SMILE FM TZ

SMILE FM TZ Radio � Broadcasts, Advertisements production,Events plan

TUILINDE AMANI YETU
09/12/2025

TUILINDE AMANI YETU

Kwa huzuni kubwa tunatangaza kifo cha Raila Odinga, kiongozi mkuu wa upinzani wa Kenya,na waziri mkuu mstaafu amefariki ...
15/10/2025

Kwa huzuni kubwa tunatangaza kifo cha Raila Odinga, kiongozi mkuu wa upinzani wa Kenya,na waziri mkuu mstaafu amefariki akiwa na umri wa 80 nchini India. Baba wetu wa kisiasa atakumbukwa daima.

KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE 🇹🇿Baba wa Taifa, Mwanga wa Fikra na Uzalendo.14 Oktoba | Nyerere Day“Uongozi ni Wito, sio F...
14/10/2025

KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE 🇹🇿
Baba wa Taifa, Mwanga wa Fikra na Uzalendo.
14 Oktoba | Nyerere Day
“Uongozi ni Wito, sio Fursa.” — Mwalimu J.K. Nyerere

KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE 🇹🇿Baba wa Taifa, Mwanga wa Fikra na Uzalendo.14 Oktoba | Nyerere DayUongozi ni Wito, sio Fu...
14/10/2025

KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE 🇹🇿
Baba wa Taifa, Mwanga wa Fikra na Uzalendo.
14 Oktoba | Nyerere Day
Uongozi ni Wito, sio Fursa.— Mwalimu J.K. Nyerere

⚽🔥 Jana ilikuwa   … wiki hii tunasubiri  !👉 Swali ni moja tu: nani ata funika zaidi mwaka huu? 🤔Tuambie maoni yako hapa ...
11/09/2025

⚽🔥 Jana ilikuwa … wiki hii tunasubiri !
👉 Swali ni moja tu: nani ata funika zaidi mwaka huu? 🤔

Tuambie maoni yako hapa 👇

Taasisi isiyo ya serikali ya Mati foundation,imekabidhi pikipiki zinazotumia nishati ya umeme kwa watu wenye ulemavu mko...
09/09/2025

Taasisi isiyo ya serikali ya Mati foundation,imekabidhi pikipiki zinazotumia nishati ya umeme kwa watu wenye ulemavu mkoa wa Manyara ili kuwasaidia kufanya shughuli zao kwa ufanisi.

Hafla ya makabidhiano imeongozwa na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mati super brand ltd,inayozalisha na kusambaza vinywaji changamshi,David Mulokozi ambaye amekiri watu wenye mahitaji maalumu katika jamii wanahitaji kujenga uchumi na kustawi.

“ Mati super brand tumekabidhi pikipiki kwa mati foundation kwa ajili ya ndugu zetu wenye ulemavu hasa ziwasaidie katika shughuli zao”..Mulokozi.

MATI TECHNOLOGIES LTD YALETA MAPINDUZI TEKNOLOJIA YA NDEGE NYUKI DRONE.Kampuni ya Mati Super Brands Ltd kupitia kampuni ...
03/09/2025

MATI TECHNOLOGIES LTD YALETA MAPINDUZI TEKNOLOJIA YA NDEGE NYUKI DRONE.

Kampuni ya Mati Super Brands Ltd kupitia kampuni tanzu Mati Technologies imekuja na teknolojia ya kisasa ya Ndege nyuki (drone) kwa ajili ya sekta ya kilimo na huduma nyingine za kijamii ili kuongeza ufanisi.

Hatua hii inalenga kuongeza tija, kupunguza gharama na kurahisisha kazi kwa wakulima na taasisi mbalimbali nchini.

Akizungumzia hatua hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Mati Group of Companies, Bw. David Mulokozi, amesema kampuni hiyo imeamua kuwekeza kwenye teknolojia ya drone zitakazotumika kunyunyizia dawa mashambani, kupima maeneo, kupanda mbegu, kusafirisha mizigo, kusaidia kaguzi mbalimbali nk.

Mulokozi ameeleza kuwa drone hizo zinazotengenezwa ndani ya nchi zitauzwa kuanzia shilingi milioni 17 kulingana na mahitaji ya mteja, hali itakayowawezesha wakulima wengi kuzimudu kulinganisha na Gharama kubwa za uagizaji bidhaa hizo nje ya nchi.

Mkuu wa wilaya ya Babati,Emmanuela Kaganda amesema mwenge wa uhuru utazindua jengo la kisasa la utawala lilipopo Bagara ...
14/07/2025

Mkuu wa wilaya ya Babati,Emmanuela Kaganda amesema mwenge wa uhuru utazindua jengo la kisasa la utawala lilipopo Bagara ziwani.

Kaganda ameeleza hayo wakati akifafanua ujenzi wa miradi hiyo kwa wana habari,ambapo amebainisha jengo hilo la ofisi ya utawala limejengwa na wananchi kwa kushirikiana na halmashauri.

"tutatembelea ofisi za serikali ya mtaa zilizojengwa na nguvu za wananchi kwa kushirikiana na halmashauri bagara hapa ziwani"Kaganda.

Kaganda ameongeza kuwa mwenge wa uhuru utatembelea miradi 16 katika halmashauri zote za wilaya hiyo,ambapo miradi 8 mjini na mengine 8 vijijini.

Hata hivyo miradi mitano itawekewa mawe ya msingi,miradi mitano itazinduliwa na miradi mingine itakayosalia itashuhudiwa na mwenge wa uhuru.

Miradi yote katika halmashauri zote mbili za wilaya ya Babati imetumia takribani bilioni 10.

Mwenge wa uhuru utapokelewa Galapo katika halmashauri ya Babati vijijini.

Address

Negamsi
Babati
255

Opening Hours

Monday 05:00 - 00:00
Tuesday 05:00 - 00:00
Wednesday 05:00 - 00:00
Thursday 05:00 - 00:00
Friday 05:00 - 00:00
Saturday 05:00 - 00:00
Sunday 05:00 - 00:00

Telephone

+255684728971

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when SMILE FM TZ posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to SMILE FM TZ:

Share

Category