11/09/2025
Jina la kitabu hiki, Chakula ni Uhai na Chanzo Kikuu cha Migogoro ya Kiafya na Vifo vya Mapema, linafurahisha, lakini, pia linashtua na kufundisha wasomaji wake. Ni kweli, Chakula ni Uhai, maana kina kazi zake maalum katika miili ya binadamu. Hata hivyo, kitakuwa cha Uhai k**a kitaandaliwa vizuri, kitapikwa vizuri na kuliwa kwa kufuata kanuni bora nane za ulaji wa mlo kamili. Kwa upande mwingine, kitakuwa “Chanzo kikuu cha Migogoro ya Kiafya na Vifo vya Mapema,” iwapo kitakiuka kanuni hizo zinachoki fanya kilete afya njema na Uhai. Hii ni pamoja na kuharibiwa wakati wa maandalizi yake, mapishi yake na kuliwa vibaya. Kitabu hiki chenye Sura 18, kinatoa elimu muhimu sana kwa wasomaji kuhusu namna chakula kinavyotakiwa kiwe cha Uhai na namna kinavyoweza kuwa chanzo kikuu cha migogoro ya kiafya na vifo vya mapema. Chanzo cha magonjwa mengi yasiyoambukiza, yaani, magonjwa ya moyo, kisukari, figo, shinikizo la juu la damu n.k. ni chakula. Kwa hakika, upo msemo maarufu kuwa “Jinsi ulivyo, ni matokeo ya chakula unachokula na vinywaji unavyotumia.” Tunapendekeza kitabu hiki kisomwe na watu wote wanaotamani kuwa na afya njema na maisha marefu yenye furaha