelea Mwenye Manufaa
NYIGU aina ya ichneumon ana sura ya ajabu na yenye kutisha. Lakini kwa nini anaonwa kuwa kimelea? Kwa sababu kwa kawaida hutaga mayai yake juu au ndani ya buu la mdudu mwingine au buibui.
Kuna zaidi ya aina 3,000 za nyigu wa
ichneumon huko Amerika Kaskazini. Nyigu hao ni sehemu ya jamii kubwa ya nyigu mbalimbali ambao ni vimelea. Wanasayansi wanakadiria kwamba kuna zaidi ya aina 40,000 za wadudu hao ulimwenguni pote.

Nyigu hao wana ukubwa mbalimbali, kuanzia sentimeta 0.3 hadi sentimeta 5 hivi. Tumbo lao jembamba lililojipinda ni refu kuliko kichwa na kifua pamoja. Nyigu hao wana vipapasio virefu tofauti na nyigu wengine.

Kitu kinachomtofautisha zaidi na nyigu wengine ni mrija unaofanana na sindano ulio kwenye ncha ya tumbo lake. Yeye hutaga mayai kwa mrija huo ambao kwa kawaida huwa mrefu kuliko mwili wake. Mrija huo ni mwembamba k**a singa ya farasi na una nyuzi tatu zinazosongasonga ambazo husukuma yai kutoka kwenye mrija.

Nyigu hao hutambuaje buu ambapo watatagia mayai? Nyigu wa k**e aina ya
Megarhyssa, wa jamii ya ichneumon,
ameonekana akigongagonga mti kwa kipapasio chake ili kutambua kelele za buu lililo sentimeta mbili au zaidi chini ya gamba la mti. Anapotambua buu, yeye hugongagonga zaidi. Kisha, yeye huanza kutoboa gamba hilo kwa mrija wake.
Watu ambao wamemchunguza wanasema hivi: “Nyigu anapogusa buu kwa ncha ya mrija, yai moja husukumwa nje ya mrija na kutagwa juu ya buu au karibu nalo.” Yai linapoanguliwa, buu jipya hula mafuta na majimaji ya buu la awali. Kisha buu jipya hufanyiza kifuko cha hariri ambapo linakulia na kuwa nyigu aliyekomaa. Nyigu anapotoka nje ya mti, huwa tayari kuvamia wadudu wengine.
Ingawa inaweza kusemwa kwamba nyigu hao ni vimelea hatari, wana kazi muhimu. Mabuu yao hula wadudu ambao huharibu mimea, k**a vile aina fulani ya kunguni, mdudu alaye pamba, aina fulani ya nondo, mbawakawa, na kadhalika. Kwa hiyo, yaelekea nyigu hao huzuia ongezeko la wadudu wanaoharibu mazao.

Hata ingawa nyigu hao ni wengi sana, si rahisi kuwaona kwa sababu wao hula, huzaana, na kutaga mayai mbali na wanadamu. Hao ni baadhi tu ya viumbe wengi ambao wanadamu hawajawaelewa

Fahamu zaidi Maisha ya Chura Na Baraka KaayaBaada ya kufamu zaidi Maisha ya chura wa kihansi kwenye post ya Nyuma karibu...
31/01/2017

Fahamu zaidi Maisha ya Chura

Na Baraka Kaaya
Baada ya kufamu zaidi Maisha ya chura wa kihansi kwenye post ya Nyuma karibu tena upate kufahamu zaidi kuhusu aina zingine za vyura na Maisha lakini pia hadisi ya kukujenga kuhusu mdudu huyu.

Maisha ya chura huaanza k**a yai
lililotegwa kwenye maji pamoja na mayai maelfu. Hutoka kwa umbo la
ndubwi (pia: kiluwiluwi) ambayo ni
funzo la chura huendelea na kipindi cha kwanza cha maisha yake katika maji. Hupumua kwa yavuyavu na mwanzoni huku akiwa hana miguu bali mapezi k**a samaki na mkia . Viluwiluwi wengi wakiwa kwenye maji wanakula majani au mwani hata k**a baadaye k**a chura mzima wanakula wadudu wengine.

Baada ya muda kiluwiluwi hulaga miguu minne na mapafu . Utumbo unabadilika na kujiandaa kwa chakula kipya kinachopatikana kwenye nchi kavu. Umbo hufanana na chura mzima.
Kipindi hiki cha utoto kwenye maji hudumu kati ya wiki tatu hadi miaka miwili kutegemeana na spishi za chura. Mara nyingi ni k**a wiki 10 - 15.

Chura mzima kwenye nchi kavu
Akitoka kwenye maji chakula chake ni wadudu. Lakini chura wakubwa wameonekana pia kula
mamalia wadogo, samaki na chura wadogo zaidi. Spishi kadhaa wana ulimu wa kunata wanashika wadudu wanaopita haraka lakini wengine wanak**ata windo kwa kutumia mikono yao.

Bali na maelezo haya kuna pia spishi kadhaa wanaorudi kuishi katika maji lakini wanapumua kwa mapavu na wachache sana wanaendelea kula majani. Spishi kadhaa wanaendelea kuishi kwenye miti.
Chura wenyewe wanaliwa na ndege , samaki, nyoka na mamalia. Katika nchi kadhaa watu wanakula chura, kwa mfano Ufaransa, China na Ufilipino.
Kuna takriban spishi 5,600 za chura.

Familia za Afrika
Archaeobatrachia
Alytidae, Vyura ulimi-sahani
Mesobatrachia
Pelobatidae, Vyura miguu-sepeto
Pipidae, Vyura-kucha
Neobatrachia
Arthroleptidae, Vyura-filimbi
Brevicipitidae, Vyura kichwa-kifupi
Bufonidae, Vyura sugu
Dicroglossidae, Vyura ulimi-panda
Heleophrynidae, Vyura pepo
Hemisotidae, Vyura pua-sepeto
Hylidae, Vyura-miti
Hyperoliidae, Vyura-mafunjo
Mantellidae, Vyura bukini
Microhylidae, Vyura domo-jembamba
Petropedetidae, Vyura-vijito
Phrynobatrachidae, Vyura-madimbwi
Ptychadenidae, Vyura vigongo
Pyxicephalidae, Vyura dubwana na
vyura maridadi
Ranidae, Vyura sahihi
Rhacophoridae, Vyura-povu
Sooglossidae, Vyura wa Shelisheli

Pia K**a ilivyo kwa wadudu wengine tunajifunza mengi na kuyakinganiasha na maisha ya binadamu na hii hadithi maarufu ya CHURA.

Mwanasayansi toka ujerumani
Heinzmann , aligundua kuwa chura akiwekwa kwenye chombo tuseme sufuria yenye maji baridi , halafu maji hayo yakaanza kupashwa moto kidogo kidogo , basi chura huyo wala hatohangaika kutoka kwenye maji, na hatimaye kufa wakati maji hayo yatakapokuwa ya moto kweli kweli. Ingawaje kuna mabishano ya kisayansi kuhusu usahihi wa madai ya Heinzmann, leo utajifunza kitu kuhusu habari hii ya chura.

Kumbuka ukimweka chura kwenye maji ambayo tayari ni ya moto , atakurupuka haraka. Utafiti nilioleza hapo juu ni k**a utamweka kwa maji ya baridi.
Mara nyingi ili binadamu akubaliane kwa urahisi na mabadiliko, basi mabadiliko hayo ni lazima yafanyike kidogo kidogo k**a hiyo habari ya chura.

Jamii yetu inaporomoka kimaadili siku hadi siku, kiwango cha elimu kinashuka na hata ufanisi makazini ni ishu. Hata hivyo matatizo hayo ya mfumo wetu wa maisha hayajaanza leo, hayakuwa makubwa kiasi hiki kipindi kirefu kilichopita, ila yameendelea kukua kidogo kidogo k**a vile yale maji yanavyoongezwa joto ili kumuunguza chura. Hatukusikii wala hatuoni ni shida, tumebaki kulaumiana ila mbaya zaidi k**a vile yule chura, bado hatuchui hatua ya kujikwamua kwa haraka kwa kuwa ni k**a tumekwishajizoelea hali hii.

Bado unayo nafasi ya kuamka, na kubadili kile kinachokukera. Usikatishwe tamaa na mfumo mzima wa maisha ya jamii, mabadiliko ya kweli ya jamii hayategemei wote sisi kubadilika kwa wakati mmoja. Kila mmoja wetu akibadilika kidogo kidogo jamii itafika mbali.

WAJUE VYURA WA KIHANSINa Baraka KaayaKaribu tena mwendelezo wa makala mbalimbali zinazohusu wadudu wa sampuli kadhakadha...
30/01/2017

WAJUE VYURA WA KIHANSI

Na Baraka Kaaya
Karibu tena mwendelezo wa makala mbalimbali zinazohusu wadudu wa sampuli kadhakadha ambapo leo utafahamu zaidi kuhusu Chura wa Kihansi ambao kitaalamu hufahamika k**a ‘Nectophrynoides asperginis’

Chura wa Kihansi k**a zilivyo raslimali nyingine ni maliasili muhimu ya watanzania.Chura wa kihansi aligundulika mwaka 1996 katika mapromoko ya maji yaitwayo Mhalala yaliyoko ndani ya Milima ya Udzungwa katika Wilaya ya Kilombero,Mkoa Morogoro.Chura huyu anaishi kwenye mazingira ya maji yanayotiririka na kutoa mvuke mwingi sana kutokana na nguvu ya maji.Chura huyu ambae kitalaamu anaitwa Nectophrynoides asperginis hapatikani sehemu nyingine yeyote duniani isipokuwa katika bonde la Kihansi nchini Tanzania tu.

Chura wa kihansi ni chura pekee katika jamii ya vyura waliopo duniani kwa sababu vyura hawa hutaga mayai na kukaa nayo kwenye kifuko kilichopo ndani ya chura mwenyewe hadi muda wa kuanguliwa unapofika na ndipo hutoa vitoto hai.Kwa lugha rahisi ni kwamba Chura hawa huzaa kwa sababu hatagi mayai yakaonekana bali hukaa ndani ya Chura mwenyewe.

Chura huyu anatofautiana na vyura wengine kwa sababu vyura wa jamii nyingine hutaga mayai na kuyaacha majini ambako huanguliwa wakati mama yao hayo,wakati Chura wa kihansi huangulia tumboni na kuwazaa watoto wakiwa hai,tabia hii ya kuzaa ndio inayomfanya chura huyu kuwa wa kipekee duniani
Chura huyu amewekwa kwenye kundi la viumbe wanaolindwa kutokana na kutoweka kwake na kuwekwa kwenye kifungu cha kwanza cha Mkataba wa Biashara ya Wanyamapori na Mimea iliyo hatarinikutoweka.Mkataba huu kwa Kiingereza unaitwa "Convention on International Trade in Endangered Species" (CITES) na kisheria chura huyu hawezi kufanyiwa biashara ya aina yeyote hapa duniani.

Maporomoko ya korongo la Mto Kihansi ambayo ndiyo makazi ya asili ya Chura hawa yana ukubwa wa eneo la urefu wa Kilometa nne na upana wa nusu Kilometa.Bonde la Mto Kihansi linapatikana katika mto Kihansi unaoanzia katika Wilaya za Mufindi na Kilolo Mkoa wa Iringa na kupeleka maji yake katika Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro.
Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi zake zimekuwa zikiandaa mradi wa utunzaji wa mazingira katika bonde la Mto Kihansi "LKEMP" Mradi huu unasimamiwa na Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira "NEMC "

Katika kurudisha mazingira asilia ya vyura hawa,mradi wa "LKEMP"wameweka mabomba yanayotoa maji yenye uvuke unaofanana na ule wa asilia kwa ajili ya kurudisha uoto uliokuwapo.Kazi hii imekua ikifanyika kwa kushirikiana na idara ya Wanyamapori kupitia taasisi yake ya utafiti wa wanyamapori "TAWIRI" Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira " NEMC" ,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Sokoine.

Fahamu zaidi kuhusu kunguni.Na Baraka KaayaLicha ya kuhusishwa na uchafu, na mazingira duni, kunguni ameibuka kuwa mdudu...
29/01/2017

Fahamu zaidi kuhusu kunguni.

Na Baraka Kaaya
Licha ya kuhusishwa na uchafu, na mazingira duni, kunguni ameibuka kuwa mdudu mwenye uwezo mkubwa wa kustahimili hatari dhidi ya maisha yake.
Utafiti mpya umebaini kuwa wadudu hao wanaweza kustahimili sio tu tanuri ya moto na baridi kali bali pia madawa ya kisasa ya kuua wadudu wanaotambaa.
Kunguni wamegundulika kuwa wanaweza kustahimili kupuliziwa dawa nyingi ya sumu kwa kuimarisha uwezo wake wa kujikinga dhidi ya sumu moja baada ya nyengine.

Wadudu hao ambao huishi kwa kufyonza damu ya wenyeji wake wakiwa usingizini wanauwezo mkubwa wa kibayolojia ya kujikinga dhidi ya sumu kali.Hii ni kusema kuwa kadri vizazi vya kunguni vinavyopuliziwa madawa yenye sumu ndivyo wadudu hao wanavyoimarisha uwezo wake wakuzuia maafa miongoni mwa watoto wao.

Aidha, watafiti wanaema kuwa vipimo 1000 vya sumu kali aina ya (neo-nicotinoid) vinahitajika kuua kunguni mmoja huko Marekani katika majimbo ya Cincinnati na Michigan ikilinganishwa na maeneo mengine duniani.
Watafiti hao sasa wanasema kuwa kuna hatari kubwa ya mdudu huyo kuenea kote duniani kutokana na utandawazi na soko huria ambao umefanya ulimwengu kuwa kitongoji kikubwa tu.
Aidha wanasayansi hao wanashauri kutafutwa mbinu tofauti na mpya ya kukabiliana na kunguni pasi na kutumia sumu, k**a vile kutafuta wadudu wengine wanaoweza kuwala ilikuzuia wadudu hao kuenea kote duniani.Taarifa hiyo ilichapishwa katika jarida la utabibu la The Journal of Medical of Entomology.

“Usiwaache Kunguni Wakuume!”
KUFIKIA katikati ya karne ya 20, ilionekana kwamba wanadamu wamefaulu kuwadhibiti kunguni. Watu fulani walifahamu kunguni kupitia tu wimbo wa zamani wa Kiingereza ulioimbwa na watoto wa shule za nasari (au chekechea) uliosema: “Usiwaache kunguni wakuume.” Hata hivyo, katika miaka ya 1970, nchi nyingi ziliamua kupiga marufuku matumizi ya dawa ya DDT—iliyokuwa dawa kuu ya kuua kunguni—kwa kuwa ilikuwa yenye sumu na iliharibu mazingira.

Hata hivyo, kemikali nyingine zilipotumiwa ilionekana kwamba kunguni walikuwa sugu na hazikuwaua. Pia watu walianza kusafiri mara nyingi zaidi na bila kujua walihama pamoja nao. Matokeo yakawaje? Ripoti moja ya mwaka wa 2012 kuhusu kuwadhibiti wadudu hao inasema: “Katika miaka 12 ambayo imepita kunguni wameanza kuonekana tena nchini Marekani, Kanada, Mashariki ya Kati, nchi kadhaa za Ulaya, Australia, na katika sehemu fulani za Afrika.”
Huko Moscow, Urusi, katika mwaka mmoja hivi karibuni, ripoti za kutokea kwa kunguni ziliongezeka mara kumi kuliko ilivyokuwa hapo awali. Wakati huohuo, upande ule mwingine wa ulimwengu, huko Australia, kumekuwa na ongezeko la asilimia 5,000 la kunguni tangu mwaka wa 1999!
Watu fulani hubeba kunguni bila kujua wanapoenda dukani, kwenye kumbi za sinema, au hotelini. “Upende usipende utabeba kunguni,” anasema meneja fulani wa hoteli nchini Marekani. “Maadamu hoteli inapata wateja lazima kunguni wataendelea kuwapo.” Kwa nini ni vigumu kiasi hicho kuwamaliza kunguni? Unaweza kujilindaje? Kunguni wanapovamia nyumba yako, unaweza kuchukua hatua gani zinazofaa ili kuwaondoa na kuwazuia wasirudi tena?
Wadudu Wasiokufa kwa Urahisi
Kwa kuwa wadudu hao ni wadogo k**a mbegu ya tofaa na wana mwili bapa, kunguni wanaweza kujificha mahali popote pale. Wanaweza kujificha katika godoro lako, fanicha zako, sehemu ya ukutani ya kuunganishia vitu vya umeme, au hata kwenye simu yako. Kwa kawaida kunguni hupenda kujificha mita tatu hadi sita kutoka kwenye vitanda na maeneo ya kuketi. Kwa nini? Ili wawe karibu na chakula chao, yaani, wewe!
Mara nyingi, kunguni huwauma watu wanapolala. Hata hivyo, watu wengi hawahisi wanapoumwa kwa sababu mdudu huyo humdunga mtu kitu kinachogandisha kinachomwezesha kuendelea kula kwa dakika kumi hivi bila kukatizwa. Na ingawa kunguni wanaweza kula kila juma, imesemekana kwamba wanaweza kuendelea kuishi bila kula kwa miezi mingi.

Tofauti na mbu na wadudu wengine, inaonekana kwamba kunguni hawaenezi magonjwa ya kuambukiza. Hata hivyo, wanapomuuma mtu wanatokeza mwasho na baadaye sehemu hiyo inavimba, na watu wengi huathiriwa kihisia. Watu walioumwa na kunguni wanaweza kupoteza usingizi, kuaibika, na hata kufikiri kwamba kunguni amewauma muda mrefu baada ya wadudu hao kutoweka. Jarida moja nchini Sierra Leone linasema kuwa kunguni “ni wasumbufu sana na wanawakosesha watu usingizi” na linaonya kuhusu “aibu inayohusianishwa na kunguni.”

Kuwadhibiti Kunguni
Kunguni wanaweza kumsumbua mtu yeyote. Ni rahisi kuwadhibiti ukitambua mapema kwamba wapo. Kwa hiyo, jifunze kutambua ishara za kwamba wapo nyumbani na unaposafiri. Chunguza fanicha zako na vitu vingine vya mbao pamoja na mizigo, uone ikiwa kuna mayai madogo yanayofanana na mbegu ndogo nyeusi au alama za damu. Tumia tochi unapowatafuta kunguni ili uweze kuwaona.

Usiruhusu kunguni wawe na sehemu nyingi za kujificha. Ziba nyufa zote ukutani na kwenye viunzi vya milango. Ingawa kunguni hawaletwi na uchafu, itakuwa rahisi zaidi kuwatambua na kuwadhibiti ikiwa unasafisha nyumba kwa ukawaida na kupunguza vitu vilivyorundamana. Ukiwa hotelini, unaweza kupunguza uwezekano wa kubeba kunguni kwa kuepuka kuweka masanduku yako sakafuni na kitandani.

Kunguni Wanapovamia Nyumba Yako
Ukipata kunguni nyumbani au hotelini, huenda ukawa na wasiwasi au hata ukaaibika. Dave na mke wake waliumwa na kunguni walipokuwa likizoni. Dave anasema: “Tuliaibika sana. Tulijiuliza tutawaambia nini watu wa familia na marafiki tutakapofika nyumbani? Je, wakati wowote wanapojikuna au kupatwa na mwasho wa ngozi wangejiambia ni kwa sababu walitutembelea?” Hata ingawa ni kawaida kuwa na maoni k**a hayo, usiache aibu ikuzuie kutafuta msaada. Wizara ya Afya ya Mwili na Akili ya New York City inatoa uhakikisho huu: “Ni vigumu, lakini inawezekana kuwaangamiza kunguni.”
Chunguza uone k**a kuna kunguni kisha uchukue hatua za kuwazuia wasijifiche nyumbani kwako
Hata hivyo, usifikiri kwamba ni rahisi kuwamaliza kunguni. Kunguni wakivamia nyumba yako, unaweza kupata msaada kutoka kwa mtaalamu wa kuwadhibiti wadudu wasumbufu. Ingawa kemikali zilizotajwa awali hazitumiwi tena, wataalamu hao hutumia mbinu kadhaa zinazofaa ili kuwaangamiza kunguni. Dini M. Miller, mtaalamu wa wadudu anasema hivi pia: “Kuwadhibiti kunguni kunahitaji ushirikiano mkubwa sana kati ya wakaaji wa nyumba, wamiliki wa nyumba yenyewe, na kampuni ya kuwadhibiti wadudu wasumbufu.” Kwa kufuata mwelekezo wa mtaalamu na kuchukua tahadhari zinazohitajika, unaweza kutimiza sehemu yako na ‘kutowaacha kunguni wakuume’!
Wataalamu wa wadudu wanasema kwamba kunguni hula damu ya wanadamu na wanyama wengine kutia ndani wanyama-vipenzi.
Toa Maoni yako..

Address

Arusha

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when LangMedia Tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share