28/10/2025
Kumbukumbu ya Watakatifu Simeon na Yuda, Mitume
Mtakatifu Simeon
Mtakatifu Simeon mtume, alizaliwa huko Yudea, Uyahudi, wakati wa utawala wa Warumi. Alikuwa pia ndugu wa Bwana Yesu. Alikuwa mmoja kati ya mitume 12 wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Tunaona anatajwa katika maandiko (Matendo 1:13, Luke 6:15, Mathayo 10:4 Marko 3:18) na alikuwa mmoja kati ya wanafunzi makini.
Tunaona pia baada ya Pentekoste, aliendelea kukaa Jerusalem pamoja na Yakobo. Na alipouwawa Yakobo, Simeon alikemea vitendo vibaya vya Wayahudi. Ikatokea machafuko ambayo yalisababisha Mtakatifu Simeon kukimbilia ng'ambo ya mto Jordan, katika mji mdogo ulioitwa Pella. Alirudi tena Jerusalem na kuchaguliwa kuwa Askofu
Lakini baadae naye alik**atwa akashtakiwa kwa kuwa mkristo na akahukumiwa kuuwawa. Baada ya mateso makali, akauwawa kwa amri ya Atticus, gavana wa Warumi.
Mtakatifu Yuda, Mtume
Mtakatifu Yuda mtume , alizaliwa Galilaya, Uyahudi, nyakati za utawala wa Warumi, katika karne ya 1. Alikuwa mwana wa Clopas.
Alikuwa ni kaka wa Yakobo mtume, pia alikuwa na undugu na Bwana Yesu, Alikuwa mmoja kati ya mitume 12 wa Bwana wetu Yesu Kristo. Katika maandiko tunamuona katika Luka 6:16, matendo 1:13, Yohana 14:22 , Mathayo 13:55, Marko 6:3 na Jude 1:1.
Baada ya Pentekoste, Mtakatifu Yuda alianza kuhubiri na kufundisha, katika miji ya Judea, Samaria, Idumaea, Syria, Mosepotamia, na Lyidia.
Alirudi Jerusalem mwaka 62, kumsaidia Mtakatifu Simeon ambaye alichaguliwa kuwa Askofu wa Yerusalemu.
Aliondoka tena akienda Armenia, ambako aliendelea na kumuhubiri Kristo. Mtakatifu Yuda nae aliuwawa kwa ajiri ya kushikiria imani yake huko huko Armenia, katika karne hiyo hiyo ya kwanza.
Mabaki yake pamoja na ya Mtakatifu Simeon yapo katika Basilica la Mtakatifu Peter huko Roma.
Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Abraham
Mt. Anastasia II
Mt. Anglinus
Mt. Eadsin
Mt. Faro
Mt. Ferrutius
Mt. Fidelis of Como
Mt. Godwin
Mt. Honoratus wa Vercelli
Mt. Joachim Royo
Mt. John Dat
Mt. Remigius
Mt. Salvius
Watakatifu Simeon na Yuda Mitume, Wenyeheri na Watakatifu Wengine wote wa Leo, Mtuombee.
www.radiombiu.co.tz